Reincarnation na rebirth ni kitu kile kile

Inakuaje mtu anaamini hivi haya mambo ambayo hayana hata maana.
I mean Reincarnation ndio nini hata mtu ajitahidi kueleza atakuwa anatupa opinion yake wala sio objective knowledge.

Ni aina fulani ya saikolojia ya kujifariji kwamba ukishindwa na maisha haya, utapata nafasi kwenye maisha mengine.
 
Ni aina fulani ya saikolojia ya kujifariji kwamba ukishindwa na maisha haya, utapata nafasi kwenye maisha mengine.

Inaitwa egoism ambayo tunayo kwaasili yetu tunataka kuishi kila siku na wakati uhalisia ni kwamba tutakufa. Sasa hii egoism ambayo inatufanya kutaka kuishi ina fanya projection ya kuwepo maisha mengine.nawakati hayapo.
 
Kiranga hebu nithibitishie kama gari linatumia mafuta ili kwenda, Kumbuka kuna lubricants dereva fuses battery wiring na vingine vingi, ukiona gari inatembea barabarani ni mkusanyiko wa vingi
 
Last edited by a moderator:
Kiranga hebu nithibitishie kama gari linatumia mafuta ili kwenda, Kumbuka kuna lubricants dereva fuses battery wiring na vingine vingi, ukiona gari inatembea barabarani ni mkusanyiko wa vingi

Umeshindwa ku critique argument yangu.

Sijasema gari linatumia mafuta tu, nimesema linatumia mafuta.

Na ukutaka uthibitisho endeaha gari linalotumia mafuta mpaka mafuta yaishe halafu uone kama utaweza kuenelea kuendesha kwa kutumia lubricants na vingine vingi.

Na mafuta yanaonekana, yanapimika.

Hiyo roho na nafsi iko wapi, inaonekanaje na inapimkaje?

Na kama haionekani na kupinika, utatuthibitishiaje kwamba roho au nafsi zipo na si hadithi tu?
 
Last edited by a moderator:
Hakuna reincarnation wala rebirth. Huo wote ni ushirikina tu.

Oh no sio ushirikina tu bibi ni MAKUNYANZI
a.k.a wrinkles kuanzia kwenye mishavu yako iliyochoka kwa ajili ya kiherehere + wivu wa kizee, hadi huko uvundoni kwako!

To hell with you bi kidudeo!
 
Ndio maana SIKU ya kwanza kumuona Obama nilimshangaa sana akili iliniambia kuwa nilishawahi piga story na yule sela....kumbe yawezekana reincarnation imetake place.
Mmmh ila hayo masomo ni magumu sana
 
Oh no sio ushirikina tu bibi ni MICHIRIZI a.k.a wrinkles kuanzia kwenye mishavu yako iliyochoka kwa ajili ya kiherehere + wivu wa kizee, hadi huko uvundoni kwako!

To hell with you bi kidudeo!

Umeshindwa kujibu unaanza kuhororoja na kubwabwaja bila mpango.

Uvundoni usingekujuwa bila kuwa umepanusa kwa mama'ko.
 
Umeshindwa kujibu unaanza kuhororoja na kubwabwaja bila mpango.

Uvundoni usingekujuwa bila kuwa umepanusa kwa mama'ko.

Haa haa umepaniki eeh bibi kizee unayetaka kufia mikononi mwa viserengeti boys!

By the way tulia hivo hivo sindano ikuingie kwenye hivo vitako vyako vilivyolendemka ka mlenda!
 

Lakini mafuta sio energy, jaza gari mafuta Halafu utoe battery au fuses nk uone Kama litaenda
 
Kiranga hebu nithibitishie kama gari linatumia mafuta ili kwenda, Kumbuka kuna lubricants dereva fuses battery wiring na vingine vingi, ukiona gari inatembea barabarani ni mkusanyiko wa vingi

Nashangaa :whistle:-- mbona ipo namna ya kumjibu Kiranga ama kuzungumza naye lakini daima huwa mnashindwa?

Hmmm

Kwanza hili ni wazi : mazungumzo na mashauri yote ya namna hii yaweza kuwa ni gumzo tupu...

Kuwa kwake namna hii inamaana yote yanayozungumziwa na kujadiliwa hapa hayatupeleki popote ila kuishia humu humu. Hili kwangu mimi kama mtu, ni jambo lisilo na thamani yoyote na basi sijisikii kulazimika kwa namna iwayo yoyote ile kuwa sehemu ya 'gumzo'...

Ila...

Unakuja wakati ninajisikia kujifurahisha kwa lolote kadri nijisikiavyo na hivi ndivyo ninavyofanya.

Kuna namna mbili za kuonekana kama vile kuelekea kuyafikia 'maarifa'; (i) namna kanushi (ii) namna kubalishivu....

Namna kubalishivu ndiyo ya kwanza na yenye kutawala, hiyo ya kwanza huja kutokana na hii ya pili.

Namna kubalishivu ni nyingi ya ahadi-- labda uweza na mawezekano... Namna kanushi ni isiyokujali yote yajayo na namna kubalishivu.

Mashauri ya Mungu huangukia upande wa namna kubalishivu, ila 'shauri la mungu' linaweza kuonekana kama dhana katika mashauri tu; mashauri si ukweli hasa ila namna fulani 'muakisiko' wa hiyo yenyewe kulingana na vipawa vyetu kuzitafsiri habari za milango yetu ya fahamu.

Katika hali ya kawaida ya mashauri na majadiliano, mimi kama mtu pia ninapenda kuchukua upande wa namna kanushi. Kwa kuwa mashauri tu bila ushahidi wa nguvu na ishara zaidi kwangu ni ubatili. Vile vile yale yote yanayoonekana kwangu kama dalili ya 'ushamba' ama kutojua mambo katika sura ya kheri kamili kwangu pia ni ubatili -- haijalishi yanakuja kwa sura gani, mapokeo ya imani, dini ama kasumba tu ya kiutamaduni, mila na desturi. Katika hali ya kawaida mimi kama mtu, sina mapenzi na dini za mapokeo, desturi 'pofu' za kimakundi...

Lakini...

Kwa kuwa, mtu akiacha mambo batili na kuanza kuchunguza yote kwa faragha yake -- mengi yanawezekana ambayo si wazi kwa makundi ya watu; basi kwa neema, yapo ambayo kwangu mimi kama mtu yanafanyika na kuendelea na yasiyo na ushirika na mengine yaliyotamalaki ila ikibidi kushiriki -- kheri yake itajibayanisha na hayo. Kwa hivyo, ufanyapo bidii kuyang'amua yajayo na utayari wako wa kipekee, usiwe na shauku la kupenda ama kudhani mwingine ndiye atakayethibitisha ubora wako...

Niamuapo kusimamia upande wa namna kubalishivu, mimi kama mtu nina ujumbe na nina kusudi. Ni wakati wa kujaribu kufunua jambo ama mambo, sitajarajii wala kutegemea nitaeleweka mara moja; sitarajiii kama nitaaminika kwa kuwa haya si kusudi lenyewe hasa. Kusudi limo kwenye nia yangu tu kwamba ninataka kujitahidi kuwa wa msaada katika yule ama wale wanaoelekea kutambua ni nini kinafanyika na kuendelea...

Namna kubalivu ni muktadha wa mabadiliko yasiyokoma -- kujinasibu na mabadiliko kwa kheri zaidi. Kama ni ubora basi kwa matunda ya jitahada ni wale waliokusudika tu ndiyo watakaong'amua kinachoendelea... si kila mtu mwenye macho anaona, na si mwenye masikio anasikia... Ipo namna habari njema huwafikia wale tu walio na nasibu ya kuipokea na si vinginevyo.

Ikiwa hujijui wewe ni nani, daima utayumbishwa na yale yanayotegemea makusudio yako dhaifu ama kutokufaa katika mapana ya kheri na jaala yako. Katika kuitafuta njia iliyosahihi, namna yake si sawa na 'hekima' ya duniani. Duniani kuna ujuaji, kuna kushindana, kuna kupigana na kujidhirisha eti wewe ni nani... Katika faragha yako ya nafsi na roho, huna chochote cha kupambana nacho ila wewe mwenyewe...

Sasa, mtu yeyote na asihangaike kumjibu mwingine ili kwamba ajione yeye ni mwenye kujua. Na ikiwa utafanya hivyo bakisha sehemu katika nafsi kujiambia kwamba wafanya la namna hiyo kwa ajili tu ya mazungumzo lakini ikiwa hakuna tija yeyote, ya maana zaidi -- achana na shauri la jambo husika.

Namna kanushi na namna kubalishivu ni mbili katika moja, ipo kweli yake, ipo haki yake...

Sina mpango wa kunata na 'via negativa' ya Buddha kwa sasa, ila ndiyo ni kweli hasa; mwishoni mwa yote ni Buddha.

Ila 'via pozitiva' ipo kwenye muktadha wa dhamma na pia kitu ambacho hapa kitasubiri zaidi -- hekima juu ya kile katika mafundisho ya Buddha huja na mashauri ya 'Sambogha kaya'.

Mdadisi yeyote na achunguze -- ikiwa Buddha alikanusha kuhusu 'Sonafi', je u-Bodhisatva unawezekanaje?

Buddha ni starehe ya mwisho, kama hujayaiva ya 'ma-Avatara', Buddha inakupasa kumsikia kwenye bomba tu, haha.

Hmmmmm
 
mose usitumie neno kushindwa kwakuwa kila mmoja ana jinsi yake ya kujibu kulingana na maono yake na uamuzi wa namna ya kujibu
Unaweza kumjibu mtu kwa njia fupi rahisi na ya kueleweka AU unaweza kumjibu mtu kwa njia ndefu yenye uchambuzi wa kina kwenye jambo husika
Na hii yote Inategemea mtiririko wa mada husika na uelewa juu ya kile kinachojadiliwa..
 
Last edited by a moderator:

Haya, ninalichukua neno lako kwa kuwa unaniomba nifanye hivi...

Japo ninaona kama -- Kiranga kama mtu 'anawashika' hasa.

Kiranga mimi ninamsubiri kumuonesha vitu fulani na siyo kumtangazia dini.

Ila 'nimejitambulisha' kwake kwa namna inayofaa -- labda siku za toka awali sana.

Ila ningefurahi kuona silika kama ya Kiranga kwa wajumbe wengi humu; kwa maana kuna mambo ya kiufundi hasa kuweza hata kushiriki na watu, ila yanataka kweli mtu/watu (w)anayejifikirisha hasa -- na kutambua wakifanyacho.

Tunahitaji kusonga mbele zaidi ya mawazo na mawaidha ili kujinasibu uwezo hasa wa kuashiria kana kwamba kuna kitu chafanyika na kuendelee ndani yetu.

Tunahitaji kuhamisha ufundi wetu wa mawazo katika vitendo, kufaa ustaarabu na ustawi wetu.

Upo uwezekano wa kuleta mapinduzi katika tekinolojia, mimi kama mtu nitaanza na 'Nishati Bure' na mifumo/makinika pepetua, hichi ambacho hata katika uzi huu mmegusia kufungumanisha ya mashauri ya Mungu--mmejiandaa kusikia, mmejiandaa kujua... Lakini siku moja Kiranga, akipenda, nitaelekezana naye na hata katika kazi ; kuhusu nasibu za 'telepotia' na mawasiliano yasiyotumia 'umeme/sumaku'.

Hmmmmm
 

Tunaenda vizuri sasa... Kwa afya ya mjadala huu naomba nilete picha hii na vidodoso vyake vyote kama vilivyoainishwa kwenye muktadha wa mduara mzima katika uhalisia wake
Tujadili hili kwa Lugha nyepesi kila dodoso na kila kipande kwenye huu mchoro... Waweza angalia tuanze na kipi
 

Pamoja na maelezo marefu mazuri...

Hujathibitisha kwamba nafsi au roho ipo.
 
Pamoja na maelezo marefu mazuri...

Hujathibitisha kwamba nafsi au roho ipo.

Hataa...

Maneno mengi ama machache, sina hamu ya kukujibu ama kukueleza lolote...

Wewe una wakati wako sahihi kukutana na mimi, hapa nisome -- uniulize ukipenda; japo nitapima ikawa yafaa kukujibu ama la. Lakini usitarajie mimi kukuthibitishia lolote kama mashauri matupu.

Ila kuna kitu kimoja ninaweza kukudodosea... Namna yako ya mdahalo haina tija hasa; kuna vitu haijalishi umekuwa ukifuatilia huku ama kule, bado hujaweka sawa akilini mwako. Ninaviona lakini sina mpango wa kuvinyooshea vidole kwa sasa, ila kuna namna fulani ukijiweka -- moja kwa moja nitakuonesha na wewe utaaamua kama namna hii ya kuiingiliano vitendo ina maana ama haina.

Kwa mfano hilo unalouliza, sitakujibu -- ila nitajibu kupitia wengine kadri nitakavyoona kufaa na kupenda.

Bado haujajiandaa kupokea yale ya muhimu sana ambayo ningependa kushiriki -- nikilazimisha uta dhalilisha jitihada ni hilo halitakuwa jambo zuri. Unahitaji nidhamu fulani ila hiyo kwako bado haijafanyika.

Wewe una kitu kimoja, sioni mwingine yeyote humu ndani ya JF mpaka leo ambaye anaweza kuja kunielewa itakapofika wasaa wa kuzungumza kuhusu 'vitu' kuwa hapa, na kuhama kuwa pale, pasipo 'kusafiri' katikati... Ila, laiti ungelijua! Hili unalohoji ndilo linalowezesha hilo -- jua kwamba roho ipo, sonafi ipo ...

Ni katika mazingira fulani, Mtu kama Buddha yuko sahihi kusema hakuna 'sonafi'... Lakini jiulize tu labda Bodhisatva, ni sehemu ya mtu anayejaalika kuwa 'Buddha'... Basi, Boddhisatva ni muktadha ule ule wa 'Sonafi' ila ipo haki yake, ndiyo maana taarifa husema mara nyingi Buddha alipozungumza hili wapo waliomuuliza moja kwa moja--sasa si ndio sonafi hiyo(?) Husemwa ilipokuwa ikifikia hapo Buddha alikuwa 'anakausha'... Anakaa kimya. Sasa maana yake jiongeze mwenye.

GI Gurdieff, alikuwa anasema mtu hana 'roho/sonafi' mpaka aifanye hiyo katika yeye... Sasa ukijongeza katika haya mawili utajinasibu kujua kitu kama vile, muktadha wa 'sonafi' upo isipokuwa kama ilivyo kwa Buddha na Gurdieff, wa kwanza anakanusha kwa sababu hataki chochote cha kuhusika na mtu asiyenasibika kuelekea 'Taamuli'... Wa pili ananasibisha jitihada za mtu kuwa 'Bodhisatva'...

Humu katika huu uzi bado wanamashauri kuotea hata usawa huu wa maarifa na hekima yake. lakini In Shaa Allah, tuombe kheri, maarifa yaendelee kupenyeza...

ooops, nimekujibu sijakujibu (?)

Hmmmm
 

Huna hamu ya kunijibu wala kunieleza lolote wakati unajaribu kunijibu na unajaribu kunieleza mambo?

Unajua kama unakwenda ama unarudi?

Namna yangu ya mdahalo haina tija hasa kivipi? Wewe unajivika vipi uamuzi wa kwamba namna gani ya mdahalo haina tija? Au kwa sababu umeshindwa kujibu swali tu unasema mdahalo wa aina hii hauna tija? Na kama hauna tija kwa nini unaendelea kushiriki?

Kama kuna vitu sijaweka sawa akilini mwangu unaviona lakini hutaki kuvionyeshea kidole, huoni hapo kwamba wewe kauli yako hii ndiyo haina tija? Na zaidi ya kukosa tija, haionyeshi uthibitisho na inaweza kabisa kuwa ni chaka la kujifichia unalotumia ili usinibu maswali?

Mimi nahitaji nidhamu? Wewe unayekataa majibu kwa kusema namna yangu ya mjadala haina tija bila maelezo huhitaji nidhamu?

Wewe unayesema kuna vitu sijaweka sawa bila kuthibitisha, kuvitaja wala kuelezea zaidi, huhitaji nidhamu?

Unaweza kuthibitisha kwamba roho/nafsi ipo?
 





 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…