Reincarnation na rebirth ni kitu kile kile

Reincarnation na rebirth ni kitu kile kile

Nakumbuka novel ya across the bridge....

1444709519773.jpg
 
Nimengojea kuona ikiwa kuna mtu yeyote anaweza kuotea mahala sahihi pa kuuliza juu ya 'Uzaliwa Upya'(?)...

Ila wacha nijifurahishe...

Ipo sehemu katika 'nafsi-roho' -- kama saikia ya mtu; hiyo ni yenye kudumu zaidi kupita mauti ya mwili. Kwenye tundiko langu la kuingilia uzi huu nimemulika hilo...

--- Kuna gumu moja kuliotoea ili kuling'amua ukweli wake, je, ni kwa nini katika mapokeo ya Ubuddha hakuna jambo la 'Sonafi' kukubalika kama muktadha wa uzima na uhai wa mtu ama kiumbe (?)

Sehemu ya mapokeo ya ilimu ya 'Uamkaji' kiroho huzungumzia jambo la mtu kutoweza kufikia 'fahari' ya uzima zaidi na mambo ya miili ya kiroho pasipo yeye 'Kuzaliwa Mara ya Pili'... Je, kuzaliwa mara ya pili, kama vile Yesu pia alipata kuulizwa na wafuasi wake. ni jambo lile la kurudi katika 'tumbo' la mwanamke (?) Yesu alikanusha, na akagusia shauri mbadala -- Je, 'Uzaliwa upya' ni basi wafaulika kwa namna ipi?

Uzaliwa wa kwanza ni namna ya 'Utwaaji Mwili' hapa ama kule; Wa pili, Mpya, ni namna ya kufanyika 'kiumbe kipya'... Hapa ni pa kuotea uwezekano wa fahari ya namna mpya ya maumbo na uzima... Kwenye mapokeo ya mafundisho ya Yesu, Ni mtu anayefahamika kwa jina la Paulo alikuwa Msikirifu mwenye kuzungumza vema juu ya siri za 'fahari ya miili ya Kimbingu' -- Kwamba Kristu ni fahari zaidi ya mwili wa mauti. Mwenye kheri anaweza kuotea ya msingi kutoka kwa Paulo...

Kwenye Mapokeo ya Ubuddha, kama yale ya Kitibet, huzungumzwa ya mtu kuzaliwa upya na kupata kuitwa 'Djwal' -- 'Mwenye kuzaliwa mara mbili'... Ni jinsi gani muktadha wa mafundisho ya Yesu yanafanana na mafundisho ya taasisi nyingine ya mapokeo ya Kiimani? Hili linapasa kutukumbusha sote umuhimu wa kufanya visomo linganishi kwa maarifa yote yakiwapo haya ya dini, imani na mapokeo... Labda haya ni yenye kufanana, kuingiliana na hata kukamilishana zaidi...

--- Gumu jingine litakuja na swali la kugusia ikiwa 'nafsi' hufungamana na 'dhana za mungu' na 'madhahiriko'... Katika Ubuddha hakuna 'suala' la mungu (?) Je, suala hili 'limechomoka' vipi katika maarifa na hekima ya mapokeo ya Kibuddha?

Kuna mengi tunadhani tunajua lakini ukweli unaweza kuthibitishia kuwa hatujui ile hasa; ila kama vile Paulo alivyopata kusema:

[SUP]"[/SUP][SUP]11 [/SUP]Nilipokuwa mtoto mdogo, nilisema kama mtoto mdogo, niliwaza kama mtoto mdogo, nilifikiri kama mtoto mdogo. Nilipokuwa mtu mzima niliacha mambo ya kitoto. [SUP]12 [/SUP]Kwa maana sasa tunaona sura kama ya kwenye kioo, lakini wakati huo tutaona uso kwa uso. Sasa nafahamu kwa sehemu, wakati huo nitafahamu kikamilifu, kama vile ninavyo faha mika kikamilifu."

Lakini kabla ya hili, hili pia ni shauri la muhimu kulitilia maanani:

"
[SUP]6 [/SUP]Lakini miongoni mwa watu waliokua kiroho, tunafundisha maneno ya hekima, hii si hekima ya ulimwengu huu au ya watawala wa nyakati hizi ambao watatoweka. [SUP]7 [/SUP]Hekima tunayofundisha ni hekima ya siri ya Mungu ambayo imefichwa kwa wanadamu, na ambayo Mungu aliipanga kabla ulimwengu kuwepo, kwa ajili ya utukufu wetu. [SUP]8 [/SUP]Watawala wa nyakati zetu hawakuielewa hekima hii. Kwa maana kama wangeliijua, wasingalimsulubisha Bwana wa Utukufu.

[SUP]9 [/SUP]Lakini, kama Maandiko yasemavyo, "Hakuna aliyeona, hakuna aliyesikia, hakuna aliyewaza, kile ambacho Mungu amekiandaa kwa ajili ya watu wampendao." [SUP]10 [/SUP]Lakini Mungu amekidhihirisha kwetu kwa njia ya Roho wake. Roho huchunguza kila kitu, hata mambo ya ndani ya Mungu. [SUP]11 [/SUP]Kwa maana ni nani anajua mawazo ya mtu isipo kuwa roho aliye ndani ya huyo mtu? Vivyo hivyo hakuna mtu anayeelewa mawazo ya Mungu isipokuwa Roho wa Mungu. [SUP]12 [/SUP]Sisi hat ukupokea roho ya dunia hii bali Roho aliyetoka kwa Mungu ili tuweze kuelewa yale ambayo Mungu ametupatia bure. [SUP]13 [/SUP]Haya ndio tunayozungumzia, lakini si kwa maneno tuliyofundishwa na hekima ya wanadamu bali kwa maneno tuliyofundishwa na Roho, nasi tunafa fanua mambo ya kiroho kwa watu wa kiroho. [SUP]14 [/SUP]Mtu ambaye hana Roho wa Mungu hawezi kupokea mambo yanayotoka kwa Roho wa Mungu kwa sababu mambo hayo ni upuuzi kwake; na hawezi kuyaelewa kwa kuwa hayo yanaeleweka tu kwa msaada wa Roho.
[SUP]15 [/SUP]Mtu wa kiroho anao uwezo wa kupima kila kitu, lakini yeye hapimwi na mtu. [SUP]16 [/SUP]"Kwa maana ni nani amefahamu mawazo ya Bwana ili apate kumshauri?" Lakini sisi tunayo nia ya Kristo."

Hmmm
 
Bujibuji nafsi kwa kiingereza ni 'self', nafsi hukaa kwenye mwili ulio hai, kinyume na hapo hakuna nafsi, kwakuwa nafsi huletwa na muunganiko wa roho + mwili
Roho huwepo hata baada ya kifo, na huweza kuhama na kuingia kwenye mwili mwingine -reincarnation
soul ni nini na spirit ni nini?
 
Imekuwa ikiongelewa mara kwa mara kuhusu uwepo wa roho kwenye miili mipya izaliwayo au suala la kuzaliwa upya kwa ujumla, lakini baadhi ya wengi wamekuwa wakipinga suala hili. Kuna ukweli wa asilimia nyingi tu kuhusu suala hili lakini wapo wasiomini, hatushangai kutokuamini kwao kwa sababu wapo ambao hawaamini hata kama MUNGU yupo sasa mtu kama huyu huwezi kumlazimisha na wala huwezi kumbadilisha hata kidogo kwa sababu ilishasemwa kunako maandiko matakatifu kuwa huwezi kuubadilisha unywele mmoja kuwa aidha mweupe ama mweusi, LAA [ MATHAYO 5 : 36 ].


Hebu tutazame au tujiulize suala moja ya kwamba ; kuna kitu kinaitwa BIRTHMARK. Kuna baadhi ya vizazi walishafanya zoezi la kuwaweka MARK wapendwa wao wa karibu ambao walikaribia kufa unajua nini kilitokea…?, ilitokea kuwa walizaliwa watoto wakiwa na zile MARK ambapo ilipelekea kuwa ni moja kati ya evidence that the soul has been REBORN.

Na pia, kuna watu ambao walikufa wakiwa na majeraha ya risasi kwenye miili yao, sasa kwa watu wenye kufkiri kwa GREAT THINKERS walifanya tafiti za kina juu ya hili, japo wengi hawajui watu wanapozaliwa kwa nini wanakuwa na vitu kama SCARS au hata BULLET WOUNDS na vitu kama hizo ila kwa tafiti ambazo tayari zimekwisha fanywa tayari watu wame-connect DOTS kuhusu hizi mambo na ku-prove kuwa the soul has been REINCARNATED.

Inaweza kuwa ni ngumu kuamini lakini ukweli ni kwamba, alishatokea mwanamke ambaye alishakufa then baada ya REBIRTH ikatokea kuwa akaja kuolewa na mwanawe ; UNATAKA KUJUA ILIKUAJE...?.

mshana jr anajua hii kitu.
 
soul ni nini na spirit ni nini?

Soul(psyche) na spirit (pneuma) ni vitu vinavyochanganya wengi, lakini spirit ni sehemu ya roho, ambapo spirit ilihusishwa na Mungu(imani) zaidi angalia hizi picha
 
Hii michoro rahisi sana, lakini kila nikiitazama naona eitha inanichanganya au inanifanya nichanganyikiwe, nadhani nahitaji darasa maalum, nifundishwe taratibu na kwa hatua, nadhani hata wewe hii kitu ilikuchukua muda ndipo ukaijua vizuri
Bujibuji wewe ili uwe Bujibuji unatengenezwa na vitu vitatu kwa kiingereza tunaita ME MYSELF n I, kikikosekana kimojawapo hakuna Bujibuji bali kuna roho ya@bujibuji au mwili wa Bujibuji
Ili mwanadamu akamilike anahitaji mwili roho na nafsi (self, body n mind/me myself n I) 1444797645378.jpg tukirudi kwenye swali letu LA awali utaona kuwa roho ndio kiunganishi cha body n spirit 1444797765839.jpg lakini hapohapo ili upate moyo unahitaji vitu viwili soul n spirit...
Labda ni vitu vinavyojichanganya Sana lakini ukirudia kusoma kwa utulivu utaelewa
 
Last edited by a moderator:
View attachment 298632 Kiranga tukiacha ushabiki kando hebu tujadili huu michoro picha

Kwa ninibunasema "tukiacha ushabiki kando"?

Nani analeta ushabiki?

Unaweza kuthibitisha kwamba roho ipo?

Mchoro mtu akiweza kuchora ngazi isiyo na mwisho, hilo lina maana kuna ngazi isiyo na mwisho?
 
Last edited by a moderator:
Kwa ninibunasema "tukiacha ushabiki kando"?

Nani analeta ushabiki?

Unaweza kuthibitisha kwamba roho ipo?

Mchoro mtu akiweza kuchora ngazi isiyo na mwisho, hilo lina maana kuna ngazi isiyo na mwisho?

OK tujadili hivyo vitatu katika uhalisia wake nafuta neno 'ushabiki'
 
Energy inajulikana na kupimika, sijauliza energy.

E=MC squared.

Nimeuliza roho, roho ni nini? Unaweza kuthibitisha kwamba ipo?

Roho ni energy na sikubaliani nawewe hata chembe Kiranga kuwa energy inapimika
Ni kwa mfano nikikuuliza kuwa ni kipi kinafanya gari litembee au mashine yoyote ifanye kazi...kwa hakika hutakuja na jibu moja na hapo ndio maana halisi ya energy inapokuja
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom