Hotuba ya papa iliyoishtua Dunia. Hakika huyu ni mtakatifu kweli kweli

deblabant

JF-Expert Member
Oct 7, 2022
901
1,334
HOTUBA YA PAPA FRANCIS ILIYOSHITUA DUNIA

Tafadhali soma hotuba ya Baba Mtakatifu.
Bila kujali dini yako, ona jinsi Papa Francis alivyoandika vyema kuhusu familia.

FAMILIA NI MAHALI PA MSAMAHA, ...

©️ Hakuna familia iliyokamilika.

©️ Hatuna wazazi walio wakamilifu,
- hata wewe mwenyewe siyo mkamilifu.
Hatufungi ndoa na mtu mwenye ukamifu na wala hatupati watoto wenye ukamilifu.

©️ Tunashutumiana wenyewe kwa wenyewe. Hatuwezi kukaa pamoja bila kukoseana.

©️ Mara kadhaa huwa tunavunjwa moyo. Ndiyo. Kuna sababu na mambo mengi yanayo wavunja moyo wanafamilia wenzetu katika nyakati mbalimbali .

©️ Hakuna ndoa yenye afya, au familia imara bila kuwa na utaratibu wa kufanya mazoezi ya kusameheana. Msamaha ni dawa inayoleya raha na furaha katika familia.

©️ Msamaha ni muhimu kwa afya ya akili na uhai wa kiroho. Bila kujali ukubwa wa kosa, au mkosaji; familia iliyokosa msamaha inakuwa makao ya ugomvi na ngome ya shetani na maovu.

©️ Bila msamaha, familia inapata ugonjwa na inakuwa na afya mbaya.

©️ Msamaha ni utakaso wa roho, husafisha roho na huleta uhuru na amani moyoni. Hakuna dhambi yenye ukubwa hadi kutostahili msamaha. Mtu asiyesamehe hana Amani rohoni mwake na hana ushirika na Mungu.

©️ Kutosamehe ni UOVU na sumu inayonwathiri na kumuua mtu asiye samehe.

©️ Kutunza maumivu ya roho kwa kutosamehe ni kujiharibu wewe mwenyewe. Ni kujitafuna wewe mwenyewe .

©️ Wanafamilia wasiosamehe wana ugonjwa wa kimwili, kihisia, na kiroho. Na wanaugua kwa namna mbili.

Kwa sababu hiyo, familia lazima iwe sehemu ya uhai badala ya kuwa sehemu ya kifo; mahali pa msamaha, paradiso na siyo jehanamu; mahali pa uponyaji na siyo magonjwa; sehemu ya kufanyia mazoezi ya msamaha na siyo mahakama ya kuwatia watu hatiani.

Msamaha huleta furaha mahali penye huzuni; huleta uponyaji mahali penye ugonjwa .

Familia ni mahali pa msaada na siyo mahali pa umbea na masengenyo baina ya wanafamilia family. Familia inapaswa kuwa sehemu ya kukaribishana badala ya kukataana. Aibu iwapate watu wanaopanda mbegu ya ufitini. Katika familia sisi ni wanafamilia na si maadui.

Wakati mtu anapopata matatizo na changamoto anachohitaji ni msaada.

¤ Kutoka kwa Baba Mtakatifu Francisco

Tafadhali peleka ujumbe huu kwa familia zote unazozifahamu. Unaweza kusaidia kuponya familia zenye majeraha na kuzipatanisha.

Tunapaswa kuwapokea watoto wetu wanaoathirika na dawa za kulevya na pia kuwaongezea upendo.

Muwe na siku njema.🙏🏽
 
Niilidhani umeshtuka pengine ameruhusu walawiti watoto waliopo kanisani wafukuzwe makanisani
Umenishtua Unavyojiita kishetani kabisa??
Unamkufuru Mungu kabisaa??
Wewe ni Pumbafu ulitakiwa uleburn humu!
Hufai kujadiliana humu!!
 
Ujumbe mathubuti na mujarabu kabisa.

Ila wasabato hatupendi kusikia Baba Mtakatifu (Baba mtakatifu ni Mungu).
 
Ujumbe mathubuti na mujarabu kabisa.

Ila wasabato hatupendi kusikia Baba Mtakatifu (Baba mtakatifu ni Mungu).
Baba mtakatifu siyo lazima awe mungu hata wewe ni baba mtakatifu nyumbani kwako mana watoto wanatumzwa kikamilifu
 
Hotuba zenyewe unaandaliwa yeye ni kusoma tu

Siyo kweli. Mfumo wa kanisa, toka kale hauruhusu mdogo kumwandalia waraka mkubwa. Hayo yapo Serikalini.

Kwa upande wa Kanisa, ni mkubwa pekee ndiye anayeruhusiwa kuandaa waraka kwaajili ya mdogo ili kwenda kuwasomea waumini.
 
Back
Top Bottom