Ndiyo kaka.
Tawire.
Si uchambuzi hasa ila ni tafsiri kutoka mahala palipo tanguliwa kutajwa.
Dhana ya Utwaaji Upya Mwili, ni zaidi ya nadharia -- kwa maana humu bado ni shauku na udadisi wa kimawazo unahusu... Leo tunazungumza humu; kesho, mimi na wewe; yule na yeye -- tutaketi ukumbini halafu tutafanya yale yenye kuweza kuleta maono na njozi za asili moja hata ingine.
Haijalishi mtu kuamini ama kutoamini katika utwaaji upya mwili, mtu yeyote anaweza kupatiwa mazingira ya kung'amua hili katika yeye... Lakini namna ya kujua yaliyo katika nafsi zetu zingine, mahala pengine, wakati mwingine -- mbele ama nyuma ni hali yetu ya kawaida kabisa... Akili ya kubaini hili kidogo ndiyo namna yake ni tofauti na ufikirifu wetu kuhusu 'ukuwa wetu' na 'nafsi'.
Namna inayohusika na sisi kuwa hapa, kuwa kule -- wakati huu ama ule una makanika yake ambayo mtu katika hali ya kawaida aweza kushindwa kutambua maana yake; japo kuishi kwetu na kuyamudu maisha kwa ufanisi wa namna mbalimbali, ni 'matunda' na 'ishara' ya siri ya 'utwaaji upya mwili'.
Mimi kama mtu ninapenda kushiriki mashauri yanayojenga msingi wa mawezekano bora zaidi ya ustawi na ustaarabu wa mtu. Tu(n/t)ayaangalia haya kwa kuwa, ndani yetu sisi tunayo silika ya kupenda ama kutaka kujua ni wapi tulipotoka na ni wapi tunakwenda... Je, Wakati ni kitu gani katika sura ya harakati zetu -- siku hadi siku (?) ... Kiu yetu ya kukua, kustawi na kufurahi zaidi yatutaka kuweka muafaka kati ya maarifa yetu, uzoefu wetu na hakika ya mema... Mawili haya ndiyo mihimili ya uadilifu wa mtu katika tamaduni na ustaarabu... Dini zote ziko na watu ili tukatisha majibu ya watu na jaala zao -- kwa kuinyonya misingi ya hofu na ujinga katika mtu. Hata Mungu, kwa wengi ni fumbo -- lakini dini limeziba pengo la kiu na haja ya mwanadamu kwa kuleta mifano ya picha nyingi kuhusu Uwepo wa mungu aliye hivi ama vile, aliye huku ama kule... Mwamuzi wa hatma ya mtu kuwa na kwenda huku ama kule... Lakini yote yaliyopata kusemwa juu ya mungu, ni hiyari ya mtu kuyakubali ili kumtawala ama kuachana nayo na basi kurudia katika hamu na kiu yake ya kutatua fumbo...
Yote ambayo yamepata kuzungumzwa kwetu ama miongoni mwetu kuhusu Mungu, mbingu na nchi, akhera na kuzimu -- vyaweza kuwa ni muakisiko wa sehemu fulani ya ukweli katika maisha na labda tena -- katika tafakuri ya mtu. Lakini maisha na ufunuo ndiyo taamuli ya hakika ya mtu katika mapito na ubarikika wake.
Amebarikiwa ni mtu asiyeshikwa na hofu katika kuyachunguza yote na tena hata yeye mwenyewe.
Amebarikiwa ni mtu mpole katika kubaini ukungu katika jicho lake na basi kuyasafisha macho yake.
Amebarikiwa ni mtu mwenye moyo na nia safi, kwa maana huyu njia yake ni nyoofu kuuelekea ukweli...
Sasa tuseme, haya yote tuliyopata kuyasikia yamekuwa ni sehemu ya ukweli iliyo ni siukweli, tutapojifanya kuwa kamili zaidi basi tujua ilivyobora zaidi...
Yapo mambo mengi -- hata pasipo idadi -- katika ulimwengu kuhusiana na madhahiriko na mbegu zake... Kuyabaini hayo kwa namna yenye kheri, ni kutambua kiini cha 'hadhi' na 'sifa' za sura na maumbile ya vitu. Mtu unaweza kuanza kulipa nafasi hili, akilini mwako; labda tunavielewewa vitu, jambo na mambo kwa kudra ya mfananishano na milingashano; pia yawezekana kuwa na hakika ya kwamba 'ukubwa' na 'hadhi' ya kitu ni nusu ya nje ya jambo linaloweza kuwa limefichama nje ama ndani ya kingine...
Mungu ni dhana duni iliyofaa siku za zamani ya kupendelea kuona 'fumbo la uzima' ni mfano wa mtu mwenye mamlaka, mtu mwenye nguvu, mtu mhifadhi... Kwa kuwa mtu wa zamani, alifaa kwa upeo na kina cha kizamani. Kadri sasa tunaingia ulimwengu wa maarifa kuongezeka, watu wote hawana budi kujiongeza ili kuweza kulitambua fumbo la uzima katika kheri na mapana ya maendeleo ya leo.
Mungu toka sasa, kwa watu atatambulika kama (i) hadhi ya mtu na si mtu hasa (ii) Sifa akili inayotawala kuendesha maumbo yote na kuyahifadhi huku yakitanuka na kusinyaa kwa namna zake anuai (iii) Pumzi ama nguvu uhai iliyokote na mote... Vitu vyote vipo katika mungu na mungu yumo katika kila kitu.
Zama hii -- nakuelekea mwishoni kwa karne hii hasa, tunaelekea kwenye vilele viwili ya kiustawi na ustaarabu, Kwanza, tutaingia kipindi ambacho tutagundua mbinu nyingi za kupata nishati ama tuseme kufua vitendo kazi visivyokoma ; Pili, tutasonga mbele sana katika mifumo ya tekinolojia za habari, mawasiliano na uthibiti; hata kwenye kufikia uwezo wa kuintafesi (kuunganisha kiufundi na matumikizi yake) uelekitronishi umeme na mwanga na akili zetu... Sasa haya mawili yatawezekana kama uthibisho wa haya yalitajwa kwa kutangulia kuhusu umahala pote pa akili na uweza wa nguvu, zamani tukiishia 'kumuachia mungu' wa kudhanika kiusadikifu.
Mambo makubwa tunaelekea kuyafanya; lakini kwa yeyote -- asije kusema itakuwa ni 'miujiza' -- maana yote yanawezekana kwa yule mwenye imani katika hakika.
Basi na mimi ninachukulia uwepo wangu katika mashauri ya namna hii, hata humu JF, ni katika kusaidia wale walio tayari kuuingia ulimwengu ambao sayansi na imani vyawa kitu kimoja, hatimaye. Siyo kila mtu ana utayari; ila wengine itachukua muda mpaka waje waone mawezekano mengine mapana ya kifanywa na wenzao yasiyoelezeka ila tu kwa kushuhudia kile ambacho wao akili zao bado ni nzito na mioyo yao vile vile.
Injili ya Zama za Ndoo ya Yesu ni kitabu bora kabisa, ninashauri kila aliye na moyo mkunjufu akipitie kwa maana, mashauri yake mengi yamesheheni hekima na maarifa kuhusu kutaniko/ingiliano la viumbe, uhai na uzima wake ndani na nje yake.
Na hapa ninatafsiri sehemu ya pitio la kitabu, na Michael F. O'Keeffe
The Trek of Souls
From Ignorance to Divinity
a single-paragraph review of The Aquarian Gospel
by Michael F. O’Keeffe
In this marvelous book, Jesus explains that every living thing is a deity manifest, and each has a soul, which is on a very long trek – from total unawareness of its own divinity, to full consciousness. Every creature, after many incarnations, eventually becomes fully aware of its divine lineage; and later, during subsequent incarnations, each one learns more and more about accessing and utilizing divine strength, wisdom and love; until eventually, every one (plant, animal and human) achieves pure perfection – oneness with God (our Father). He said that He, Jesus, is our example of a man who achieved oneness. He is our elder brother, come to teach us. Jesus is our example of that which we all will eventually become. (He became immortal; He is always with us; He waits for us.)
Masafa ya Sonafi
Kutoka Ujinga hadi Umanani
Aya moja ya pitio la Injili ya Zama za Ndoo
Na Michael F. O'Keeffe
Katika kitabu hichi cha kupendeza ajabu, Yesu aeleza ya kwamba kila kitu hai ni dhahiriko la daiti*, na kila kimoja kina sonafi, ambayo ipo katika masafa marefu sana -- kutokea utokuwamacho na umananifu wake hadi kwenye ukuwamacho. Kila kiumbe, baada ya utwaaji mwili kadha wa kadha, huwaye kufikia kuwa macho na ukoofu wake manani; na baadaye, katika kipindi cha utwaaji mwili kufuatia, kila moja yajifunza zaidi na zaidi kufikia na kuzitumia nguvu zake manani, hekima na upendo; mpaka hatimaye, kila moja (mmea, mnyama na binadamu) ajifanikishia ukamilifu safi - uhali moja na Mungu (Baba yetu). Alisema kwamba yeye, Yesu, ni mfano wa mtu aliyejifanikishia uhali moja. Yeye ni kaka yetu mkubwa, aja kutufundisha. Yesu ni mfano wa kile ambacho sisi wote huwaye kufikia kuwa.
(Yeye alifikia kuwa asiyekoma uhai; Yeye daima yuko nasi; Yeye atusubiri.)
___________
Daiti - Nafsi nguvu ya kimungu juu ya jambo ama sifa, yenye uweza wa kuongozea njia za kheri na mawezekano kwa kadri ya kudra zake
Chanzo:
The Aquarian Age Gospel of Jesus, the Christ of the Piscean Age Author Levi H. Dowling