Kiranga hebu nithibitishie kama gari linatumia mafuta ili kwenda, Kumbuka kuna lubricants dereva fuses battery wiring na vingine vingi, ukiona gari inatembea barabarani ni mkusanyiko wa vingi
Nashangaa :whistle:-- mbona ipo namna ya kumjibu Kiranga ama kuzungumza naye lakini daima huwa mnashindwa?
Hmmm
Kwanza hili ni wazi : mazungumzo na mashauri yote ya namna hii yaweza kuwa ni gumzo tupu...
Kuwa kwake namna hii inamaana yote yanayozungumziwa na kujadiliwa hapa hayatupeleki popote ila kuishia humu humu. Hili kwangu mimi kama mtu, ni jambo lisilo na thamani yoyote na basi sijisikii kulazimika kwa namna iwayo yoyote ile kuwa sehemu ya 'gumzo'...
Ila...
Unakuja wakati ninajisikia kujifurahisha kwa lolote kadri nijisikiavyo na hivi ndivyo ninavyofanya.
Kuna namna mbili za kuonekana kama vile kuelekea kuyafikia 'maarifa'; (i) namna kanushi (ii) namna kubalishivu....
Namna kubalishivu ndiyo ya kwanza na yenye kutawala, hiyo ya kwanza huja kutokana na hii ya pili.
Namna kubalishivu ni nyingi ya ahadi-- labda uweza na mawezekano... Namna kanushi ni isiyokujali yote yajayo na namna kubalishivu.
Mashauri ya Mungu huangukia upande wa namna kubalishivu, ila 'shauri la mungu' linaweza kuonekana kama dhana katika mashauri tu; mashauri si ukweli hasa ila namna fulani 'muakisiko' wa hiyo yenyewe kulingana na vipawa vyetu kuzitafsiri habari za milango yetu ya fahamu.
Katika hali ya kawaida ya mashauri na majadiliano, mimi kama mtu pia ninapenda kuchukua upande wa namna kanushi. Kwa kuwa mashauri tu bila ushahidi wa nguvu na ishara zaidi kwangu ni ubatili. Vile vile yale yote yanayoonekana kwangu kama dalili ya 'ushamba' ama kutojua mambo katika sura ya kheri kamili kwangu pia ni ubatili -- haijalishi yanakuja kwa sura gani, mapokeo ya imani, dini ama kasumba tu ya kiutamaduni, mila na desturi. Katika hali ya kawaida mimi kama mtu, sina mapenzi na dini za mapokeo, desturi 'pofu' za kimakundi...
Lakini...
Kwa kuwa, mtu akiacha mambo batili na kuanza kuchunguza yote kwa faragha yake -- mengi yanawezekana ambayo si wazi kwa makundi ya watu; basi kwa neema, yapo ambayo kwangu mimi kama mtu yanafanyika na kuendelea na yasiyo na ushirika na mengine yaliyotamalaki ila ikibidi kushiriki -- kheri yake itajibayanisha na hayo. Kwa hivyo, ufanyapo bidii kuyang'amua yajayo na utayari wako wa kipekee, usiwe na shauku la kupenda ama kudhani mwingine ndiye atakayethibitisha ubora wako...
Niamuapo kusimamia upande wa namna kubalishivu, mimi kama mtu nina ujumbe na nina kusudi. Ni wakati wa kujaribu kufunua jambo ama mambo, sitajarajii wala kutegemea nitaeleweka mara moja; sitarajiii kama nitaaminika kwa kuwa haya si kusudi lenyewe hasa. Kusudi limo kwenye nia yangu tu kwamba ninataka kujitahidi kuwa wa msaada katika yule ama wale wanaoelekea kutambua ni nini kinafanyika na kuendelea...
Namna kubalivu ni muktadha wa mabadiliko yasiyokoma -- kujinasibu na mabadiliko kwa kheri zaidi. Kama ni ubora basi kwa matunda ya jitahada ni wale waliokusudika tu ndiyo watakaong'amua kinachoendelea... si kila mtu mwenye macho anaona, na si mwenye masikio anasikia... Ipo namna habari njema huwafikia wale tu walio na nasibu ya kuipokea na si vinginevyo.
Ikiwa hujijui wewe ni nani, daima utayumbishwa na yale yanayotegemea makusudio yako dhaifu ama kutokufaa katika mapana ya kheri na jaala yako. Katika kuitafuta njia iliyosahihi, namna yake si sawa na 'hekima' ya duniani. Duniani kuna ujuaji, kuna kushindana, kuna kupigana na kujidhirisha eti wewe ni nani... Katika faragha yako ya nafsi na roho, huna chochote cha kupambana nacho ila wewe mwenyewe...
Sasa, mtu yeyote na asihangaike kumjibu mwingine ili kwamba ajione yeye ni mwenye kujua. Na ikiwa utafanya hivyo bakisha sehemu katika nafsi kujiambia kwamba wafanya la namna hiyo kwa ajili tu ya mazungumzo lakini ikiwa hakuna tija yeyote, ya maana zaidi -- achana na shauri la jambo husika.
Namna kanushi na namna kubalishivu ni mbili katika moja, ipo kweli yake, ipo haki yake...
Sina mpango wa kunata na 'via negativa' ya Buddha kwa sasa, ila ndiyo ni kweli hasa; mwishoni mwa yote ni Buddha.
Ila 'via pozitiva' ipo kwenye muktadha wa dhamma na pia kitu ambacho hapa kitasubiri zaidi -- hekima juu ya kile katika mafundisho ya Buddha huja na mashauri ya 'Sambogha kaya'.
Mdadisi yeyote na achunguze -- ikiwa Buddha alikanusha kuhusu 'Sonafi', je u-Bodhisatva unawezekanaje?
Buddha ni starehe ya mwisho, kama hujayaiva ya 'ma-Avatara', Buddha inakupasa kumsikia kwenye bomba tu, haha.
Hmmmmm