mensaah
JF-Expert Member
- Sep 12, 2016
- 927
- 1,311
Ni sahihi kabisa mkuu, hata kwa sisi wakristo tunaambiwa unapotoa msaada ama sadaka hata mkono wa kushoto hupaswi kujua mkono wa kuume/kulia umetoa kiasi gani.kwa hiyo kwa wanaozingatia maadili kweli wanapotoa misaada hawatangazwi.Mkuu kwenye kutoa kuna mambo mawili, kuna wanaotoa kwa kutafuta sifa mbele ya jamii ili wakubalike. na ambao wanatoa kidini (ibada). Anayetoa kwa nia ya kukubalika mbele ya jamii atafanya kila njia kile anachotoa kionekane. Anayetoa kiibada (uislam na ukristo zote zina ibada ya kutoa) atatoa bila mbwembwe na huenda kwa kificho. Kuna watu leo hata wakitoa sahani ya wali wataalika media. Hata hivyo mi nimeshuhudia shule ambayo baadhi ya vyumba vimejengwa na SS Bakhresa eneo furani jijini dar ambapo pia ana kiwanda cha kuoka mikate kwenye eneo hilo. lakini huyu ndugu pia kuna raia wanamsubiri kila siku kwenye vituo vyake vya biashara na anawapa cash ili wajikimu na maisha