sinajinasasa
JF-Expert Member
- Dec 10, 2013
- 2,988
- 4,144
Nimeona kwenye taarifa ya habari ITV kuwa Reginald Mengi amechangia ujenzi wa kitua cha afya huko Mbeya shilingi milioni 25. Najiuliza huyu mzee ana moyo wa aina gani, au dini yake ndio imemjenga kuwa na huruma ya kuguswa na matatizo ya watu? Ameshachangia sehemu nyingi tu zaidi ya hiyo.
Hapa bongo tunao matajiri ambao tunakula bidhaa zao kila siku kama Bahresa na Mo Dewji na Manji. Hawa kazi yao ni kukusanya pesa tu lakini hakuna mrejesho kwa wananchi, mnatulisha masoda na majuice ambayo hayajengi afya bora zaidi ya kuleta magonjwa! kwanini basi msirudishe faida zenu japo sehemu kidogo kwa kusaidia sehemu zenye mahitaji kama shule, vituo vya afya nk?
Sijawahi kusikia hawa jamaa wamesaidia public au dini zao hawa zinafanana kwamba ukifanya biashara na kulipa kodi inatosha? kuna faida gani ya kuwa na tajiri namba moja kijana Katika Afrika ambaye hata maskini hawajivunii uwepo wako.
Fedha nyingi hazileti afya wala long life, sioni necessity ya ku accumulate wealth kiasi kikubwa bila kuwapa nafuu maskini somewhere kutoka katika faida unazozipata kwenye biashara zako. Mengi angekuwa na biashara ndogo ndogo wallahi ningeamua kumuunga mkono kwa kuuza bidhaa zake.
Bidhaa za Mo na Azam zimejaa kila kona nchini, lakini mrejesho hakuna zaidi ya ule wa kiuchumi kwamba ametengeneza ajira. Hawa matajiri wengine wanaona kitu cha maana kuchangia kwenye michezo kuliko kugusa roho za watu. Kwa kweli Mzee Mengi anapaswa kuungwa mkono kwa kila jambo.