Nani wa kumuishi Reginald Mengi?

Filosofia ya Rorya

JF-Expert Member
Sep 20, 2021
3,214
3,587
Reginald Abraham Mengi aliishi kwa ajili ya wenzake ambao ni wahitaji kwenye jamii.

Tumeshuhudia akila na kunywa nao pamoja, akiwaruzuku na kuwafadhili mavazi na mitaji ya ujasiriamali.

Makundi yafuatayo kwenye jamii yalishiriki kufanyika hadhira ya ndoto yake hiyo:-

1. Wazee hususan wa Dar.
2. Wanaoishi na ulemavu.
3. Vijana.

Namba 1 alikunywa na kula nao na kuwakabidhi bahasha.

Namba 2 alikula, kunywa nao na kuwapa mitaji na miundombinu ya kuwarejeshea thamani ya ubinadamu wao.

Namba 3 aliwapa mitaji na kutuza (kwa fedha) vipaji vyao na kuamsha ubunifu wao. Alienda mbali zaidi akaendesha mashindano ya kubuni mawazo bora ya ujasiriamali na kutuza washindi.

Faida ya ujasiriamali wa RAM sehemu yake aliirejesha kwenye jamii kupitia utaratibu wa CSR.

Maswali magumi:-

1. Nani leo anaishi legacy hii ya RAM?

2. Kuna mtu anakusudia kuiishi hii legacy ya RAM kwa miaka ijayo?

3. Taasisi za RAM hakuna hata moja inayoweza kuendeleza legacy hii ili kuambukiza jamii pana kutekeleza legacy na kurithisha vizazi vijavyo?

4. RAM tunamuishi vipi leo, kesho, mtondo na mtondogoo?

5. Hakuna wajasiriamali wakubwa kama alivyokuwa RAM ambao wanaweza kunia, kudhamiria na kuthubutu kuwatengeneza RAM wengi wapya?

6. Je, salaam za rambirambi nyingi zile na hotuba za taasisi mbalimbali ikiwemo hotuba ya serikali wakati wa kuupumzisha mwili wa RAM leo zimefeli kutekelezeka waliyoyaahidi?

7. Mataifa tajiri yana mfumo ambao tajiri ndiyo anakufa lakini utajiri wake haufi bali unaendelezwa kwa manufaa ya jamii na serikali. Makampuni makubwa ya biashara yaliyotumika kukolonisha Afrika bado yanaishi hata leo licha ya safu za wamiliki wake na warithi wake kufa.

Toa maoni yako nini kifanyike kuhuisha legacy ya RAM na kumuishi kivitendo.
 
Back
Top Bottom