Elections 2010 REDET walituambia, tukawakejeli

unaumwa wewe na majibu ya ndio hapana kwenye polls ili wasimuudhi mkuu! tafuta cha kufanya

I remember my dad used to tell me "Don't argues with fools coz' people will not notice the difference!"
 
Hakuna lolote hao REDET ni vibaraka wa system na huyo mmoja VC ni mwanamtandao na mwingine ni mshauri wa Mkulu katika masuala ya kisiasa. You got that?

Hayajui haya,basi tu kutaka ajimwage naye asomeke humu!
 
Nakumbuka walisema watafanya utafiti tena September ngoja tusubiri.

Hivi utafiti wao ukija kuwa wa ukweli kuwa Dr.Slaa anapendwa na watu alafu anafuatia Zitto na wa tatu JK vibarua vyao vitaendelea?
 
Tatizo la utafiti limekuwa kumshindanisha JK na watu ambao walikuwa hawajatangaza kugombea. Wafanye opinion poll sasa hivi kati ya: JK, Slaa na Lipumba then walete matokeo. Wanaweza wakafanya sasa hivi, ingine katikati ya kampeni na ingine mwishoni.
 
Mkuu Kitila, huo utafiti wana kila sababu ya kusita kuufanya wakati huu. Wanajua ukweli uko wapi na wataogopa kuutoa kwani wanajua madhara yake kwa mshikaji wao. Hivi sasa itakuwa kazi kweli kweli kujaribu kuzipindisha hizo takwimu kwa sababu ukweli uko wazi hata kwa kipofu.
 
Hawa REDET wanaiga utamaduni wa nchi za magharibi hasa marekani ambapo opinion polls zinatumika kutekeleza matakwa ya chama watafiti wanachokipenda!! Sasa huku kwetu REDET ni chombo ambacho kila siku utafiti wake na matokeo yake yataonesha upendeleo kwa ccm na ndio maana viongozi wa REDET mara baada ya chaguzi hutunikiwa vyeo na watawala kama bahashishi kwa kuwatimizia malengo yao!! Mmoja wao alipewa uVC wa chuo kikuu na mwingine ni commissioner wa Tume ya Uchaguzi baada ya uchaguzi wa 2005!! Utafiti wao sio objective kwasababu samples wanazotumia kufikia mahitimisho yao zinakuwa biased.
 
REDET hawakusema lolote kwani kushindwa kwa wabunge wa CCM siyo jambo lililokuwa linahitaji utafiti. Tayari ilishajulikana wazi kabisa baada ya kumfungia Zito kuhudhuria bunge kwa kutetea migodi ya madini wabunge wengi wa CCM waliohusika wangekuwa matatizoni. Hata bibi yangu alisema hatawachagua CCM tena kama kazi yao ni kuwateteta wazungu wachukue dhahabu zetu bure. In fact hata Kikwete ni mmoja wao ila tulifundishwa kutomkandya baba yetu hadharani; itabidi tusubiri hadi siku ya fainali.

Sielewa hao maprofesa wetu wa REDET wanatumiaje ubongo wao iwapo utafiti wanaofanya ni ule ambao hata bibi yangu ambaye hakwenda shule anaujua.
 
wana(jf a.k.a chadema) utafiti ukifanyika JF obvious SLAA atashinda.....na utafiti ukifanyika ndani ya chadema ni obvious pia SLAA atakuwa wa kwanza then ZITTO kisha JK awe wa mwisho....Lakini toa utafiti wako uwe na uwanja mpana zaidi........THE SMILING PRESIDENT WILL SHINE....... Tupende kujiambia ukweli ndipo tutakuwa salama...........hapa waweza sema wa kwanza atakuwa JK......SLAA.....LIPUMBA....then wengineo!
 
I remember my dad used to tell me "Don't argues with fools coz' people will not notice the difference!"

Another saying is that if you argue with an ignorant/ a fool, s/he will pull you down to his level and beat you by his/ her experience. The point is that don't stop arguing but make sure in the course of arguing a fool or an ignorant does not pull you down to his level. JF is for great thinkers but I doubt if there is any membership requirements, say, level of education, number of research papers published in renowned peer reviewed journals, etc.
 
Wakuu ningependa kuuliza, kwenye serikali ijayo, kama Kikwete atashinda, Profesa Rwekaza sympho Mukandala, atakuwa mbunge wa kuteuliwa na hatimaye Waziri, katibu mKuu wa wizara au balozi. Nilisikia "funufunu" kama hizo.

Redet wako pale kwa interest za watu, no wonder wanayosema yanakuwa na mwelekeo fulani. Si yote wanayosema ni uongo na si yote wanayosema ni kweli.

Waposema kukubalika kwa Kikwete wanakuwa na maana fulani kuhusu namna wananchi wanavyomchukulia. Lakini hii haina maana JK anafaa kwa asilimia ngapi kuwa rais. Tunatakiwa tujue vigezo wanavyotumia, nadhani Dk Kilian kunasiku moja alieleza vizuri pale kwenye jengo la Redet kuhsu vigezo wnaavyotumia.
 
Hawa REDET wanaiga utamaduni wa nchi za magharibi hasa marekani ambapo opinion polls zinatumika kutekeleza matakwa ya chama watafiti wanachokipenda!! Sasa huku kwetu REDET ni chombo ambacho kila siku utafiti wake na matokeo yake yataonesha upendeleo kwa ccm na ndio maana viongozi wa REDET mara baada ya chaguzi hutunikiwa vyeo na watawala kama bahashishi kwa kuwatimizia malengo yao!! Mmoja wao alipewa uVC wa chuo kikuu na mwingine ni commissioner wa Tume ya Uchaguzi baada ya uchaguzi wa 2005!! Utafiti wao sio objective kwasababu samples wanazotumia kufikia mahitimisho yao zinakuwa biased.

Tuache ushabiki usio na maana wala tija!Hata mimi Dr. Slaa namkubali, and i think kuliko Kikwete! Lakini ingawaje namkubali Slaa kuliko Kikwete, bado naikubali CCM (as A well established institution)Kuliko CHADEMA! Aidha, kumkubali Slaa wala hakunipi shaka kwamba Kikwete na CCM yake watashinda. Kukataa ukweli huu ni sawa na kukataa ukweli kwamba kati ya jua na dunia, kinachozunguka ni dunia na sio jua! Katika akili ya kawaida inaonekana kinachozunguka ni jua na sio dunia! Slaa anakubalika; lakini tangu lini watanzania wameacha kuchagua chama badala ya mtu?! Kwa CHADEMA gani? Hii hii tunayoijua wote!! Tusidanganyike na mbwembwe za kupaa na helikopta kupita kuomba udhamini! Hivi kweli Slaa hapa alipo ameshafikia pale ambapo Lytatonga Mrema alifikia 1995?! Jambo pekee ninaloamini mimi ni kwamba Slaa(sio CHADEMA) atazipunguza kura za Kikwete kwa kiasi cha kutosha tu lakini sio kushinda! Na atashinda wala sio kwa kuiba kura bali kwa kura halali kabisa za mamilioni ya Watanzania ambao huwaambii lolote kuhusu Kikwete na CCM yao. Wala msidanganyike na kura za maoni zinazopigwa humu JF ambazo mimi peke yangu naweza kusema NDIYO au HAPANA hata mara elfu moja! Inawezekana kabisa kwamba REDET wanatumiwa, lakini ule utafiti wa Synovate ulikuwa tofauti sana na REDET?! nao wanatumiwa?! Tusisahau, kukubalika moja, kuchaguliwa kitu kingine! Mwenye macho haambiwi tazama, am afraid watu wameingiwa na mavumbi ya helikopta ya CHADEMA!
 
Tazama utafiti unaofanywa na jamiiforum, majibu ndo haya. sample ni muhimu sana kwenye kupata matokea sahihi ya utafiti. ndo maana nikapinga kuwa watanzania wakawaida hawawezi kusema kuwa daily news ndio gazeti makini, ingawa ndio ukweli wenyewe. sasa redet wanapata wapi majibu yao, wanajijibu wenyewe hao

Bado una imani na serikali ya Kikwete? (3640 Votes)

  1. NDIYO (YES) 21%
    (764 Votes)

  2. HAPANA (NO) 75%
    (2738 Votes)

  3. Sijui (Undecided!) 4%
    (138 Votes)
 
Tuache ushabiki usio na maana wala tija!Hata mimi Dr. Slaa namkubali, and i think kuliko Kikwete! Lakini ingawaje namkubali Slaa kuliko Kikwete, bado naikubali CCM (as A well established institution)Kuliko CHADEMA! Aidha, kumkubali Slaa wala hakunipi shaka kwamba Kikwete na CCM yake watashinda. Kukataa ukweli huu ni sawa na kukataa ukweli kwamba kati ya jua na dunia, kinachozunguka ni dunia na sio jua! Katika akili ya kawaida inaonekana kinachozunguka ni jua na sio dunia! Slaa anakubalika; lakini tangu lini watanzania wameacha kuchagua chama badala ya mtu?! Kwa CHADEMA gani? Hii hii tunayoijua wote!! Tusidanganyike na mbwembwe za kupaa na helikopta kupita kuomba udhamini! Hivi kweli Slaa hapa alipo ameshafikia pale ambapo Lytatonga Mrema alifikia 1995?! Jambo pekee ninaloamini mimi ni kwamba Slaa(sio CHADEMA) atazipunguza kura za Kikwete kwa kiasi cha kutosha tu lakini sio kushinda! Na atashinda wala sio kwa kuiba kura bali kwa kura halali kabisa za mamilioni ya Watanzania ambao huwaambii lolote kuhusu Kikwete na CCM yao. Wala msidanganyike na kura za maoni zinazopigwa humu JF ambazo mimi peke yangu naweza kusema NDIYO au HAPANA hata mara elfu moja! Inawezekana kabisa kwamba REDET wanatumiwa, lakini ule utafiti wa Synovate ulikuwa tofauti sana na REDET?! nao wanatumiwa?! Tusisahau, kukubalika moja, kuchaguliwa kitu kingine! Mwenye macho haambiwi tazama, am afraid watu wameingiwa na mavumbi ya helikopta ya CHADEMA!

Ninapozungumzia objectivity katika utafiti, ni tafiti zote ziwe za REDET, JF au SYNOVATE. Ili kupata majibu yaliyo sahihi utafiti unatakiwa uwe na sample kubwa ambayo pia ni representative, mfano mzuri ni huu utafiti wa JF unauliza kama wanajanvi wanaipenda serikali ya Jakaya au La. Sample ya watu wanaoulizwa ni biased kwasababu wengi wa wanajanvi naweza kusema hawaipendi ccm na ni wachache sana ukilinganisha na population ya million 40 ya waTanzania, kwahiyo basi ni dhahili kuwa matokeo yake yataiponda CCM na hayatakuwa representative ya maoni ya majority ya WaTanzania!! Hivyo hivyo kwa taasisi za REDET na SYNOVATE!! Synovate kwa mfano tafiti zake hazitiliwi maanani sana kule Kenya kwa sababau hizi hizi za kuwa biased for the establishment.
 
REDET hawana affiliation yoyote na chama chochote., ni mindset za watu ambao siku zote ni wabishi. Sisi wana JF ni wasomi, tunajua maana ya utafiti. Labda mtu angekosoa malengo ya utafiti uliofanywa na REDET, siyo kukosoa matokeo ya utafiti huo. Halafu magazeti husomwa na literate population, wanakijiji wa swaswa ni wangapi wanaojua hata mmagazeti matatu maarufu tz?? Tuache upumbavu bana!!!!:

nod::yawn:
 
Pokola tafadhali usiwe na jazba!! Tafiti nyingi pamoja na hizi za REDET hukusanya data ambazo huzitumia kutafsiri matokeo ya tafiti hizo; ni hizi hizi data ambazo hupikwa na hawa watafiti ili matokeo ya tafiti yalingane na matakwa/malengo ya watafiti!! Haya malengo ya watafiti sio independent of the wishes of the people who finance these researches who in the case of REDET ni pomoja na taasisi za kutoka nje!! Kama huamini muulize Mukandala source yao ya funds.
 
REDET hawana affiliation yoyote na chama chochote., ni mindset za watu ambao siku zote ni wabishi. Sisi wana JF ni wasomi, tunajua maana ya utafiti. Labda mtu angekosoa malengo ya utafiti uliofanywa na REDET, siyo kukosoa matokeo ya utafiti huo. Halafu magazeti husomwa na literate population, wanakijiji wa swaswa ni wangapi wanaojua hata mmagazeti matatu maarufu tz?? Tuache upumbavu bana!!!!:

nod::yawn:

Duh upumbavu tena mzee, haya bana!!!!
 
Spiderman, huyu junior aende lupango kidogo, amevunja amri ya kwanza!
 
REDET walishazungumza mapema! Watu wakawakejeli kwamba eti wanatumiwa!! Gazeti la Tanzania Daima likadai eti REDET inatumiwa na Kikwete; kwamba REDET wanapotoa utafiti kuonesha kukubalika kwa Kikwete kunajenga saikolojia ya wapiga kura wamchague Kikwete!! Aibu zaidi, Tanzania Daima waliibuka na tahariri iliyoikandia REDET; kwavile tu ripoti hiyo ya REDET ilionesha Kikwete angeshinda kwa asilimia nyingi endapo uchaguzi mkuu ungefanyika wakati wa utafiti uliokuwa umefanyika na REDET!

Bila shaka Tanzania Daima wangekubaliana na utafiti wa REDET endapo ungesema CHADEMA kingeshinda!! Wakati Tanzania Daima walipotoka na tahariri ya kukejeli utafiti wa REDET, walisahau kwamba siku chache tu kabla ya hapo wao walikuwa wameibuka na kura za maoni zilikuwa zimeendeshwa humu JF!

Hata wana CCM nao wakaupinga utafiti wa REDET, kisa tu kilitabiri mabaya kwa wabunge kadhaa kwamba wangepigwa chini!! KIKO WAPI? Nyota njema imeonekana asubuhi! Asubuhi asubuhi, tayari wabunge kadhaa wa CCM wamegalagazwa hata kabla ya uchaguzi mkuu wenyewe bado! Nasikia karibi wabunge 50 chali na game bado linaendelea! Hao ni wale waliopteza mikononi mwa wana-CCM wenzao! Je, ni wangapi kwa waliosalia watakaopoteza viti vyao kwa upinzani?!

Mimi si Mwana CCM, CHADEMA wala REDET; ila ningependa kuwashauri Watanzania kujenga utaratibu wa kuamini tafiti zetu! Sina hakika, lakini naamini REDET imeundwa na wasomi hivyo kubeza tafiti zao ni kubeza umuhimu wa wasomi wetu.

Inawezekana REDET wakati wanafanya utafiti wao walimtumia Lipumba na Mrema kama wagombea kutoka kambi ya upinzani. Sasa hivi ukilinganisha Mrema na Tambwe kwenye kura za maoni hata ya Udiwani, Tambwe atamzidi Mrema. Huo ni mfano mfupi tu, REDET wanatakiwa kufanya huo utafiti sasa hivi baada ya Dk. Slaa kutangaza kugombea.
 
Inawezekana REDET wakati wanafanya utafiti wao walimtumia Lipumba na Mrema kama wagombea kutoka kambi ya upinzani. Sasa hivi ukilinganisha Mrema na Tambwe kwenye kura za maoni hata ya Udiwani, Tambwe atamzidi Mrema. Huo ni mfano mfupi tu, REDET wanatakiwa kufanya huo utafiti sasa hivi baada ya Dk. Slaa kutangaza kugombea.[/FONT ]

Mwelekeo wa matokeo ta tafiti za REDET hata wakifanya sasa baada ya DR. Slaa kuingia ulingoni hayatakuwa tofauti na matokeo yao ya awali kwasababu nilizoziainisha hapo awali. Tafiti zao zina malengo mahususi!!
 
Back
Top Bottom