REDET walituambia, tukawakejeli | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

REDET walituambia, tukawakejeli

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by NasDaz, Aug 3, 2010.

 1. N

  NasDaz JF-Expert Member

  #1
  Aug 3, 2010
  Joined: May 6, 2009
  Messages: 11,308
  Likes Received: 1,655
  Trophy Points: 280
  [FONT=&quot]REDET walishazungumza mapema! Watu wakawakejeli kwamba eti wanatumiwa!! Gazeti la Tanzania Daima likadai eti REDET inatumiwa na Kikwete; kwamba REDET wanapotoa utafiti kuonesha kukubalika kwa Kikwete kunajenga saikolojia ya wapiga kura wamchague Kikwete!! Aibu zaidi, Tanzania Daima waliibuka na tahariri iliyoikandia REDET; kwavile tu ripoti hiyo ya REDET ilionesha Kikwete angeshinda kwa asilimia nyingi endapo uchaguzi mkuu ungefanyika wakati wa utafiti uliokuwa umefanyika na REDET!

  Bila shaka Tanzania Daima wangekubaliana na utafiti wa REDET endapo ungesema CHADEMA kingeshinda!! Wakati Tanzania Daima walipotoka na tahariri ya kukejeli utafiti wa REDET, walisahau kwamba siku chache tu kabla ya hapo wao walikuwa wameibuka na kura za maoni zilikuwa zimeendeshwa humu JF!

  Hata wana CCM nao wakaupinga utafiti wa REDET, kisa tu kilitabiri mabaya kwa wabunge kadhaa kwamba wangepigwa chini!! KIKO WAPI? Nyota njema imeonekana asubuhi! Asubuhi asubuhi, tayari wabunge kadhaa wa CCM wamegalagazwa hata kabla ya uchaguzi mkuu wenyewe bado! Nasikia karibi wabunge 50 chali na game bado linaendelea! Hao ni wale waliopteza mikononi mwa wana-CCM wenzao! Je, ni wangapi kwa waliosalia watakaopoteza viti vyao kwa upinzani?!
  [/FONT]

  [FONT=&quot]Mimi si Mwana CCM, CHADEMA wala REDET; ila ningependa kuwashauri Watanzania kujenga utaratibu wa kuamini tafiti zetu! Sina hakika, lakini naamini REDET imeundwa na wasomi hivyo kubeza tafiti zao ni kubeza umuhimu wa wasomi wetu. [/FONT]
   
 2. Technician

  Technician JF-Expert Member

  #2
  Aug 3, 2010
  Joined: Mar 30, 2010
  Messages: 843
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  You are right some time but not so much time men.
   
 3. Freetown

  Freetown JF-Expert Member

  #3
  Aug 3, 2010
  Joined: Apr 6, 2008
  Messages: 887
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  sasa kuna wagombea wa upinzani ambao wakati wa utafiti hawakuwa wametangaza nia ya kugombea, na hivyo utafiti uliofanyika ulikuwa unamlenga mtu mmoja ambaye hakuwa na mpinzani. sasa fanyeni utafiti sasa ambao utatoa picha halisi.
   
 4. M

  Magezi JF-Expert Member

  #4
  Aug 3, 2010
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  Hoja yako iko biased
   
 5. G

  Gagnija JF-Expert Member

  #5
  Aug 4, 2010
  Joined: Apr 28, 2006
  Messages: 6,316
  Likes Received: 618
  Trophy Points: 280
  Kauli ya Kikwete juzi baada ya kuchukua fomu ina "negate" matokeo ya utafiti huo. Labda wafanye utafiti mwingine kipindi hiki baada ya Dr Slaa kutangaza nia.
   
 6. Kilbark

  Kilbark JF-Expert Member

  #6
  Aug 4, 2010
  Joined: Feb 25, 2008
  Messages: 558
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Hakuna lolote hao REDET ni vibaraka wa system na huyo mmoja VC ni mwanamtandao na mwingine ni mshauri wa Mkulu katika masuala ya kisiasa. You got that?
   
 7. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #7
  Aug 4, 2010
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,470
  Likes Received: 5,852
  Trophy Points: 280
  Tulichopinga ni kuhusu kukubalika kwa JK....hilo la wabunge wengi wa CCM kuanguka ni utafiti wetu hapa JF wao REDET wakakopi kama wanvyokopi wengi wengineo toka humu...kumbuka hao REDET ni member humu
   
 8. Joseph

  Joseph JF-Expert Member

  #8
  Aug 4, 2010
  Joined: Aug 3, 2007
  Messages: 3,527
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  Tunataka REDET wafanye tena utafiti wao sasa maana kwa wakati huo hali haikuwa kama ilivyo sasa
   
 9. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #9
  Aug 4, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Kwa jinsi tulivyoona rushwa kushamiri katika kura za maoni ndani ya teuzi za wagombea wa CCM, hawa REDET wanaweza tu kuaminika endapo watakuwa wanaongeza kipengele katika matokeo ya tafiti zao: "Wagombea wa CCM watatumia rushwa kupata ushindi wa kishindo."

  Nashangaa kwa nini REDTE huwa hawaweki element za kuwapo kwa rushwa katika tafiti zaoi kuhusu CCM, kitu ambacho kinajionyesha dhahiri -- hata mtoto wa miaka kumi anakliona!
   
 10. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #10
  Aug 4, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0

  Umenena ndugu yangu. Pamoja na kwamba wameshaona wenyewe kwa macho yao, Redet wanao ubavu, katika tafiti zao, kuuliza swali kama hili: 'Jee, CCM na (wagombea wao) inaweza kushinda kwa kishindo bila rushwa?'
   
 11. Mwanamayu

  Mwanamayu JF-Expert Member

  #11
  Aug 4, 2010
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 7,944
  Likes Received: 2,091
  Trophy Points: 280
  Hivi matokeo yalihusu kura za maoni za CCM au uchaguzi mkuu kwa ujumla? Kwa nini NEC ya CCM inabadilisha matokeo ya kura za maoni kwa baadhi ya wanachama wake?

  Nafikiri ni vema kupima "quality" ya tafiti za REDET baada ya uchaguzi mkuu Oktoba. Je, unajua vigezo vya utafiti wenye "quality"? Je, na wa Synovate unatuambiaje?
   
 12. Luteni

  Luteni JF-Expert Member

  #12
  Aug 4, 2010
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 2,274
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Nakumbuka walisema watafanya utafiti tena September ngoja tusubiri.
   
 13. Tuko

  Tuko JF Bronze Member

  #13
  Aug 4, 2010
  Joined: Jul 29, 2010
  Messages: 11,186
  Likes Received: 397
  Trophy Points: 180
  REDET inawezekana imeundwa na wasomi ndio, lakini haifanyi utafiti wa kisomi. Huwezi kumuuliza mtu kuwa eti unadhani Kikwete atashinda uchaguzi, alaf unampa majibu ya
  a) Hapana
  b) Inawezekana
  c) Naamini
  d) Ndiyo

  Majibu unayopata unaconclude kuwa uchaguzi ungefanyika leo asilimia 75% watamchagua!!! watamchagua dhidi ya nani?
   
 14. Geza Ulole

  Geza Ulole JF-Expert Member

  #14
  Aug 4, 2010
  Joined: Oct 31, 2009
  Messages: 11,078
  Likes Received: 4,016
  Trophy Points: 280
  unaumwa wewe na majibu ya ndio hapana kwenye polls ili wasimuudhi mkuu! tafuta cha kufanya
   
 15. Masikini_Jeuri

  Masikini_Jeuri JF-Expert Member

  #15
  Aug 4, 2010
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 6,809
  Likes Received: 364
  Trophy Points: 180
  Kinachotokea sasa kimedhihirishwa na ule utafiti hata kama bado hatujafika kwenye uchaguzi mkuu lakini mchakato wa kuelekea huko unatupatia sura yake jinsi itakavyokuwa naunga mkono hii hoja; ni kweli hatuamini tafiti; mimi pia kama mtoa hoja SINA CHAMA nachokiunga mkono!
   
 16. GY

  GY JF-Expert Member

  #16
  Aug 4, 2010
  Joined: Nov 2, 2009
  Messages: 1,280
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 133
  Tazama matokeo ya huo utafiti unaoitwa wa wasomi

  "Gazeti la DAILY NEWS lilionekana kuwa ndio gazeti linaloaminiwa zaidi"

  Je mimi mtu wa kawaida nikihoji matokeo ya utafiti huu ntakua nimekosea?
   
 17. M

  Mwanjelwa JF-Expert Member

  #17
  Aug 4, 2010
  Joined: Jul 29, 2007
  Messages: 961
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35

  Wewe mwananchi wa kawaida huwezi lisoma hili gazeti. Hili Gazeti mpaka vbiunga vya Nairobi linauzwa na linaisha labla hata ya Dar hayajaisha. Sina uhakika na utafit wao lakini Gazeti liko juu sana kwa watu wanaofuatlia mambo tofauti.
   
 18. GY

  GY JF-Expert Member

  #18
  Aug 4, 2010
  Joined: Nov 2, 2009
  Messages: 1,280
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 133
  Haya, kweli kabisa gazeti liko makini, na mpaka Nairobi linauzwa, good

  Je utafiti huu ulihusisha watu wa aina gani, wananchi wakawaida ambao hata hawajui kuwa kuna gazeti kama hilo? ulihusisha wakenya? ulihusisha wasomi toka CHUO KIKUU (In Tanzania chuo kikuu means university of Dar es Salaam), au ulihusisha watafiti wenyewe tu, wakawa wanajibu maswali yao....kwangu mimi hiki ni kiashiria cha utafiti uchwara,,,ukienda kijiji cha swaswa huko Dodoma leo hii, ukihoji wananchi ambao ni typical wanakijiji wa swaswa je ni gazeti gani makini Tanzania, je watajibu daily news?
   
 19. N

  NasDaz JF-Expert Member

  #19
  Aug 4, 2010
  Joined: May 6, 2009
  Messages: 11,308
  Likes Received: 1,655
  Trophy Points: 280
  Hivyo ndivyo wanadamu tulivyo mkuu
   
 20. N

  NasDaz JF-Expert Member

  #20
  Aug 4, 2010
  Joined: May 6, 2009
  Messages: 11,308
  Likes Received: 1,655
  Trophy Points: 280
  You are right, nahisi hata wao walisema endapo uchaguzi ungefanyika wakat wanafanya utafiti wao!
   
Loading...