Dont get me wrong bro, sio kwamba ninamuunga mkono zitto hapa, hapana....
Issues hapa ni kubwa zaidi ya Zitto, Zitto kajichanganya kafanywa mfano tu.Tukiongea tuongee concepts kwa kina, ufinyu wa mawazo wa wanasiasa wa Tanzania. Wanafikiri wakituambia Nyerere alikuwa unpredictable hilo lina justify unpredictability.
Hawajui kwamba hata huyo Nyerere mwenyewe hakutaka kuji identify na unpredictability, rais akiwa unpredictable katika nchi inayofuata rule of law na fair trade biashara haiendi, investments haziji, stock markets hazipandi.
Zitto kama angekuwa amesoma uchumi angejua kwamba unpredictability is not a desirable factor. Ubovu wanasiasa wetu uchwara wanaendekeza ego, yaani mtu anajiona demigod aliye above rule of law na rational predictability.
Huyu atatufaa kutuongoza kweli? Mchumi asiyejua kwamba unpredictability si sifa nzuri, ni sifa mbaya. Anaujua uchumi kweli huyu? Anaijua siasa kweli huyu ? Tumesema kwamba Kikwete ni mchumi jina asiyejua uchumi, na Zitto naye ?
ila kukosea kuandika kwangu naweza kukusamehe lakini what he has been doing lately brings more questions than answears.
Hapa kakosea zaidi ya kuandika, hata ukiondoa hayo ya nje. Hapa kajionyesha yeye si mtu anayependa sheria. Mtu anayependa kuwa unpredictable hapendi kuwekewa mipaka, anapenda udikteta. Hapa kakosea kuchagua lugha asiyoiweza kujieleza, inaonekana sio tu kwamba hajui kiingereza vizuri, bali pia hajui hata kama hajui, angejua hajui naona angetumia Kiswahili asiadhirike bila sababu ya msingi.
Hapa kakosea kwa kukosa staha, kusema "mimi ni unpredictable" mbunge ni sawa na kuwaambia wananchi waliokupigia kura kwamba hamnijui, mmenipigia kura kwa ghiliba zangu tu, lakini naweza kuwabadilikia muda wowote, mimi si unpredictable bwana? Ndiyo maana mwanasiasa aliyekomaa wakati wote anatakiwa ku cultivate image ya predictability, na kamwe si unpredictability.
Mfano Kuweka post hii hapa ni kwa faida gani, is he questioning Nyerere motives or is he justifying himself being unpredictable cause nyerere was unpredictable pili kuongea na TBC1 kuhusu Chadema.
Anajaribu kuonyesha kwamba kwa sababu Nyerere alikuwa unpredictable, huwezi kutia shaka kwamba unpredictability si kitu kizuri. Kwanza hajui kuna watu wanamuona Nyerere si mali kitu na kwa hiyo kuwapa mfano wa Nyerere kuwa impress ni ushamba. Pili, hata huyo Nyerere mwenyewe hakuwahi kusema yeye ni unpredictable, alikuwa kila siku anasema principles zake.
Mtu akikwambia yeye ni unpredictable, kwa maana nyingine anakwambia hana guiding principles zinazojulikana. kama anazo guiding principles zinazojulikana tayari kashakuwa predictable.
Ukiona mwanasiasa anajigamba kwamba yeye ni unpredictable ujue huyo hafai, anaweza kukuambia moja halafu akakugeuzia kibao akasema kageuka, si unpredictable bwana, na kashakwambia hivyo, utamlaumu kwa lipi wakati mtu kashakwambia yeye unpredictable ?
Hii inaniacha huku nikijiulize does this boy think about the outcomes of his actions.
Wamelewa madaraka hawa watu, wakienda kuwashikia akili watu vijijini huko wanajiona vimungu mtu tayari, they can do no wrong, they can say no wrong.
Where is the famed Tanzanian humility in saying "I am unpredictable". It is a gross creed of arrogance.
Have some humility Zitto.