@Kiranga heshima mbele mkuu, nadhani tunatoka kwenye hoja aliyowasilisha Mheshimiwa Zitto Kabwe na kutokomea kwenye kujadili lugha ya kiuandishi. Si vizuri kubezana k.h.s vyuo na kushabikia lugha ya mkoloni (kizungu). Turudi kwenye kuijibu hoja iliyo mbele yetu, kwa nini Mwalimu aliunga mkono Biafra?
Shukrani.
"Miafrika Ndivyo Tulivyo- Nyani Ngabu"
Na pale nilipoongea falsafa za Machiavelli katika "The Prince" nilikuwa nimetoka ndani ya hoja?
Nilipoongelea historia ya Lyndon Johnson katika US Senate with relations to "predictability" nimetoka katika hoja?
Nilivyoongelea irony ya humility ya Nyerere kupigiwa mfano wa arrogance ya Zitto nimetoka katika hoja?
Nilivyoongelea kwamba "the truly unpredictable cultivate an aura of predictability, and those who tout themselves as unpredictable must be predictable rookies" nimetoka katika hoja ?
Au macho yako hayaoni vizuri? Au ni lawama za ubongo kuweza ku process mambo? Maana nimeongelea hoja all over the place, nikasema hata Kiingereza ni hoja, kwa maana at the very least inatuonyesha Zitto hajui kuchagua lugha ambayo anaiweza zaidi, kwa hiyo ana poor decision making process, hii ni hoja tofauti kabisa na uwezo wa lugha.
Nimeongelea fraudulent representation hapa, Zitto anakaa bungeni na kutuambia anapata habari zake kutoka kwenye Wall Street Journal, sasa huyu mtu ambaye kiingereza cha darasa la nne kinampa matatizo Wall St Journal atasoma vipi ? Anaproject image ya usomi wa Wall St Journal wakati grammar ya primary school inamshinda ? Hapa hata ukisema kutojua kiingereza si kosa, mimi naona kuna utapeli.
Mbona wabunge wengi hawajui Kiingereza hata cha kuombea maji, wameuchuna, hawajaja hapa kujitutumua, na wala siwezi kuwasema kwa sababu tu hawawezi kiingereza.
Halafu ukifikiri kwamba main point ya hii thread ni Biafra utakuwa umekosea comprehension. I will give you a pass kwa sababu ukiangalia kijuu juu tu, ukaangalia kichwa cha thread, utafikiri point ni "Kwa nini Nyerere ali support Biafra"
Actually ukiangalia post ya Zitto iliyoanzisha hii thread, na post aliyo i quote, utaona point ya thread ni kwamba Zitto anatetea unpredictability yake, ambayo anaifananisha na Nyerere kuwa unpredictable kwamba ingawa alikuwa Pan African muda mwingine alikuwa unpredictable.
Zitto alivyoanza thread tu inakuonyesha kwamba huyu mtu si makini.