Re: Why Did Nyerere Support Biafra? - Semantics !

Kiranga,

Pana wakati unanitibua na pana wakati inabidi nikubaliane na wewe.

Ngoja kwanza: Kuna huyu kaandika kuhusu Makabila ya Zimbabwe, Haile Selasi, Msumbiji na Upupu mwingine. Huyu na yeye ni mweupe na heri angeliandika kwa Kiingereza ili ajitetee baadaye kuwa hafahamu lugha kama Mzee wa vijisenti. Nashukuru Member mmoja kamjibu vizuri tu mropokaji huyo ambaye sitaki hata kumkumbuka jina.

Kiranga tena: Unajua kuna watu tumesoma na kuishi duniani sehemu tofauti na huko kujifunza lugha tofauti. Sasa inafika siku, unafahamu lugha nne au tano kwa juujuu tu ila ukweli unakuwa hufahamu lugha yoyote.

Kuhusu Kiingereza cha darasa la nne: Hili nakubaliana na wewe waziwazi. Pana siku nikiwa kwenye Bus nchi ya wageni, alikuwepo mtoto mmoja ndani ya Bus kama kichaa kichaa hivi ila kijana alikuwa na akili za ajabu sana. Alikuwa na umri kama wa miaka 7 hivi. Kama mtoto kuna mengine alikuwa akichemsha, mengine kama vile kutukana na mengine mambo ya Kisomi haswaa. Katika kuongea kwake, nilisikia akisema "The law of the jungle: Survive of the fittest." Mama mmoja niliyekuwa nimekaa naye, anaweza kuwa Mwalimu, alitoa karatasi mfukoni na kumuomba yule mtoto arudie. Mtoto alirudia na mama akaandika.
Wenzetu vitu kama hivi kweli wanasomewa na wazazi wao tangu hawajaanza kusoma. Wanafunzwa historia za watu wao mashuhuri. Ni kawaida mtoto kukuambia maneno kama "viungo vya binadamu visivyotumika, hupotea...." Sijui kama nimeitafasiri vema kwa Kiswahili (Use and disuse – Individuals lose characteristics they do not require (or use) and develop characteristics that are useful - Lamarck's Theory). Ila ukweli unabaki kuwa System yetu ya kusomesha Primary school ambao ndiyo msingi, kwa miaka mingi ilikuwa mbaya sana na sasa ni kama imekufa kabisa. Watoto wanasoma ili kufaulu na wengi wanafaulu kwa mitihani kuibiwa na mwisho unabaki na kizazi cha Wachakachuaji.

Ningeliomba hili swala la kushuka elimu tulifungulie thread yake PEKE YAKE. Ni swala Muhimu sana kwa watoto wetu na future ya Taifa. Ukiweza basi anzisha thread yake peke yake maana mie naenda kulala, mmenishindisha hapa leo, upppsss!!!!
 
did you say that???
Zakumi banned for 80 years
Na wewe ni zao la UDSM?

Hahaha...Zakumi kweli uzalendo umekushinda:embarrassed:

@Ivuga: Yes I did. Kama unaweza kuishi kwenye jamii ambayo itakufanya utoe mchango kwa jamii. Kwanini uendelee kuishi na jamii yenye mawazo kama ya project ya sayansi iliyoshindwa ya mwanafunzi wa darasa la tatu.
@Omega Psi Phil: Sikupita UDSM. Lakini mimi ni nani wa kutathimini UDSM? Na wana UDSM wataita Mzumbe, SUA au UDOM modern high schools. Lakini wao ni nani wa kutathimini wenzao? Kuweni humble na elimu zenu.
@Mkubwa Dawa: Kurudisha passport sio kitu rahisi. Lakini pumba kama hizi za hapa, zinafanya usi-regret uamuzi wako.

Anyway, political capital ya Mbunge yoyote kama vile Zitto ipo kwa wale wanaomchagua. Mimi ni nani wa kumwambia kuwa alichofanya ni vibaya wakati hata kwenye daftari la uraia simo.
 
Sawa bwana wewe na "proffessional job" yako. Mtu wa UDSM unadhihirisha kabisa.

Ungesoma posts kwa makini, ungejua hapa kuna maswala mengi zaidi ya ujuzi lugha yanazungumzwa.

Kuna fraud hapa. Kuna decision making hapa. Kuna stereotype hapa. Kuna political intrigue hapa.

Lakini kwa sababu wewe unaongelea "proffessional job" huwezi kuona depth yoyote.

Wewe na mwenzako Zitto hamchekani, mmenyonya ziwa moja.

Yaani unadhihirisha zaidi tu kwamba UDSM ya "tragedy of the commons" na mediocrity si ki fluke cha mtu mmoja, ni pattern.

Tatizo lako wewe ni mwepesi mno kurukia nje ya hoja na kupersonalize mijadala labda nikukumbushe ulikotokea

quote_icon.png
Originally Posted by Kiranga
why did nyerere supported.....Why did nyerere opposed

Hizi lugha za watu jamani hizi, zinaumbua sana.

Ndiyo mambo ya UDSM tuliyokuwa tunasema hapa. Huyu ni Zitto Kabwe au mshashi tu kajibandika jina? Maana kama Kabwe hatari. Naona nataka kuwa kama yule mchizi aliyekuwa anadai Regia atoe namba yake ya kadi CHADEMA ndiyo aamini kwamba anayeandika madudu yale ni Regia.

Zitto anaharibu mpaka nakuwa siamini kama ni Zitto wa kweli au wa kuchonga.

Lakini kwa products za UDSM siwezi kushangaa.

Sihitaji kusoma kwa makini maelezo yako hapo juu kujua ulikuwa unazungumzia nini! With just that one sentence tayari umeshamjudgge Zito na the so called UDSM products.
 
Kwa hiyo major yako ilikuwa Kiswahili au Kifaransa? Na hakukuwa na electives nje ya major yako? Au wewe unazungumzia Kiingereza kama somo?

Na ulimaliza lini UDSM? Kama hautajali kutuambia.....

Mkuu twende tartiibu, mjadala ulianzia hapa
quote_icon.png
Originally Posted by Kiranga
why did nyerere supported.....Why did nyerere opposed

Hizi lugha za watu jamani hizi, zinaumbua sana.

Ndiyo mambo ya UDSM tuliyokuwa tunasema hapa. Huyu ni Zitto Kabwe au mshashi tu kajibandika jina? Maana kama Kabwe hatari. Naona nataka kuwa kama yule mchizi aliyekuwa anadai Regia atoe namba yake ya kadi CHADEMA ndiyo aamini kwamba anayeandika madudu yale ni Regia.

Zitto anaharibu mpaka nakuwa siamini kama ni Zitto wa kweli au wa kuchonga.

Lakini kwa products za UDSM siwezi kushangaa.

And that is why nikakoment specifically on that kwamba huhitaji kwenda UDSM kujifunza hili.
 
Nani kasema unahitaji kwenda UDSM kujifunza hili ?

Naona na wewe unahitaji kujifunza lile somo la LOGIC as suggested in one of the threads. Well umekosoa sentensi, ukaja na ur own clarification mwisho ukakonclude "zao la UDSM"
 
Naona na wewe unahitaji kujifunza lile somo la LOGIC as suggested in one of the threads. Well umekosoa sentensi, ukaja na ur own clarification mwisho ukakonclude "zao la UDSM"

Kwa hito sentensi ya Zitto ndio itumike kutuhukumu wahitimu wote wa UD? Kuna watu humu wanahitaji kupimwa akili sio bure.
 
Naona na wewe unahitaji kujifunza lile somo la LOGIC as suggested in one of the threads. Well umekosoa sentensi, ukaja na ur own clarification mwisho ukakonclude "zao la UDSM"

Elimu yetu ya chini inajulikana udhaifu wake, inasikitisha lakini ndiyo hali halisi.

Siwezi kuilaumu fully shule ya Ujiji huko alikosoma Zitto kwa sababu Zitto hajui kiingereza cha darasa la nne, naweza kuilaumu kidogo.

Lakini kwa sababu Zitto aliweza kuendelea akapita Chuo Kikuu cha Dar na udhaifu wake ukabaki pale pale, akawa na Kiingereza kibovu kuliko cha darasa la nne, basi hii inaonyesha UDSM kuna kupoteza wakati sana. Mtu atasoma vipi chuo kikuu ambacho lugha ya kufundisha ni kiingereza, ka miaka mitatu au minne, bila kujua kwamba "did supported" is a no-no ?

Wewe mtu kamanda jeshini, huko nyuma alipitia uskauti, akafuzu, akafika mpaka JKT, akapita, akaenda mpaka Monduli Military Academy akapita, kama hajui hata kujenga tent, kitu alichofundishwa tangu scout, na jeshini alitakiwa anakitumia kila siku, surely scout watakuwa na lawama yao, lakini hawa Monduli ndio kabisaaa, wataonekana hata kazi za kiskauti wameshindwa kumuwezesha huyu mwanajeshi.

Vivyo hivyo kwa Zitto Kabwe. Zitto angekuwa na elimu ya darasa la saba, tungelaumu kidogo hiyo shule yake ya msingi, lakini tungesema under the circumstances wamejitahisi. Lakini Zitto ana elimu ya Chuo Kikuu, inaonekana basi hapo Chuo Kikuu wtu hawajifunzi kitu maana hata lugha ya mawasiliano wanachapia, sasa wanawasiliana vipi? Si ndiyo hapo wanaanza mambo ya kubahatisha.

Halafu hata ukiacha lugha, kama wanavyosema wengine. Mtu aliyeelimika, mwanasiasa anayejua rule of law, accountability, historia yetu ya kupenda humility na ku shun arrogance, anaweza kusimama na kusema kwa kujivuna kabisa, macho makavu " I am unpredictable" na vimifano uchwara vya kina Nyerere humo humo.

Hivi hata ukiacha mambo ya lugha, unaona mtu huyu kaelimika kweli huyu? Yaani nilitegemea hata mazezeta ya UDSM yaweze kujua kwamba siasa is all about projecting humility and predictability, it makes people comfortable, it is elegant, it even makes markets comfortable.

Mtu kasoma uchumi anajivunia unpredictability ? Mbunge wa watu sensitive kama watanzania anajitangaza arrogance yake ?

Waliompigia kura kwa kufikiri wanamfahamu leo wakisikia jamaa kasema yeye unpredictable watajisikiaje? Mtu anayetengeneza controversy kirahisi hivi kaelimika huyu? Nilitegemea hata the worst from UDSM wawe way above this despicable mockery of a parliamentarian.
 
Fuatisha thread sio unarukia train kwa mbele tu.

BTW, 'Mr.I know everything', nakusubiria unipe article yako kutoka kwa journal ambayo (nanukuu) 'siwezi kuinunua' (kwa sababu ni mapedeshee tu kama wewe ndio wenye kuimudu gharama yake), ili tujifunze umahiri wako wa kutumia 'dictionary' ya lugha ya mama..

fingers crossed...
 
BTW, 'Mr.I know everything', nakusubiria unipe article yako kutoka kwa journal ambayo (nanukuu) 'siwezi kuinunua' (kwa sababu ni mapedeshee tu kama wewe ndio wenye kuimudu gharama yake), ili tujifunze umahiri wako wa kutumia 'dictionary' ya lugha ya mama..

fingers crossed...

Unaniwekea maneno si yangu.

Siwezi ku compromise privacy yangu kwa misifa, kunja vidole mpaka vikatike.
 
Hujaonyesha kama umefuatisha, ungefuatisha ungeona pattern ilivyojichora kwa wenzako .

Nikiangalia tu post yako ya kwanza naeza kujua upeo wako finyu, prejudices na complexities ulizonazo kuhusu UD na wahitimu wake, na hii sio mara ya kwanza.

Sasa cut the crap na hiyo sijui kufuatisha sijui treni, wewe ni hater tu wala huna mpango wowote.
 
Nikiangalia tu post yako ya kwanza naeza kujua upeo wako finyu, prejudices na complexities ulizonazo kuhusu UD na wahitimu wake, na hii sio mara ya kwanza.

Sasa cut the crap na hiyo sijui kufuatisha sijui treni, wewe ni hater tu wala huna mpango wowote.

A wise man once told me, don't argue with a fool
Cause people from a distance, can't tell who is who
-Guru
 
Back
Top Bottom