Re:Montesorri College na Sheria Ngumu

Zanzibar Spices

JF-Expert Member
Jul 14, 2013
7,362
2,000
Jamani hembu niambie kama kuna mtu amekutana na haya na kama ni kweli au la.

Nina Sisters wangu wawili niliwapeleka pale kwa Interview ya Kozi ya Ualimu.
Waliingia kwenye Interview Huku wamevaa Shungi kama kawaida.

Then baada ya Interview wakawa wamefanya vizuri na kuambiwa kwamba wamefaulu.
Ila Masharti ni kwamba hawatotakiwa kuvaa shungi na wanatakiwa kuacha vichwa wazi watakapoanza masomo rasmi kwa muda wote.
Sasa kwa sie waislam ni tatizo kubwa.
Ila cha kushangaza ni kwambwa kuna watawa(masisters)wao hawaambiwi kitu na kuruhusiwa kuvaa kama wanavyotakiwa na kufunika vichwa kwakuwa ni watawa.

Je hii ni kweli ni utaratibu wao au la?
Na kama ni kutokufunika kichwa kwa Mabinti waumini wa Kiislam je inakuwaje masisters(watawa)wao wanaruhusiwa?

Na Kibaya Zaidi ni kwamba interview niliambiwa ni Tsh:15,000 kwa kila mmoja,na masharti hayo hawakuambii mwanzo,maana kama ingekuwa ni mwanzo baadhi ya watu wangeingia mitini.Ila interview wanakuachia uingie kama ulivyokuja,baada ya interview ndio wanakuambia kwamba umefauli ila shungi hapa hazitakiwi ila kwa watawa tu.No refund for Interview fees.

Montessori ni wazuri sana na wanafanya vizuri sana kitaalum na wahitimu wao ni mahiri sana kwenye nafasi zao

Je nikweli huu ni utaratibu au mwalim alieutoa alikuwa na sababu zake binafsi
 
Undisputed

Member
Nov 8, 2013
40
0
Ni chuo cha masista kile hata viongozi asilimia kubwa ni masista mi nadhan sometym ukitaka cha uvunguni sharti.... na kama unaweza hauwezi utahathiri imani yako ni bora ukaacha kujiunga! waambie ndugu zako wafanye maamuzi sahihi! Montessori wapo vizuri sana. wakitoka pale hawakosi kazi! kazi yetu kushauri tuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuu...
 
Feiaidan

JF-Expert Member
Jun 1, 2013
204
225
Nafikiri itakuwa wameweka hizo taratibu kulingana na imani yao, kama ni cha masister itakuwa ndio sababu wanatoa kipaumbele kwa masister tu, lakini ni heri kwamba wanapokea na watu wasio masister.
 
barafu

JF-Expert Member
Apr 28, 2013
6,714
2,000
Mkuu viremba vya masista si ushungi,kuna tofauti ya ushungi na kiremba cha masista
Pili,mtaka cha uvunguni sharti ainame, tusifungwe na taratibu ambazo si amri ktk kuyafiikia malengo yetu.
Kila mahali na utaratibu wake,”When you are in Rome,Do as the Romans do“.Kwa hadhi ya Montessori sio watu wa kukudhlumu hiyo Tsh 15,000/=,kama wangekuwa na hila ya kukukatalia wala hata wasingekuita ktk kujiunga nao.Kila mahali na taratibu zao,sio tu ushungi pale hawataki vikorombwezo vingi,wana kikomo cha mavazi,vyakula na maisha kwa ujumla...wanajua kulea wanawake,kiukweli hata mkeo akisoma pale atakulelea vizuri sana watoto.
Kumbuka Montessori ndio wakufunzi wa walimu wa chekechea karibu Dunia nzima,marais wengi wakubwa Duniani wamepita ktk mikono yao,cheti chao kinauzika ndani na nje ya nchi,brand yao ni kama Cocacola,McDonald,Nike,Sony,Gucci,L'evis,Toyota au Honda.
Sijawahi kujuta kumpeleka mke wangu kusomea ualimu wa chekechea,kanilelea watoto wangu vizuri sana,kwa kweli hawa jamaa wanajua namna ya kumfundisha mtu kujua Saikolojia ya mtoto,licha ya mimi kuwa na Masters,nimekuwa “mwanafunzi“ wa mke wangu kwa mambo mengi yahusuyo watoto na ukuwaji wao.
Ondoa dhana ya ubaguzi,wangetaka kuwabagua ndugu zako hata kuwaita wasingewaita.Wapeleke dada zako,siku wakija kutambua waliiacha nafasi ya kujifunza montessori kisa hijabu watakuwa wamechelewa sana,Ni ushauri tu,bado imani yako ni ya muhimu,ni uamuzi wako kuchagua.
 
mwantui

JF-Expert Member
Mar 22, 2011
1,624

You deserve to be a great thinker..
 
NDEKUYO

Senior Member
Oct 6, 2012
184
225
Ila nyinyi Waislamu mna mtihani kweli. Mmechelewa kusoma kisa nguruwe ajabu wengine shku za leo mnakula sasa tena usipate taaluma kisa hijabu huo ni ujinga kabisa. Anzisheni chuo chenu mbona pale chuo kikuu chenu pale mnawalazisha wanawake wote wavae hijabu?
 
Zanzibar Spices

JF-Expert Member
Jul 14, 2013
7,362
2,000
Unajua ukiwa hujazaliwa mikoa ya pwani ni mtihani sana kwa badhi ya watu.
Kiswahili tabu sana.
Shungi,Kilemba ,hijabu an Nikabu ni vitu tofauti kabisa

Huyu mwingine nae zuzu anasema nguruwe,na mada hii haihusiani kabisaa,sijui kama sio wale wa Division 5
kwani hata huo Ukristo wapi umehalalisha nguruwe na Pombe siku ya sikukuu kama leo.

Mada iliulizwa eleza kwa uelewa wako kama walivyoeleza kina ,Undisputed,Masulubwete na Feiaidan

Hakukuwa na swala la ubaguzi,ilikuwa swala la kujua na kupata ufafanuzi
Anyway,kila mtu na uwezo wake wa kufikiria na uwezo wake wa kufafanua
 
NDEKUYO

Senior Member
Oct 6, 2012
184
225
Usilete dhalau ww kuna mtu wa dv 5 hapa duniani? Lakini pia ni ufahamu wenu nyinyi watu bado naamini ni mtihani hakuna namna ya kujitoa hapo. Maada nje ya ufahamu wako una maudhui ya udini unavyosema masister then unataka dada zenu akina Asha na mwanaharabu wafanane hapo umegusa udini. Shungi na hijabu ndiyo yale yale mtajua wenyewe. Nikusadie nimekulia Bagamoyo nimesoma Bagamoyo Sek nina masters na ninafanya vizuri sn kwenye taaluma yangu. Nasisitiza waisilaam acheni kulalamika tafute namna ya kujikwamua.
 
Mkuu yani kukuelewesha kooote kule bado tunatukanana??
 
Rakeem

Member
Aug 9, 2011
94
0
Usilete dhalau ww kuna mtu wa dv 5 hapa duniani? Lakini pia ni ufahamu wenu nyinyi watu bado naamini ni mtihani hakuna namna ya kujitoa hapo. Maada nje ya ufahamu wako una maudhui ya udini unavyosema masister then unataka dada zenu akina Asha na mwanaharabu wafanane hapo umegusa udini. Shungi na hijabu ndiyo yale yale mtajua wenyewe. Nikusadie nimekulia Bagamoyo nimesoma Bagamoyo Sek nina masters na ninafanya vizuri sn kwenye taaluma yangu. Nasisitiza waisilaam acheni kulalamika tafute namna ya kujikwamua.

Mjomba mbona una panic hivyo.Siku hizi kila mtu ana masters kaka usione kama ndo omega.Waislam wajikwamue na nini kaka
 
Zanzibar Spices

JF-Expert Member
Jul 14, 2013
7,362
2,000
Duh,kweli jamaa amepanic.Pole Mshkaji kwa ulivyonielewa
Nilifkiria atasema la maana.
Kumbe Masters?mbona zipo mtaani sana kama njugu
Maana na ulichoandika wewe ndio balaa zaid,maana udini kabisaa.
Masters hizi za kufanyia mtihani usimtishi mtu,kuna mwezio aliingia na elimu hii akasema anaomba msaada wa mwalim wa Kiingereza cha kuandika na kuongea.Na kama una Masters na umenielewa na kujibu hivyo,basi ni masters ya kichina na ninawasiwasi juu ya uelewa pia,na nyie ndio mnadharaulisha wenye Masters makini.

Anyway,samahanini nyote mliokwazika na topic hapo juu.
Unajua mi nipo Zanzibar,na sikujua kama ni chuo cha masisters na nilijua ni chuo Binafsi na ndio maana niliandika vile.
Samahanini sana kwa nyote mliokwazika na Topic hii na pia Samahani kwa Uongozi wa Montessori kwa kueleweka vibaya.

Pia ningeomba Moderator a Remove these posts ilu kuondoa huu mkanganyiko ambao mwisho wake unaonekana hauna jema kwa sote.
 
lutamyo

JF-Expert Member
Apr 13, 2011
641
250
mkuu, heshimu taratibu za watu, mfano mzuri ni shule na chuo cha kiislam cha weepers kibaha huingii getini bila kufunika kichwa hata kama unaenda kumsalimia ndugu yako humo chuoni na hiyo ina aply hadi kwa wafanyakazi na vibarua wote plus wageni wote. nakushauri wapeleke weepers
 
Edward Teller

JF-Expert Member
Oct 31, 2010
3,905
2,000
Jamani hembu niambie kama kuna mtu amekutana na haya na kama ni kweli au la.

Nina Sisters wangu wawili niliwapeleka pale kwa Interview ya Kozi ya Ualimu.
Waliingia kwenye Interview Huku wamevaa Shungi kama kawaida.

Then baada ya Interview wakawa wamefanya vizuri na kuambiwa kwamba wamefaulu.
Ila Masharti ni kwamba hawatotakiwa kuvaa shungi na wanatakiwa kuacha vichwa wazi watakapoanza masomo rasmi kwa muda wote.
Sasa kwa sie waislam ni tatizo kubwa.
Ila cha kushangaza ni kwambwa kuna watawa(masisters)wao hawaambiwi kitu na kuruhusiwa kuvaa kama wanavyotakiwa na kufunika vichwa kwakuwa ni watawa.

Je hii ni kweli ni utaratibu wao au la?
Na kama ni kutokufunika kichwa kwa Mabinti waumini wa Kiislam je inakuwaje masisters(watawa)wao wanaruhusiwa?

Na Kibaya Zaidi ni kwamba interview niliambiwa ni Tsh:15,000 kwa kila mmoja,na masharti hayo hawakuambii mwanzo,maana kama ingekuwa ni mwanzo baadhi ya watu wangeingia mitini.Ila interview wanakuachia uingie kama ulivyokuja,baada ya interview ndio wanakuambia kwamba umefauli ila shungi hapa hazitakiwi ila kwa watawa tu.No refund for Interview fees.

Montessori ni wazuri sana na wanafanya vizuri sana kitaalum na wahitimu wao ni mahiri sana kwenye nafasi zao

Je nikweli huu ni utaratibu au mwalim alieutoa alikuwa na sababu zake binafsi
nenda zanzibar kavue samaki-kila siku hamuishi kulalamika
 
platozoom

JF-Expert Member
Jan 24, 2012
9,002
2,000
Duh,kweli jamaa amepanic.Pole Mshkaji kwa ulivyonielewa
Nilifkiria atasema la maana.
Kumbe Masters?mbona zipo mtaani sana kama njugu
Maana na ulichoandika wewe ndio balaa zaid,maana udini kabisaa.
Masters hizi za kufanyia mtihani usimtishi mtu,kuna mwezio aliingia na elimu hii akasema anaomba msaada wa mwalim wa Kiingereza cha kuandika na kuongea.Na kama una Masters na umenielewa na kujibu hivyo,basi ni masters ya kichina na ninawasiwasi juu ya uelewa pia,na nyie ndio mnadharaulisha wenye Masters makini.

Anyway,samahanini nyote mliokwazika na topic hapo juu.
Unajua mi nipo Zanzibar,na sikujua kama ni chuo cha masisters na nilijua ni chuo Binafsi na ndio maana niliandika vile.
Samahanini sana kwa nyote mliokwazika na Topic hii na pia Samahani kwa Uongozi wa Montessori kwa kueleweka vibaya.

Pia ningeomba Moderator a Remove these posts ilu kuondoa huu mkanganyiko ambao mwisho wake unaonekana hauna jema kwa sote.

Kwa hiyo utawaondoa sisters wako kwa sababu baadhi ya Watu humu wamekusema vibaya!
Take it positively, angalia na pembua kama inafaa uwapeleke. Msome barafu hapo juu utapata kitu kizuri.
Ni wazi Montesori ni Chuo kizuri, ni uchaguzi wako kuangalia mizania ya uzuri na ubaya.

Ingawa unasema hukujua kama "ni chuo cha masista", hilo naona ni kupotosha. Kwa sababu kabla ya hapo uliwaona 'ma-sisters' na bila shaka ndiyo wasimamizi wakuu. Na naamini unajua wanatoa kozi ya ualimu ambayo ndiyo Dada zako wanataka kufanya.

Usikwazike hii ni 'social network na inakusanya kila aina ya Watu katika nyanja na makundi tofauti.

Good luck.
 
NullPointer

JF-Expert Member
Feb 7, 2011
3,465
2,000
Mbona wako sawa kabisa.. mkristo siku nikitaka kuja msikitini na viatu since kanisani tunaingia navyo, si kitawaka kwangu siku hiyo? Sasa ndio situation kama hiyo, kwa kua yupo kwao sheria zao inabidi azifuate tu au kama hawezi basi aende kwingine, its a pity kua tuna differences ila hatuna budi kuvumiliana.
 
Zanzibar Spices

JF-Expert Member
Jul 14, 2013
7,362
2,000
Labda hapa niweke sawa,nahisi sijaeleweka kwa baadhi ya watu,na watu wanachukulia kama Jazba zakidni.
Hapa issue ya udini haipo.
Mie najua kwamba kuna shule za kila dini ambazo zinaweka utaratibu wa mfumo wa kidini kwenye shule zao au vyuo vyao iwe kwa Wasilam,Wakristo nk

Sio kwamba nilikuwa najua ni utaratibu gani upo pale na mtu huwezi kumalazimisha mtu akuelewa kulingana na upeo wake.
Labda kwa taarifu ni kwamba Pale walikuwa Recommmedned na Rafii yao na yeye pia ni Muislam na alisoma pale.
Kwa uifupi kile Chuo hakichangua Muislam wala Mkristo na wala hawana udini zaidi ya hilo nililoomba ufafanuzi licha ya kwamba sikueleweka.

Dada zangu wao wali ni update all fees na taratibu zao after Interview
Mie Nipo Zanzibar na wala sijawahi kwenda na sijui kipo wapi,sasamtu kunishambulia kwamba nilikuwa najua taratibu zao mara oo umeenda plae umakuta masisters,nakuwa namie simuelewi na ndio maana hii topic inaonekana ni ya kidini,ila kwa mtu mwenye kupitia amelezo yangu ni kwamba atakuwa alinielewa nilikuwa na maana gani na nilikuwa nataka kujua nini.

Sasa kwa hali hio,baada ya wao kunitarifu juu ya utaratibu ndio nikaona niulize humu kama hilo lipo,na kwakuwa sikukujua ni Chuo cha mission.Ila kama ningejua ni Chuo kipo chini yauangalizi wa masister basi wala nisingeleta hii post,ningekuwa nimeisha ju.Mie nilijua ni Chuo cha kawaida tu

Nisingependa nielewke vibaya kwa hili na wala sio nia kuharibu jina la hiki chuo,na ja waislamu wngi sana wapo pale wanasoma na hata Dada zangu walikuwa recommended na wenzao ambao ni waislam waliosoma pale ambao wapo kwenye ajira nzuri na wapo vizuri kitaaluma.

Samahanini kwa usumbufu juu ya hili
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom