Kwanini NHIF inaweka sheria ngumu kwa wanachama wake

T-Bagwell

JF-Expert Member
Apr 6, 2017
1,174
2,290
Habari za muda huu wadau.

Mimi ni mwanachama wa NHIF kwa taktibani miaka 10 sasa lakini kuna baadhi ya changamoto nilkua nazipitia nyingine nilikua nazisikia kwa wanachama wengine lakini week iliyopita ndipo lilinikuta jambo.

Week iliyopita nilienda hospitali flani ambayo ni mbali kidogo na ninapoishi (100Km+) kwa lengo la kupata matibabu (Hospitali hiyo ndiyo hua nafanyiwaga matibabu mara kwa mara)

Kutokana na dharura iliyonikuta nilijikuta nimesahau kadi yangu ya bima.

Nilifika hospitali hapo majira ya tano Asububi, Na maongezi yalikua kama hivi.

Mimi: Habari dada, naitwa xxxx nimekuja kwaajili ya matibabu lakini kwa bahati mbaya nimesahau card ya BIMA na ninatokea mbali kidogo, je naweza kupata huduma?

Mhudumu: Hapana.

Mimi: Lakini namba za card ya bima ninayo?

Mhudumu: Hapana, mpaka utakapokua na card.

Mimi: Je nikiomba mtu anisaidie kuipiga picha kisha akanitumia naweza kupata msaada.

Nilikaa kama dakika 2 nikiwa nawaza nini cha kufanya huku nikimuangalia yule dada. Ghafla mhudumu mwingine aliyekua pembeni yake akaanza kuongea.

Mhudumu: Labda uende ofisi za BIMA uwaombe wakupe copy ya kitambulusho/utambulisho wa muda ndipo unaweza kupata huduma.

Mimi: Ahsante, Ofisi za Bima zinapatikana wapi hapa.

Yule mhudumu wa pili akanielekeza nikiwa na matumaini ya kupata huduma kwa siku hiyo kwasababu nilikua na ruhusa ya siku hiyo tuu kazini.

Mnamo saa Sita mchana nilifika ofisi za NHIF nikawaelezea yaliyotokea na lengo la mimi kufika pale.
Lakini nilichojibiwa ni kwamba “HATUNA HUDUMA HIYO”

Nikauliza, je nitapaje huduma kwasababu ninapotoka ni mbali, akanijibu mpaka card ipatikane nikasema kama nika report kama card imepotea je naweza kupata huduma ya dharura?

Nilichojibiwa ni kwamba process za kupata card ni lazima niende kituo cha polisi kupata loss report kisha niende kwa muajiri kisha nifike ofisi za NIDA.

JE, KUNA ULAZIMA GANI WA MWANACHAMA KUWA NA CARD ORIGINAL NDIPO APATIWE HUDUMA?
 
Dunia imehamia kwenye number ila msomi wa kitanzania wala haelewi. Na hayo ndiyo madhara ya elimu za kukariri. Halafu unaweza kushangaa waliokujibu hivyo wote ni degree holders.

Kwa mbaali ningeelewa kama ID ingekuwa haina namba ila ina mfumo wa kuscan/kuchanja.
 
Habari za muda huu wadau.

Mimi ni mwanachama wa NHIF kwa taktibani miaka 10 sasa lakini kuna baadhi ya changamoto nilkua nazipitia nyingine nilikua nazisikia kwa wanachama wengine lakini week iliyopita ndipo lilinikuta jambo.

Week iliyopita nilienda hospitali flani ambayo ni mbali kidogo na ninapoishi (100Km+) kwa lengo la kupata matibabu (Hospitali hiyo ndiyo hua nafanyiwaga matibabu mara kwa mara)

Kutokana na dharura iliyonikuta nilijikuta nimesahau kadi yangu ya bima.

Nilifika hospitali hapo majira ya tano Asububi, Na maongezi yalikua kama hivi.

Mimi: Habari dada, naitwa xxxx nimekuja kwaajili ya matibabu lakini kwa bahati mbaya nimesahau card ya BIMA na ninatokea mbali kidogo, je naweza kupata huduma?

Mhudumu: Hapana.

Mimi: Lakini namba za card ya bima ninayo?

Mhudumu: Hapana, mpaka utakapokua na card.

Mimi: Je nikiomba mtu anisaidie kuipiga picha kisha akanitumia naweza kupata msaada.

Nilikaa kama dakika 2 nikiwa nawaza nini cha kufanya huku nikimuangalia yule dada. Ghafla mhudumu mwingine aliyekua pembeni yake akaanza kuongea.

Mhudumu: Labda uende ofisi za BIMA uwaombe wakupe copy ya kitambulusho/utambulisho wa muda ndipo unaweza kupata huduma.

Mimi: Ahsante, Ofisi za Bima zinapatikana wapi hapa.

Yule mhudumu wa pili akanielekeza nikiwa na matumaini ya kupata huduma kwa siku hiyo kwasababu nilikua na ruhusa ya siku hiyo tuu kazini.

Mnamo saa Sita mchana nilifika ofisi za NHIF nikawaelezea yaliyotokea na lengo la mimi kufika pale.
Lakini nilichojibiwa ni kwamba “HATUNA HUDUMA HIYO”

Nikauliza, je nitapaje huduma kwasababu ninapotoka ni mbali, akanijibu mpaka card ipatikane nikasema kama nika report kama card imepotea je naweza kupata huduma ya dharura?

Nilichojibiwa ni kwamba process za kupata card ni lazima niende kituo cha polisi kupata loss report kisha niende kwa muajiri kisha nifike ofisi za NIDA.

JE, KUNA ULAZIMA GANI WA MWANACHAMA KUWA NA CARD ORIGINAL NDIPO APATIWE HUDUMA?
Pole sana mkuu
Ni ukiritimba tu wa serikali.
 
Kakweli ni miomgoni mwa mashirika ya hovyo yuliyonayo Karnes
ya 21,mbaya zaidi tunalizimishwa kutumia watumishi wa umma badala ya kuwa ni option au ushindani ili mtu uamue utumie Bima gani inayoendana na mazingira!
 
Wanaweza kutatua hizo changamoto kwa

Bio verification kama fingerprint
Pia zikihuishwa na NIDA taarifa zote zioane.
Sidhani kama kuna ugumu sana.

Waligoma na ukiacha hayo nipo na file hospitali hapo kwasababu hua nativiwaga hapo.
 
Kakweli ni miomgoni mwa mashirika ya hovyo yuliyonayo Karnes
ya 21,mbaya zaidi tunalizimishwa kutumia watumishi wa umma badala ya kuwa ni option au ushindani ili mtu uamue utumie Bima gani inayoendana na mazingira!

Niliwaza nikasema kama wangeruhusu watu kuhama basi ni dhahiri shirika lingefungwa,

Changamoto ni nyingi… nina mfanyakazi mwenzangu jina lake na la mzazi wake limetofautiana herufi moja tuu lakini wamegoma kumkampatia BIMA.
 
Back
Top Bottom