Lizaboni
JF-Expert Member
- Feb 21, 2013
- 33,894
- 20,375
Kuna kila dalili za viongozi wa sasa kucopy na kupaste tabia mbaya ya kuhamisha mtu anayevuruga katika eneo moja na kumpeleka eneo jingine. Nimesikitishwa sana na kitendo cha Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kumhamisha RPC na kumpeleka Mbeya eti kwa madai kuwa Mbeya haina Changamoto nyingi kuliko Mwanza. RPC hajaondoka peke yake bali na wasaidizi wake pamoja na Afisa Usalama wa Taifa. Hii ni fedheha kubwa kwa Mongella kwani ulichofanya ni sawa na kuondoa kinyesi chumbani kwako kwa madai kinatoa harufu kali na kukipeleka kwenye sebule ya jirani yako.
Hakika hii ni fedheha kubwa sana na ni aibu kwake. Nani asiyekumbuka jinsi Mbeya ilivyokuwa inakumbwa na matukio kadhaa ya Ujambazi enzi zile tangu Suleiman Kova akiwa RPC na muda mfupi baada ya kuondoka kwake? Nani asiyejua hilo? John Mongella, hivi unajua kwa nini ujambazi na matukio ya kipuuzi kama yale ya kuchuna ngozi watu yalishamiri sana enzi hizo na sasa yamekomeshwa? Kwa nini Mbeya unawapelekea mzoga uliowashinda kula wana Mwanza? Unataka Mbeya waanze kuishi tena kwa hofu ya kuchunwa ngozi?
Rais wangu Magufuli, naona sasa hawa wakuu wako wa Mikoa hasa wale waliokuwepo enzi zile wanaonekana kutaka kukuharibia. Inaonekana ndani yao wana ajenda ya siri ya kutaka kukuharibia ili ionekane haufanyi kazi. Kitendo cha kumhamisha RPC aliyeshindwa kazi Mwanza na kumpeleka Mbeya ni kuendeleza yale yale yaliyokataliwa na wananchi. Nakumbuka kwenye mikutano yako ya kampeni ulilieleza bayana hilo kuwa hutamhamisha mtu anayevuruga kwenye eneo jingine. Inasikitisha sasa kuona baadhi ya viongozi na watendaji wako wameanza kukiuka yale uliyoahidi na uliyoanza kuyatekeleza kwa nguvu zako zote na wananchi tunakuunga mkono.
Kama Mongella una ushahidi kuwa viongozi hao uliowatimua wamechangia kwenye matukio kadhaa ya ujambazi ama wameshindwa kuchukua hatua, suluhisho si kuwahamisha bali washughulikiwe kama wengine wanavyoshuguulikiwa. Sheria ni msumeno. Si wakiguswa watu wa kada nyingine wanashughulikiwa kwa nguvu kubwa ila wakiguswa wa kada nyingine mnawahamisha. Hiyo inajenga double standard ambayo haitakiwi katika utawala huu wa awamu ya tano.
Nawasilisha.