RC wa Arusha aanza uigizaji baada ya tetesi kuwa anahamishiwa Shinyanga

Crashwise

JF-Expert Member
Oct 23, 2007
22,227
8,739
Kuna tetesi kwamba RC Ntibenda wa hapa Arusha anapelekwa Shinyanga sasa haikueleweka ni kichaa gani leo kilimkumba RC huyo akaita waandishi wa habari akiwaambia anaenda kukabidhiwa madawati Fibre Board kufika kiwandani akaanza kwa kuzunguka ndani kiwanda kama vile mtu aliyepoteza pochi mara mwenyeji wake yaani mkurugezi wa Fibre Board kaja baada ya mazungumzo ya salamu akamwambia nimekuja unikabidhi madawati.

Mkurugezi huyo akamwambia mheshimiwa mbona tulikubaliana ni wiki ijayo RC kuona imekuwa soo kuwa madawati bado ikabidi aanze maigizo anakabidhiwa akapiga picha akiwa yeye RAS (Mapunda), DC wa Arusha( Nkurlu) pamoja na Hans Mkrugezi wa Fibre Board huku madawati yaliyokuwa yanaendelea yakionekana kwa nyuma, alipoulizwa mkurugenzi wa Fibre Board Tosky Hans alisema niliahidi madawati 1,000 na wiki ijayo yatakuwa yamekamilika leo tumefanya makabidhiano ya awali kama alivyotaka RC Makabidhiano rasmi ni wiki ijayo kwasababu hayajakamilika na tulikubaliana kuwa wiki ijayo yatakuwa yamekamilika.

Hivyo yeye na msafala wake wameyakuta yakiendelea kufanyiwa matengenezo ya mwisho tayari kwa makabidhiano ya wiki ijayo kama tulivyoahidiana alisema Hans, awali kulitokea kutokuelewana kati yake na wanahabari hasa wapiga picha akiwalaumu kwamba kwanini hawampigi picha alipokuwa kiwandani aliendelea kulalamikankuwa wanahabari wa arusha wamekuwa wakimhujumu mtafaruku huo uliishia kwa. Alice ambaye ni afisa Habari wa mkoa ametupiwa lawama na RC huyo kuwa ameshindwa kuwashawishi wanahabari kumpiga picha akiwa ndani ya kiwanda cha Fibre Board na kuahidi kumfukuza kazi..
 
Mkuu nasikia alikataza viroba sasa yeye atatumia nini maana ndio kinywaji chake nawasiwasi hata alivyokua anafanya hayo maigizo atakua alishatupia kakiroba
Nimekumbushwa kuwa ni laana imeanza kumnyemelea baada ya kupiga maarufuku walokole kuhubiri kwa kuonea kwasauti akisahau bar zinazopiga miziki..
 
Magu ataua watu, kilango wiki iliyopita amefanya sherehe kubwa sana huko kwao heeee!...
 
Nimekumbushwa kuwa ni laana imeanza kumnyemelea baada ya kupiga maarufuku walokole kuhubiri kwa kuonea kwasauti akisahau bar zinazopiga miziki..
Ndio Tatizo la maiguzo yeye ameona hana lake tena Arusha yupo chini ya CHADEMA mkoa karibia wote
 
Magu utawaua wateule wako! Hawajui unataka nini na unaelekea wapi! Wao wapo kama roboti! Wanasahau JD zao sasa wanaenda kwa mihemko na yanayojiri! Watajikuta mambo ya msingi wanachemsha kuyatekeleza! Mfano ajira na njaa....sijui kama wana mikakati ya kuzuia njaa na kuzalisha ajira! Wao wanacheza na media issue ndogo ndogo za kawaida! Sijasikia bado mikakati ya kutekeleza ile JD waliopewa! Shauri yao! Wengine wameanza vita n omba omba na parking kwenye magorofa! Sijui anatafuta nini kwa wamiliki wa maghorofa! Anaanza kuwashitaki waliotoa vibali vya ujenzi w maghorofa bila parking! Kosa la mtu mmoja au la kimfumo? Soon nae namuona atapotez focus!
 
Back
Top Bottom