Ni mwaka sasa tangu marehemu Omela Wangwe auwawe kwa kupigwa na Mwanajeshi ndani ya ofisi ya kata ya Kahama wilayani Ilemela.
Marehemu hakukamatwa kwenye tukio lolote, bali alipigiwa simu ili aje aeleze wapi alipata milango aliyokuwa anaiuza kama dalali na alikamatwa na watuhumiwa wanne na kupelekwa ofisi ya kata Kahama Ilemela baada ya kupigiwa simu aje asaidie upelelezi.
Alitokea mwanajeshi ambae alikuwa amepanga njama za kupata watu waliomuibia TV kwake. Na huyu mwanajeshi akishirikiana na migambo wa kata kwa ruhusa ya mtendaji wa kata walimpiga Omela Wangwe wakimhisia kuiba Tv ya mwanajeshi,ambae baadae alifariki Sekoutore Hospital.
Polisi kirumba walidanganya kuwa alipigwa na wanachi wenye hasira kali. Mke wa marehemu alikuona wewe mkuu wa mkoa. Uliagiza upelelezi ufanyike. Mwezi wa nne mwaka huu wapelelezi walienda Kata ya Kahama na walichukua maelezo watu walioshuhudia hili tukio,ukweli ulifahamika kuwa Omela Wangwe alipigwa ndani ya ofisi ya kata.
Jalada la kesi lilifunguliwa kwa mwendesha mashitaka wa mkoa wa Mwanza, mke wa marehemu aliambiwa watuhumiwa walitakiwa wakamatwe ili hatua stahiki zichukuliwe. Kwa mujibu wa mke wa marehemu Rco wa Mwanza alitoa amri watuhumiwa wasikamatwe.
Mke wa marehemu alikuja kukuona wewe mkuu wa mkoa ili umsaidie,na inasemekana bado mnafanya uchunguzi. Uchunguzi gani mnafanya kwa mtu aliyeuliwa kwa kupigwa mchana kweupe ndani ya ofisi ya kata?
Wewe kama mkuu wa mkoa umeshindwa hata kufanya mkutano wa hadhara ili kupata ukweli juu ya hili tukio?
Cc Wapenda haki wote.
Pia soma
- Mwanajeshi awatesa vijana na mmoja kufariki akiwatuhumu kumwibia tv yake. Je, hii ni haki?
- Polisi Mwanza mnaoshughulikia hii kesi, kuweni makini hii ni awamu ya tano, mtakuja kuumbuka