RC Makonda: Tutaweka utaratibu kwa wakazi wa Dar kufanya manunuzi kwa kutumia Credit Cards ili kudhibiti ulipaji kodi

Hivi ni wakazi wangapi wa Dar wana akaunti za benki na wanasifa ya kuweza kumiliki credit card?
Bora angeongelea malipo ya kielektroniki na si credit card. Hatuwezi kuendelea kwa kunakili tu yaliyofanyika huko kwenye mataifa yaliyoendelea saa nyingine ni bora tuangalie kwanza mazingira yetu kabla ya kuja tu na solution.
Hili swali wakikujibu Misukule wafuata upepo narudi kulala, labda wakitukane tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hi I Makonda anajua Credit card ni nini au anafikiri kila bank card ni credit card?
 
Hii inatofauti na overdraft?

Sent using Jamii Forums mobile app
Overdraft unakopeshwa cash over and above ya balance yako kwenye account. Unaweza uka-withdraw cash kwa kutumia debit card yako kama kawaida. Credit card huwezi ku-withdraw cash instead utaitumia for purchasing goods and service only. Mwisho wa mwezi utaletewa bill na utakatwa directly from the source i.e kutoka kwa mwajiri wako. Kama huna job security au reliable source of income bank haiwezi kutoa guarantee ya credit card kwako hata siku moja kwa sababu risk yake ni kubwa sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
I bet ukimuuliza bashite credit card ni nini? Hajui ...

Sio Bashite tu, hata baba yake Jiwe naye automatic hajui for sure....!!

Style yao ya kukurupukia mambo, emotions zao na haiba yao inafanana A - Z

Na inavyoonekana huwa hawafanyi kikao cha management team za ofisi zao kwanza kinachohusisha wataalamu na washauri mbalimbali kabla ya kutoka public ku - raise issue fulani....

Na kwa kutofanya hivi, matokeo yake ndo hayo sasa unatoka huko unazungumza vitu ambavyo dunia nzima inashangaa iwapo kweli huyu ni kiongozi wa rank ya juu kabisa serikalini...!!

Maana exposure na ufahamu wa mambo ni almost zero...
 
Anajuwa maana ya credit card lakini au anajisemea tu? Kama neno lilivyo CREDIT maana yake unanunuwa kwa MKOPO. Credit Card maana yake ni kadi ya mkopo.

Credit card inatolewa na financial institutions e g bank, co-op, n.k. na kuipata kwake mpaka uchunguzwe kama unavoomba mkopo kutizama uwezo wako wa kulipa na kila mteja huwekewa limit yake.

Kufanya kazi kwake ni kuwa unanunuwa kitu unaitumia kulipia na muuzaji hulipwa na aliyekupatia kadi hiyo kwa yeye kulipia % ndoogo sana ya fee kama 0.5%. Mteja unaletewa statement yako mwisho wa mwezi na kutakiwa uilipie kiwangu maalumu cha chini au unaweza kwa mkupuo mmoja ndani ya muda maalumu baada ya kutoka statement. Mara nyingi ni muda wa siku 30-45 kutoka siku uliyofanya manunuzi. Ukishindwa kulipa yote kwa mkupuo mmoja basi ile balance ya juu inaanza kuchajiwa riba na inakuwa kubwa sana riba yake. Na ukishindwa kulipa kabisa kabisa hata ile kiwangi cha chini walichokwambia ulipe basi kuna na fine ambayo nayo ni kubwa on top of ya ile riba inayopigwa hesabu kila mwezi. Utaendelea kutumia kadi yako mpaka ufikie limit uliyoekewa.

Kwa kifupi credit card ni short term loan. Ukiiendekeza ikawa ndio bank yako itakufilisi. Fees zake na riba ziko juu sana.

Tatizo kubwa ni kuwa 99.5% ya wakaazi wa Dar hatuna sifa ya kuwa na credit card!
 
Mkuu wa mkoa wa Dsm mh Makonda amesema ofisi yake itaandaa utaratibu ili wakazi wa jiji la Dsm wawe wanafanya manunuzi yao kwa kutumia credit cards badala ya fedha taslimu. Makonda amesema utaratibu huo ndio unaotumika katika miji mikubwa yote duniani ambako watu wanaotumia cash ni wachache sana.

Makonda amesema utaratibu huo utawezesha kudhibiti ulipaji wa kodi kwani utaratibu wa sasa wa kutumia EFD machines unatoa mwanya wa ukwepaji kodi.

Mkuu wa mkoa Makonda amesema hayo katika mkutano wake wa kazi na watendaji wote wa Halmashauri za jiji la Dsm pamoja na viongozi wa TRA mkoa wa Dsm.

Source: Estv habari

Maendeleo hayana vyama!

Tena unamvika title ya "Mheshimiwa"

Aheshimiweje na ujinga huu?

Watu wanamheshimu na kumpa credit mtu mwenye akili na maamuzi sahihi..!!

Marufuku kuanzia leo kumwita kiongozi yeyote "mheshimiwa fulani" unless aoneshe heshima hiyo wazi wazi na kila mtu aone....

Otherwise kumwita "ndugu fulani" is acceptable kwa sababu sisi sote ni ndugu haijalishi u kichaa ama mwerevu...

Hata Magufuli Pombe John, ni ndugu bila kujali hali yake ya uki.....
 
Anajuwa maana ya credit card lakini au anajisemea tu? Kama neno lilivyo CREDIT maana yake unanunuwa kwa MKOPO. Credit Card maana yake ni kadi ya mkopo.

Credit card inatolewa na financial institutions e g bank, co-op, n.k. na kuipata kwake mpaka uchunguzwe kama unavoomba mkopo kutizama uwezo wako wa kulipa na kila mteja huwekewa limit yake.

Kufanya kazi kwake ni kuwa unanunuwa kitu unaitumia kulipia na muuzaji hulipwa na aliyekupatia kadi hiyo kwa yeye kulipia % ndoogo sana ya fee kama 0.5%. Mteja unaletewa statement yako mwisho wa mwezi na kutakiwa uilipie kiwangu maalumu cha chini au unaweza kwa mkupuo mmoja ndani ya muda maalumu baada ya kutoka statement. Mara nyingi ni muda wa siku 30-45 kutoka siku uliyofanya manunuzi. Ukishindwa kulipa yote kwa mkupuo mmoja basi ile balance ya juu inaanza kuchajiwa riba na inakuwa kubwa sana riba yake. Na ukishindwa kulipa kabisa kabisa hata ile kiwangi cha chini walichokwambia ulipe basi kuna na fine ambayo nayo ni kubwa on top of ya ile riba inayopigwa hesabu kila mwezi. Utaendelea kutumia kadi yako mpaka ufikie limit uliyoekewa.

Kwa kifupi credit card ni short term loan. Ukiiendekeza ikawa ndio bank yako itakufilisi. Fees zake na riba ziko juu sana.

Tatizo kubwa ni kuwa 99.5% ya wakaazi wa Dar hatuna sifa ya kuwa na credit card!

Very good explanation, bro.....

Laiti ungekuwa "Special Advisor" wa RC huyu, pengine mambo yangekuwa tofauti na mashambulizi anayopokea sasa...!!

Na nadhani tatizo la viongozi wetu hawa sio issue ya elimu pekee...

Kwa sababu hata mtu aende shule na kumaliza madarasa yote duniani, si rahisi kuelewa/kuwa na ufahamu wa kila jambo...

Lililo muhimu ni kuwa tayari kujifunza siku zote, kila wakati. Hii ni zaidi sana kwa kiongozi wa umma wa kariba ya Mkuu wa Mkoa...

Kwa mfano, kwani kulikuwa na ugumu gani kabla ya kutoka hadharani na kuropoka jambo ambalo hata hana uelewa nalo kihivyo kufanya consultation ya wataalamu wake, wakamshauri na kujiridhisha kuwa akilitamka halitaleta taathira hasi kwa umma?

Pia mimi huwa najiuliza swali hili mara kwa mara juu ya viongozi wetu hawa wa kileo.....

Kwamba, hivi wanaelewa hata kuelewa tu kweli kuwa wao ni viongozi na kauli zao tu ziwe ndogo ama kubwa kama hazijafanyiwa utafiti wa kutosha zikitolewa kwa mihemuko binafsi tu zaweza kuwa na athari hasi kubwa sana ktk jamii na hata kumuathiri hata kiongozi mwenyewe?

Yeah, inawezekana ikawa ni selfish ego na kiburi cha ulevi wa madaraka tu....

Kwani mara nyingi tumewasikia viongozi hawa wakikosea na kujikuta wakipigiwa kelele na watu lakini majibu yao siku zote na mara zote yamekuwa:

"...kelele za mlango haziwezi kumzuia mwenye nyumba kulala ama hizo ni kelele za 'wasio wazalendo, wasioipenda nchi' na wanaoshirikiana na mabeberu wa Marekani na Ulaya tu.... "

Very funny eti eeeh? Yaani kiongozi mjinga afanye makosa ya wazi kabisa kwa kiwango hiki kwa sbb ya ego na ujinga wake akifikiri watu wote awaongozao ni wajinga kama yeye, then mwisho wa siku ajitetee kwa utetezi wa kijinga namna hii na watu wapige makofi na vigeregere tu??........ Aaaah, haiwezekani!!
 
Dar haijawa na maduka ya kufanya manuñuzi ya credit au debit card. Malipo kwa tigo na mpesa yenyewe bado sana. Massawe au Kimaro hahitaji credit card maana hela yake ataanza kuisumbukia tena.
M

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom