RC Makonda: Tutaweka utaratibu kwa wakazi wa Dar kufanya manunuzi kwa kutumia Credit Cards ili kudhibiti ulipaji kodi

Mkuu wa mkoa wa Dsm mh Makonda amesema ofisi yake itaandaa utaratibu ili wakazi wa jiji la Dsm wawe wanafanya manunuzi yao kwa kutumia credit cards badala ya fedha taslimu. Makonda amesema utaratibu huo ndio unaotumika katika miji mikubwa yote duniani ambako watu wanaotumia cash ni wachache sana.

Makonda amesema utaratibu huo utawexesha kudhibiti ulipaji wa kodi kwani utaratibu wa sasa wa kutumia EFD machines unatoa mwanya wa ukwepaji kodi.

Mkuu wa mkoa Makonda amesema hayo katika mkutano wake wa kazi na watendaji wote wa Halmashauri za jiji la Dsm pamoja na viongozi wa TRA mkoa wa Dsm.

Source Estv habari
Maendeleo hayana vyama!
Ile showroom ya kigamboni vip

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mmh credit card au debit card? Kuweni serious kidogo!
Nadhani bashite aliteleza ingawa hii kitu ya kadi haiepukiki. Naona watu wengi wananunua mafuta Total kwa vile kuna utafiti I wa kadi. Credit card kwa Tanzania yetu bado sana au vipi cariha ?
 
Huyu hajakoma tuu kauli kama hizi tujiulize waziri wa fedha,kamishna wa TRA wanajisikiaje wanaposikia kauli hii inatoka kwa mtu asiyehusika kabisa na kodi?

Je, kesho watu wa Dar wakiacha kutumia EFD mashine kwa kauli ya RC itakuaje?

Suala la credit card siyo la serikali kuamua bali miundo mbinu yenyewe itajipeleka huko.

Bora angehimiza malipo kwa mobile money M-PESA, Airtel money na tiGO Pesa maana hivyo vipo kwa kila raia.

ukiwa kiongozi na mawazo mazuri usingoje mpaka waziri mhusika aseme no umechaguliwa kutuongoza lete ubunifu wako wa maendeleo narudia tena lete ubunifu wako wa maendeleo usingoje aliyelala aseme

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Hakika mkuu!
 
Mkuu wa mkoa wa Dsm mh Makonda amesema ofisi yake itaandaa utaratibu ili wakazi wa jiji la Dsm wawe wanafanya manunuzi yao kwa kutumia credit cards badala ya fedha taslimu. Makonda amesema utaratibu huo ndio unaotumika katika miji mikubwa yote duniani ambako watu wanaotumia cash ni wachache sana.

Makonda amesema utaratibu huo utawezesha kudhibiti ulipaji wa kodi kwani utaratibu wa sasa wa kutumia EFD machines unatoa mwanya wa ukwepaji kodi.

Mkuu wa mkoa Makonda amesema hayo katika mkutano wake wa kazi na watendaji wote wa Halmashauri za jiji la Dsm pamoja na viongozi wa TRA mkoa wa Dsm.

Source: Estv habari

Maendeleo hayana vyama!
Sorry nadhani umesahau kuwa mfumo wetu wa masoko uko shagrabagara-Malawi ni nchi masikini ila kwa mfumo wa masoko-Kamuzu alijitahidi sana-hata kijijini unakuta branch ya peoples super market or chipiku store or chipuku plus-hapa kwetu makonda utasubiri sana
 
Tumtie moyo RC badala ya kumkatisha tamaa!
 
Halafu huyu school boy si kasoma MUCOBS, yaani pale kama angekuwa anahudhuria darasan tu angejua maana ya credit na debit cards achilia mbali kusomea masuala ya fedha.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tumtie moyo RC badala ya kumkatisha tamaa!
Hamna kumkatisha tamaa hapa,anafikilia impossibles-wewe utalipia mchicha au nyanya gengeni kwa kutumia debit card or credit card-huyo mama wa gengeni hiyo divice ya kusuport hiyo huduma ata ipata wapi? Je Makonda anajua ni alisimia ngapi ya wazazi wa Dar wana benki account?
 
Mawazo mazuri ila mazingira hayaruhusu kutekeleza hilo kwa sasa linahitaji muda wa kutosha.
 
Mkuu wa mkoa wa Dsm mh Makonda amesema ofisi yake itaandaa utaratibu ili wakazi wa jiji la Dsm wawe wanafanya manunuzi yao kwa kutumia credit cards badala ya fedha taslimu. Makonda amesema utaratibu huo ndio unaotumika katika miji mikubwa yote duniani ambako watu wanaotumia cash ni wachache sana.

Makonda amesema utaratibu huo utawezesha kudhibiti ulipaji wa kodi kwani utaratibu wa sasa wa kutumia EFD machines unatoa mwanya wa ukwepaji kodi.

Mkuu wa mkoa Makonda amesema hayo katika mkutano wake wa kazi na watendaji wote wa Halmashauri za jiji la Dsm pamoja na viongozi wa TRA mkoa wa Dsm.

Source: Estv habari

Maendeleo hayana vyama!
Duh aisee bongo itaachalini kuwa na mang'ombe??

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huyu hajakoma tuu kauli kama hizi tujiulize waziri wa fedha,kamishna wa TRA wanajisikiaje wanaposikia kauli hii inatoka kwa mtu asiyehusika kabisa na kodi?

Je, kesho watu wa Dar wakiacha kutumia EFD mashine kwa kauli ya RC itakuaje?

Suala la credit card siyo la serikali kuamua bali miundo mbinu yenyewe itajipeleka huko.

Bora angehimiza malipo kwa mobile money M-PESA, Airtel money na tiGO Pesa maana hivyo vipo kwa kila raia.
Indeed....malipo ya mobile money could work better kwenye mazingira yetu, hata nje ya Dar. Sio credit cards
 
Back
Top Bottom