RC Makonda kuanza kutoa msaada wa kisheria kwa wanawake waliotelekezwa na waume zao kuanzia leo tar 9 April

PAZIA 3

JF-Expert Member
Jan 30, 2018
1,078
1,870
Ingependeza zaidi zoezi hili lingekuwa la kitaifa,hata hivyo nampongeza RC wa Dar kwa kuandaa wanasheria kwa msaada wa kisheria!!
 
Nakuunga mkono maana kuna mijanaume Kazi yao ni kutelekeza wanawake. Unakuta wanateseka wote hali ikiwa nzuri mwanamke anatemwa.
 
Masuala ya ndoa ni magumu sana sijui kama atafanikiwa, alijaribu Mrema enzi hizo yeye alikuwa akiwapa wanaume siku 7 wajitokeze wayamalize ofisini lkn wengi walikuwa wakimwambia waende mahakamani, ambapo sheria ya ndoa bado inasema matunzo ya mtoto ni shilingi mia (100) kwa mwezi, mahakama zenyewe huwa zinaishia kuwashauri wakayamalize pembeni, refer kesi kati ya Diamond na Mobeto.

Katika suala hili la matunzo huwezi kujua mwenye makosa ni nani mwanaume au mwanamke, wakati anasuluhisha atambue kabisa kuna wanawake wajanja wanaobambikia watu watoto, kazaa na mhuni huko asiye na uwezo akaona ampelekee bwana wake wa pembeni mwenye uwezo.

Vile vile Makonda atambue kuwa hiki kinaweza kuwa chanzo cha kukomoana, kaachwa na bwana pengine kwa tabia zake chafu jamaa kaoa binti mwingine baada ya Makonda kujitokeza akaona ndiyo chansi ya kumkomoa au kujipatia kipato, ila si rule out kuwa kweli kuna wanaotelekeza watoto kwa pande zote lkn ni ngumu sana kusuluhisha jambo hili.
 
Makonda ana sifa zote za U - Sanguine.
Huanza safari mwishoni na kuimalizia mwanzoni.
 
Masuala ya ndoa ni magumu sana sijui kama atafanikiwa, alijaribu Mrema enzi hizo yeye alikuwa akiwapa wanaume siku 7 wajitokeze wayamalize ofisini lkn wengi walikuwa wakimwambia waende mahakamani, ambapo sheria ya ndoa bado inasema matunzo ya mtoto ni shilingi mia (100) kwa mwezi, mahakama zenyewe huwa zinaishia kuwashauri wakayamalize pembeni, refer kesi kati ya Diamond na Mobeto.

Katika suala hili la matunzo huwezi kujua mwenye makosa ni nani mwanaume au mwanamke, wakati anasuluhisha atambue kabisa kuna wanawake wajanja wanaobambikia watu watoto, kazaa na mhuni huko asiye na uwezo akaona ampelekee bwana wake wa pembeni mwenye uwezo.
Nakuunga mkono mia kwa mia
Wapo wanawake ambao ni vigeugeu leo anakwambia ile mimba ametoa baada ya muda kupita anaanza kudai matunzo ya mtoto utetezi wao ni kuwa mwanamke akiwa mjamzito kuna mambo anafanya bila kutegemea na ndo maana diamond alikiri kuwa pengine kosa halikuwa la baba yake......
 
Huyo jamaa ni kichaa na anatafuta CHEAP POPULARITY tu, hana lolote. Ningemuona ana akili kama angewaita kwanza hao wanaume wanaotuhumiwa kutelekeza hao wanawake, wakaongea pamoja, na labda jamaa ikionekana kweli kamtelekeza na anabisha, aendelee na anachotaka. What if tatizo likionekana ni la huyo mwanamke anayemtetea..??

Ni ngumu sn kuyapeleka mambo ya ndoa kimahakama. La sivyo mahakama zitajaa kesi za ndoa. Sheria ya ndoa na mambo ya ndoa ni magumu sn. Some wished they werent married at all, and others ask themselves why did they get married...!!
 
Elimu ya ndoa siyo 1 + 1 = 2!!!!!!!!!!!!!!
Bwana mkubwa wetu wa Dar, aka DSM Presida jitahidi kuelewa hilo kwanza wakati unaendelea na misaada mingine kwa mama hao. .
 
Nakuunga mkono mia kwa mia
Wapo wanawake ambao ni vigeugeu leo anakwambia ile mimba ametoa baada ya muda kupita anaanza kudai matunzo ya mtoto utetezi wao ni kuwa mwanamke akiwa mjamzito kuna mambo anafanya bila kutegemea na ndo maana diamond alikiri kuwa pengine kosa halikuwa la baba yake......
Ni ngumu sana binafsi nimeshakaa kwenye mabaraza ya usuluhishi, kuna wakati mnafikia hatua ya kumbembeleza mwanaume atoe matumizi, maana anaweza kusema ni kweli huyu ni mtoto wangu lakini sina uwezo na ukimuangalia kweli kachoka, mkisema afungwe hamtakuwa mmesolve chochote ndiyo mtazidisha mateso kwa mtoto, mke na sasa mwanaume naye yuko gerezani.
 
Huyo jamaa ni kichaa na anatafuta CHEAP POPULARITY tu, hana lolote. Ningemuona ana akili kama angewaita kwanza hao wanaume wanaotuhumiwa kutelekeza hao wanawake, wakaongea pamoja, na labda jamaa ikionekana kweli kamtelekeza na anabisha, aendelee na anachotaka. What if tatizo likionekana ni la huyo mwanamke anayemtetea..??

Ni ngumu sn kuyapeleka mambo ya ndoa kimahakama. La sivyo mahakama zitajaa kesi za ndoa. Sheria ya ndoa na mambo ya ndoa ni magumu sn. Some wished they werent married at all, and others ask themselves why did they get married...!!
Si aliwaambia wawatafute wanawake wao au ulitaka atumie njia gani kuwaita? Hapa watapatikana na kabla ya kufika mahakamani hilo litachukuliwa hatua kwanza
 
Ingependeza zaidi zoezi hili lingekuwa la kitaifa,hata hivyo nampongeza RC wa Dar kwa kuandaa wanasheria kwa msaada wa kisheria!!
Mwanamke aliyezaa na wanaune watatu tofauti atamshtaki yupi? Hapo ndo umalaya unapowekwa wazi
 
Usitumie neno msaada wa kisheria kama hujui wa2 wanoruhusiwa kutoa msaada was kisheria mwisho was Siku no anapoteza muda
 
Back
Top Bottom