RC Makonda awajibu wabunge, adai wanaosema amevunja sheria wana watoto nje

Majina ya madawa ya kulevya kelele zilipigwa vivyo hivyo....
Tukawaona,na tukawajua kwa Majina leo mateja Dar unawatafuta.....

Songa mbele baba
Unaishi Dar es salaam ya wapi ndugu?! Au mpita njia?!

Hivi kabisa unaamini Dar es salaam hakuna drug dealers?!

Unaweza kunitajia ni drug dealer yupi alikutwa na mihadarati miongoni mwa wale aliokuwa amewataja?!
Au Wema Sepetu na TID?!
 
Inasikitisha sana Mkuu kuona huyo mfojaji wa vyeti ambaye hana sifa ya kushika nafasi yoyote ndani ya Serikali kutokana na kuhusika na forgery anaogopwa na Mawaziri kiasi hiki kwa sababu tu ya kulindwa na kubwa la majizi

Hahaa!!

Tena nadhani ukiwapa option ama ya ku-mess up na Bashite au na Jesca; nadhani wengi wataona bora wazinguane na Jesca kuliko Bashite!!
 
Wewe uchi sana. Kitoe! Hata haibu huna.
What do you mean when you say; "but the way it's carried out it's completely unacceptable!!"

Unazijua sheria wewe? Makonda ni mtumishi wa serikali na amejipanga vizuri. Sio mkurupukaji kama wewe. Katie mbali huko. Unapiga kelele hata hujui unacho ongea. Kujiganya unajua kama Prof. Kabudi. Hakuna lolote!

You are mad! Na sio Makonda.
Kwanza uelewe unaongelea kuhusu RC Makonda kama nani wewe? RC Makonda ni serikali mkuu. Serikali lazima itimize wajibu wake. Hello amka! Tuko katika awamu nyingine ya utawala. Hatuko katika awamu ya Kikwete.
We dada vipi, mbona matusi?! Una frustration za kutelekezwa na mumeo na hivyo kuona mwokozi wako ndo Makonda; au?!

Povu kamtolee mumeo, JF unatakiwa kujibu hoja!

Usipende shari na wanaume wakati hailekei kama shari zenyewe unaziweza!!!
 
Prof Kabudi ana mtoto nje?
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amesema wale wote wanaosema kampeni yake ya kuwasaidia akina mama waliotelekezwa na watoto imevunja sheria, pengine wana watoto nje na wanaogopa kujitokeza.

Makonda ameyasema hayo leo Aprili 19, katika uzinduzi wa hospitali ya kisasa ya mama na mtoto iliyopo Chanika iliyojengwa kwa msaada wa Shirika Maendeleo la Kimataida la Korea (Koica).

“Eti wanasema navunja sheria, natakiwa nifanye faragha kama unataka faragha tunza mtoto. Mimi siogopi, nipo tayari kufungwa lakini kwa ajili wa kutetea haki za watoto. Pengine hao wanaosema navunja sheria wana watoto wao nje wanaogopa kujitokeza,” amesema.

Jana, Waziri wa Sheria na Katiba, Profesa Palamagamba Kabudi akiwa bungeni alisema kampeni hiyo inaweza kuleta hali ya sintofahamu na akabainisha kuwa inapaswa kufanyika faragha na sio kama inavyofanyika sasa.

Awali, Waziri wa Afya, Jinsia, Wanawake na Watoto, Ummy Mwalimu alisema kampeni hiyo ni sahihi ila kasoro yake ni kutokuwa na faragha, lakini akasema kwa sasa inafanyika huku picha za watoto zikifichwa.

Aliyeibua hilo bungeni jana alikuwa ni mbunge wa Ulanga, Goodluck Mlinga aliyehoji uhalali wa kampeni hiyo na akahoji kama haivunji sheria na kuwavunjia haki wanawake na watoto.

CHANZO: Mwananchi

Pia tembelea

Naibu Waziri wa Afya, Dk. Faustine Ndugulile akemea udhalilishaji watoto zoezi la RC Makonda

Msukuma: Kampeni ya Makonda ni ishara ya kukosa kazi ya kufanya

Prof. Kabudi: Makonda kavunja sheria na faragha za watu kuwaita wanawake na watoto. Ilitakiwa kuwa siri sio alivyofanya
 
Inasikitisha sana Mkuu kuona huyo mfojaji wa vyeti ambaye hana sifa ya kushika nafasi yoyote ndani ya Serikali kutokana na kuhusika na forgery anaogopwa na Mawaziri kiasi hiki kwa sababu tu ya kulindwa na kubwa la majizi
Sipati picha mawaziri wangekuwa wanakaa darasani kama shuleni!

Selemani Jafo katoka kwenye kiti chake na kwenda kupiga story na Majaliwa!

Mwakyembe nae kaenda kwa Kabudi!!

Ummy Mwalimu anaanza kumpigisha umbeya Ndalichako!

Dk Mpango anaenda kupata mawili matatu kwa Mbarawa!

Kaijage katoka nje kugonga fegi mara kwa mbaaaali anaona gari ya Bashite inakuja!

Yaani kama namuona vile Kaijage anavyotoka nduki kurudi ndani huku akipiga kelele "ndugu zanguni, anakuja! Anakuja!"

Yaani kama nawaona vile akina Ummy wanavyokimbizana kurudi kwenye viti vyao na kuanza kuzuga wanasoma ilani ya CCM huku wengine wakificha Ripoti ya CAG ili asiwadhanie walikuwa wanasoma section ya trillion 1.5!

Kila nikifumba namuona Prof Kabudi jicho limemtoka zaidi na yeye akihangaika kuificha katiba aliyokuwa anasoma ili asidhaniwe alikuwa anapekua pekua kutafuta ibara aliyoivunja Dad's beloved son!!
 
We dada vipi, mbona matusi?! Una frustration za kutelekezwa na mumeo na hivyo kuona mwokozi wako ndo Makonda; au?!

Povu kamtolee mumeo, JF unatakiwa kujibu hoja!

Usipende shari na wanaume wakati hailekei kama shari zenyewe unaziweza!!!
Wesenghe kama hawa ni kuachana nao asikupotezee muda maana hao wanaowategemea wana muda mfupi tu
 
BASHITE hana anachokijua kwa sasa yupo tu hajui lolote asubiri muda mfupi tu atayakumbuka yote ya nyuma. Namsihi aendeleee kutumia hao anaowajua au wasiojulikana lakini muda ndiye muamuzi kama pambano la mpira
 
Hahahahaha lol! Anakuja anakuja nani Bashite!!Kabudi katoa jicho analizungusha kama saa. :):)

Sipati picha mawaziri wangekuwa wanakaa darasani kama shuleni!

Selemani Jafo katoka kwenye kiti chake na kwenda kupiga story na Majaliwa!

Mwakyembe nae kaenda kwa Kabudi!!

Ummy Mwalimu anaanza kumpigisha umbeya Ndalichako!

Dk Mpango anaenda kupata mawili matatu kwa Mbarawa!

Kaijage katoka nje kugonga fegi mara kwa mbaaaali anaona gari ya Bashite inakuja!

Yaani kama namuona vile Kaijage anavyotoka nduki kurudi ndani huku akipiga kelele "ndugu zanguni, anakuja! Anakuja!"

Yaani kama nawaona vile akina Ummy wanavyokimbizana kurudi kwenye viti vyao na kuanza kuzuga wanasoma ilani ya CCM huku wengine wakificha Ripoti ya CAG ili asiwadhanie walikuwa wanasoma section ya trillion 1.5!

Kila nikifumba namuona Prof Kabudi jicho limemtoka zaidi na yeye akihangaika kuificha katiba aliyokuwa anasoma ili asidhaniwe alikuwa anapekua pekua kutafuta ibara aliyoivunja Dad's beloved son!!
 
What's going on between the two?! Kiburi cha huyu mheshimiwa kinatoka wapi!! Kiburi kinachompa hadi ujasiri wa kuwadhihaki watu kama akina Prof Kabudi!

Inasemekana na wengi wenye ufahamu wa mambo haya kuwa Makonda alimpeleka Magufuli kwa waganga wa kienyeji kumfanyia dawa za kinga ndio maana hamuheshimu; kama ni kweli basi usalama wa Taifa hawajui kazi yao na kuna umuhimu wa kuifumua taasisi hiyo!! Makonda asiruhusiwe kuonana na Rais kama vile anakwenda chooni kwani anaidhalilisha taasisi ya URAIS na ni hatari kwa usalama wa nchi!!
 
Taarifa niliyonayo muda mrefu Magu hajitambui kwa kuwa alishapigwa zongo na BASHITE yaani aliamua kummaliza kwanza kbla ya kufanya anachokijua yy na wengi wanasema ni naibu rais lakini bashite ndiye rais wa Tanzania
 
TUMZOMEE: "Profesa Kabudi huyoooooooo... kumbe umekimbia mtoto kwa m7chepuko!"

Sarcasm pembeni.

Ukweli ni kwamba Paul Makonda keshaota mapembe ya chuma na yamekomaa!

Sijui ikiwa huwa anajiuliza kabla ya kuwashushia vitofa wenzake...!!

For the first time nilikuwa shocked na jeuri ya Makonda
pale alipomfanyia rebellious hadi Mkulu mwenyewe! Ni pale Mkulu alipotamka hadharani kuwataka Ruge na Makonda wamalize tofauti zao!

Few hours later, tena wakiwa mbele za media; Makonda akaonesha wazi wazi kutokuwa tayari kumaliza tofauti zao na Ruge!!

I was shocked!! Na hadi kesho, bado Ruge na Makonda hawajamaliza tofauti zao!

Binafsi sioni tafsiri nyingine katika hili zaidi ya kwamba Makonda alimvimbia hadi bosi wake!! Na bosi ameufyata!

What's going on between the two?! Kiburi cha huyu mheshimiwa kinatoka wapi!! Kiburi kinachompa hadi ujasiri wa kuwadhihaki watu kama akina Prof Kabudi!!

I've strong feelings kwamba, hata PM hana kauli mbele ya Makonda!
Itakuwa waganga wa kienyeji
 
Naibu kasema,wakiendelea uwaziri wanaukosa na hao wabunge wajiangalie sana
 
Vipi amezungumzia juu ya kuwa tayari kupokea mtoto wa kichina mwenye asili ya kitanzania kwenye familia yake?! Na yupo tayari kuishi nae kama mtoto wake kumbe ni mtoto wa HYBRID!
 
Kumbe ndo maana "malaika mkuu" hasemi chochote anaogopa kuumbuliwa na Makonda kuhusu kichanga chake cha (waziri)!!?
 
Inasemekana na wengi wenye ufahamu wa mambo haya kuwa Makonda alimpeleka Magufuli kwa waganga wa kienyeji kumfanyia dawa za kinga ndio maana hamuheshimu; kama ni kweli basi usalama wa Taifa hawajui kazi yao na kuna umuhimu wa kuifumua taasisi hiyo!! Makonda asiruhusiwe kuonana na Rais kama vile anakwenda chooni kwani anaidhalilisha taasisi ya URAIS na ni hatari kwa usalama wa nchi!!
With reference to issue ya Makonda na Ruge; hakuna shaka hata kidogo kwamba jamaa hamheshimu Magu!

Yaani Rais wa nchi, ambae pia amekuteua anakuagiza hadharani kwamba maliza tofauti zenu na fulani but few hours later unaonesha hadharani kwamba haukubaliani na agizo ulilopewa... ulilopewa na bosi; bosi ambae ndie Rais wa nchi na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama!

Aisee... hata Mama Jesca sidhani kama ana ubavu wa kuonesha jeuri kama hiyo... I doubt!
 
Back
Top Bottom