Tuwasaidie watoto wanapopata athari za kisaikolojia pale wanapotendewa ukatili

Nyendo

JF-Expert Member
Jun 4, 2017
1,194
4,112
Watoto ni kundi ambalo haliwezi kujitetea pale linapokutana na ukatili wa aina yoyote, mara nyingi hadi watu wazima wagundue unakuta mtoto kashapa madhara aidha ya kimwili au kisaikolojia.

Ni muhimu kutambua kumsaidia mtoto aliyefanyiwa ukatili kisaikolojia ni mchakato unaohitaji tahadhari na umakini. Baadhi ya hatua unazoweza kuchukua kumsaidia mtoto huyo aliyefanyiwa ukatili na kuathirika kisaikolojia.

Tafuta sehemu salama kwa mtoto: Kama mtoto anafanyiwa ukatili wa kupigwa au aina nyingine ya ukati anakuwa anahofu na watu aliokuwa akiishi nao hata kama akiambiwa hawatarudia yeye atajua wamempa muda ila watarudia ivyo hofu hiyo itaendelea kuharibu saikolojia yake ivyo inabidi aondolewe kwa watu au mtu huyo na kuwekwa sehemu atakayokuwa na amani nayo.

Hakikisha kwamba mtoto huyo yuko salama na anaondolewa katika mazingira hatari kwa wakati. Ikiwa anahitaji ulinzi, wasiliana na mamlaka husika, kama vile polisi au huduma za ustawi wa jamii.

Muoneshe upendo na kumjali: Mpe mtoto uhakika kwamba unampenda na unamjali, lakini onesha umechukizwa na kitendo alichokuwa akifanyiwa na kama kitahitaji kuchukua hatua za kisheria basi awe na uhakika kuwa wahuika watafikishwa mbele ya sheria.

Wasiliana naye kwa upole na kama mhusika ni mtu wake wa karibu kama mzazi au wazazi mpe uhakika kuwa bado anathamani na atakuwa salama nje ya hao wazazi au walezi kwa kuwa umechukua jukumu la kuhakikisha yuko salama na anaishi vyema. Epuka kumlaumu au kumshutumu kwa yale aliyopitia mfano, ametendewa ukatili wa kupigwa na kudhuru mwili ukaanza kumlaumu kiburi chako ndio kimesababisha upigwe au wizi wako umesababisha upigwe, subiri mpaka atakapokuwa awa kisha utamuonya juu ya mienendo yake mibaya.

Mpe nafasi ya kumsikiliza: Mpe mtoto fursa au nafasi ya kuzungumza juu ya uzoefu wake na hisia zake. Sikiliza kwa makini na bila kumkatiza. Mfanye ajisikie kuwa yuko huru na salama na anaweza kueleza hisia zake bila woga na sehemu anayohitaji majibu mpatie majibu anapohitaji kutiwa moyo fanya ivyo na anapohitaji kupongezwa mpongeze.

Heshimu faragha:
Hakikisha mazungumzo na habari zinazohusiana na mtoto huyo zinabaki kuwa faragha. Usimpe mtu yeyote habari zake bila idhini yake, isipokuwa kama sheria inavyotaka, kwani pengine taarifa zake zinaweza tumika kama sehemu ya kumdhaliliha ivyo zibaki kuwa siri ili aone kastiriwa, mfano kabakwa kumtangaza itakuwa njia ya kumuumiza kisaikolojia kwani huenda watoto wenzake wakasikia na kumtania.

Mtafutie wataalamu wa saikolojia wampe msaada: Tafuta msaada kutoka kwa wataalamu wenye ujuzi kama vile wataalamu wa saikolojia, wafanyakazi wa huduma za ustawi wa jamii, au wataalamu wa afya ya akili. Wao wanaweza kutoa ushauri na msaada unaohitajika kwa mtoto na familia yake.

Mjengee msaada wa kijamii:
Hakikisha mtoto anapata msaada wa kijamii unaohitajika. Unaweza kujenga mtandao wa watu wanaomjali, kama familia, marafiki, au walimu, ambao wanaweza kutoa msaada na upendo.

Tumia njia za kuponya: Kuna njia nyingi za kuponya kisaikolojia ambazo zinaweza kusaidia mtoto kama vile ushauri wa kisaikolojia, michezo ya aina mbalimbali, au matumizi ya sanaa kama njia ya kueleza hisia. Wasiliana na wataalamu wa saikolojia ili kupata maelekezo sahihi juu ya njia bora za kuponya kwa mtoto.

Tafuta taarifa zaidi juu ya athari za kisaikolojia kwa mtoto aliyefanyiwa ukatili, fanya utafiti na uelewe athari za kisaikolojia zinazoweza kujitokeza baada ya mtoto kupitia ukatili. Hii itakusaidia kuwa na uelewa bora na kuwa na uwezo wa kumsaidia kwa njia inayofaa.

Zinagatia:
Athari za watoto kuathirika kisaikolojia ni kubwa na huwa ziweza kumuathiri mtoto hata akiwa mtu mzima na pengine akabeba chuki na kuilipiza ukubwani kwa wasiohusika, inabidi kuyatibu matatizo hayo ili kumuepusha mtoto na atahri za mbeleni na za kimakuzi.
 
Back
Top Bottom