RC Makonda: Ambaye hatakuwa na kadi ya bima, hataweza kupata huduma ya afya katika hospitali

Ghazwat

JF-Expert Member
Oct 4, 2015
23,718
66,262
8ab8834c1af1915f3f92e5e832d839db.jpg

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda amesema Serikali itaandaa mpango wa matibabu kwa kutumia kadi ya bima ya afya, kwa wakazi wa Dar, katika Hospitali zote za umma, Mwananchi ambaye hatakuwa na kadi ya bima, hataweza kupata huduma ya afya katika Hospitali za umma popote Dar es salaam.

Chanzo: Mwananchi
 
Mmh basi ndo maana maduka ya dawa yanageuka dispensary hadi kulaza wagonjwa sababu hizi hizi.

Hizo nguvu wangeweka kwenye kuboresha kwanza maslah ya manesi na madokta,kuhakikisha vifaa vya hospital vipo vya kutosha na huduma bora ndo waanze wabana wananchi kihivyo

Hii nchi bana mkuu wa mkoa anaingilia majukumu ya waziri wa afya
 
Hii haijakaa sawa. Mtu kaja Dar, kwa mipango fulani halafu anaugua sasa inakuwaje asipate huduma?
 
8ab8834c1af1915f3f92e5e832d839db.jpg
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda amesema Serikali itaandaa mpango wa matibabu kwa kutumia kadi ya bima ya afya, kwa wakazi wa Dar, katika Hospitali zote za umma, Mwananchi ambaye hatakuwa na kadi ya bima, hataweza kupata huduma ya afya katika Hospitali za umma popote Dar es salaam.

Chanzo: Mwananchi

Ile miti aliyoipanda hapo dar iliishia wapi??

So hata wasio wakazi wa Dar wakienda dar wakiumwa hawatatibiwa

Sometimes shule huwa inasaidia mtu kujitambua
 
Ahaaa! Umeona eeh! Kukurupuka mbele kwa mbele kila kona. Ndiyo sababu huwa tunasema nchi hainyooshwi bali inavurugwa!!! Wakazi wa Dar chungu nzima hawana kadi za bima na wala hawana uwezo wa kuwa nazo. Kwa hiyo hawa wataachwa wajifie tu!!!

Mmh basi ndo maana maduka ya dawa yanageuka dispensary hadi kulaza wagonjwa sababu hizi hizi.

Hizo nguvu wangeweka kwenye kuboresha kwanza maslah ya manesi na madokta,kuhakikisha vifaa vya hospital vipo vya kutosha na huduma bora ndo waanze wabana wananchi kihivyo

Hii nchi bana mkuu wa mkoa anaingilia majukumu ya waziri wa afya
 
viongozi wetu hawana plan, wanafanya maamuzi kama wanapiga chafya. wanakurupuka tu. hizo kadi za ima wanatoa bure au? stupid!!!
 
Back
Top Bottom