Swali: NHIF Inasajili Vipi Watoto wa Shule za Serikali kwa Bima ya Toto Afya Kadi?

Jumanne Mwita

JF-Expert Member
Nov 18, 2014
497
1,269
Ningependa kujua kuhusu utaratibu wa NHIF kusajili watoto wa shule za serikali kwa Bima ya Toto Afya Kadi. Awali, NHIF ilikuwa inasajili watoto ambao hata siyo wanafunzi kwa bei ile ya Tsh 50,400 bila kujali anasoma au hasomi baada ya shirika lenyewe kujipa hasara kwa kuhujumu mfuko ndio wakaja na hii sera ya vifurushi kunusuru shirika.

Je, NHIF inasajili watoto wa shule za serikali kwa Bima ya Toto Afya Kadi kama ilivyo kwa shule za private ambazo zinabigiwa debe sana, au huduma hii sasa inapatikana tu kwa shule za binafsi?

Sijapata kuona hamasa yoyote kutoka NHIF kuhusu usajili wa watoto wa shule za serikali, na nilipojaribu kuulizia katika shule za serikali, inaonekana hawafahamu chochote kuhusu utaratibu huu. Lakini shule za binafsi zinaonekana kufahamu na kutumia huduma hii.

Je, hii inamaanisha kuwa NHIF imeamua kuwabagua watoto wa familia zisizo na uwezo kwa kutoleta huduma hii mashuleni kwao? Tafadhali nisaidieni kuelewa:

1. Je, utaratibu wa kusajili watoto wa shule za serikali kwa Bima ya Toto Afya Kadi ukoje?
2. Kwanini shule za serikali hazihamasishwi au kufahamishwa kuhusu huduma hii kama ilivyo kwa shule za binafsi?
3. Kuna njia yoyote ya kuhakikisha watoto wa shule za serikali wanapata huduma hii ya bima?

Nawashukuru kwa msaada wenu na ninategemea maoni yenu yenye msaada katika kuelewa suala hili.

Asanteni,
 
Vitu vingine tuache lawama za bure,
Mlishaambiwa na NHIF, watoto wanajiunga NHIF kupitia shule, hizo shule za serikali ziende NHIF zichukue control number, zichangishe michango kwa wanafunzi wake, kisha wapewe kadi,

Issue ni moja, wazaz wa gvt schools wanalalamika buku ya msosi wa wanafunzi wao, je wakiambiwa 50400/- si wataona wanafukuzwa shule? Hivyo hakuna mwalimu mwenye muda wa kukimbizana na wazazi kuwadai hio michango, labda wazazi mjiorganize wenyewe
 
Mkuu sio rahisi kama unavyofikiri. Wameambiwa mpaka watimie idadi ya wanafunzi 100 ndipo watapata kulipa. Mimi nina watoto 2 wanasoma shule za private na 1 shule ya serikali hizi zenye mitaala ya kiingereza. Hizo shule zote zimeshindwa kufanikisha idadi ya wanafunzi 100 toka mwaka jana. Watoto wengine wako chini ya bima za wazazi wao wanaofanya kazi sekta rasmi.
Mwalimu mkuu wa hiyo shule nyingine hadi kaenda ofisini akiomba walio tayari alete majina walipe, akaambiwa wao wanapokea idadi ya wanafunzi 100 kama vipi afungue akaunti ya bank wazazi waweke pesa humo mpaka wakitimia 100. Mwalimu mkuu akaona isiwe shida asije kula ela ya wazazi akairudisha.
Yani ni kama imefutwa kiaina. Mimi niko tayari kulipa sasa kwanini nisubiri mwenzangu ambaye hayuko tayari.
 
Ni kweli tupu mkuu. Wazazi wa shule za serikali wamezoea kila kitu bure.

Kuna walati mwanangu alikuwa anasoma huko tukaombwa na walimu kwenye kikao tuchangie 50 za tour ya watoto.

Kwa nililiyo yaona kwa wazazi wale ni upumbavu wa kulialia. Siku hiyo nilimhamisha mwanangu private
 
Mkuu sio rahisi kama unavyofikiri. Wameambiwa mpaja watimie idadi ya wanafunzi 100 ndipo watapata kulipa. Mimi nina watoto 2 wanasoma shule za private na 1 shule ya serikali hizi zenye mitaala ya kiingereza. Hizo shile zote zimeshindwa kufukisha idadi ya wanafunzi 100 toka mwaka jana. Watoto wengine wako chini ya bima za wazazi wao wanaofanya kazi sekta rasmi.
Mwalimu mkuu wa hiyo shule nyingine hadi kaensa ofisini akiomba walio tayari alete majina walipe, akaambiwa wao wanapokea idadi ya wanafunzi 100 kama vipi afungue akaunti ya bank wazazi waeeke pesa humo mpaka wakitimia 100. Mwalimu mkuu akaona isiwe shuda asije kula ela ya wazazi akairudisha.
Yani ni kama imefutwa kiaina. Mimi niko tayari kulipa sasa kwanini nisubiri mwenzangu ambaye hayuko tayari.
Nimejua leo aisee hii ni hatari kwa afya, aisee serikali haina huruma na wananchi 🥲
 
Vitu vingine tuache lawama za bure,
Mlishaambiwa na NHIF, watoto wanajiunga NHIF kupitia shule, hizo shule za serikali ziende NHIF zichukue control number, zichangishe michango kwa wanafunzi wake, kisha wapewe kadi,

Issue ni moja, wazaz wa gvt schools wanalalamika buku ya msosi wa wanafunzi wao, je wakiambiwa 50400/- si wataona wanafukuzwa shule? Hivyo hakuna mwalimu mwenye muda wa kukimbizana na wazazi kuwadai hio michango, labda wazazi mjiorganize wenyewe
Hatukatai Shule za government zilivyo shida ni kuwa mzazi akihitaji kumkatia bima mtoto wake isiwe kigezo cha kusema mpaka mtimie 100 ndio mpate bima hii siyo sawa kama mchangiaji mmoja amesema hapo ni kama wameiondoa kimtindo hii bima
 
Ni kweli tupu mkuu. Wazazi wa shule za serikali wamezoea kila kitu bure.

Kuna walati mwanangu alikuwa anasoma huko tukaombwa na walimu kwenye kikao tuchangie 50 za tour ya watoto.

Kwa nililiyo yaona kwa wazazi wale ni upumbavu wa kulialia. Siku hiyo nilimhamisha mwanangu private
Aisee
 
Ningependa kujua kuhusu utaratibu wa NHIF kusajili watoto wa shule za serikali kwa Bima ya Toto Afya Kadi. Awali, NHIF ilikuwa inasajili watoto ambao hata siyo wanafunzi kwa bei ile ya Tsh 50,400 bila kujali anasoma au hasomi baada ya shirika lenyewe kujipa hasara kwa kuhujumu mfuko ndio wakaja na hii sera ya vifurushi kunusuru shirika.

Je, NHIF inasajili watoto wa shule za serikali kwa Bima ya Toto Afya Kadi kama ilivyo kwa shule za private ambazo zinabigiwa debe sana, au huduma hii sasa inapatikana tu kwa shule za binafsi?

Sijapata kuona hamasa yoyote kutoka NHIF kuhusu usajili wa watoto wa shule za serikali, na nilipojaribu kuulizia katika shule za serikali, inaonekana hawafahamu chochote kuhusu utaratibu huu. Lakini shule za binafsi zinaonekana kufahamu na kutumia huduma hii.

Je, hii inamaanisha kuwa NHIF imeamua kuwabagua watoto wa familia zisizo na uwezo kwa kutoleta huduma hii mashuleni kwao? Tafadhali nisaidieni kuelewa:

1. Je, utaratibu wa kusajili watoto wa shule za serikali kwa Bima ya Toto Afya Kadi ukoje?
2. Kwanini shule za serikali hazihamasishwi au kufahamishwa kuhusu huduma hii kama ilivyo kwa shule za binafsi?
3. Kuna njia yoyote ya kuhakikisha watoto wa shule za serikali wanapata huduma hii ya bima?

Nawashukuru kwa msaada wenu na ninategemea maoni yenu yenye msaada katika kuelewa suala hili.

Asanteni,
Shule za serikali Kuna shida kwenye ufuatiliaji wa mambo ya msingi wao wapo bize kuhamasisha pesa za chakula,mitihani na masomo ya ziada.
Binti yangu anasoma kidato cha kwanza shule binafsi (bweni) Jana karudi nyumbani kwa ajili ya likizo na bima yake mkononi!
Uongozi wa shule ulitushirikisha sisi wazazi/walezi tukalipa kiasi kinachostahili watoto wakapata bima zao!
 
Kama Taifa bado tupo nyuma sana n mambo ya msingi kama haya
 
Mkuu sio rahisi kama unavyofikiri. Wameambiwa mpaka watimie idadi ya wanafunzi 100 ndipo watapata kulipa. Mimi nina watoto 2 wanasoma shule za private na 1 shule ya serikali hizi zenye mitaala ya kiingereza. Hizo shule zote zimeshindwa kufanikisha idadi ya wanafunzi 100 toka mwaka jana. Watoto wengine wako chini ya bima za wazazi wao wanaofanya kazi sekta rasmi.
Mwalimu mkuu wa hiyo shule nyingine hadi kaenda ofisini akiomba walio tayari alete majina walipe, akaambiwa wao wanapokea idadi ya wanafunzi 100 kama vipi afungue akaunti ya bank wazazi waweke pesa humo mpaka wakitimia 100. Mwalimu mkuu akaona isiwe shida asije kula ela ya wazazi akairudisha.
Yani ni kama imefutwa kiaina. Mimi niko tayari kulipa sasa kwanini nisubiri mwenzangu ambaye hayuko tayari.
Muhimizane, au muombe muungane shule mbili
 
Hatukatai Shule za government zilivyo shida ni kuwa mzazi akihitaji kumkatia bima mtoto wake isiwe kigezo cha kusema mpaka mtimie 100 ndio mpate bima hii siyo sawa kama mchangiaji mmoja amesema hapo ni kama wameiondoa kimtindo hii bima
Hio bima imeondolewa kwa mtu mmoja mmoja kwa sababu hio hio,
Wanataka kupata wachangiaj wengi ili mfuko uwe makin
 
Shule za serikali Kuna shida kwenye ufuatiliaji wa mambo ya msingi wao wapo bize kuhamasisha pesa za chakula,mitihani na masomo ya ziada.
Binti yangu anasoma kidato cha kwanza shule binafsi (bweni) Jana karudi nyumbani kwa ajili ya likizo na bima yake mkononi!
Uongozi wa shule ulitushirikisha sisi wazazi/walezi tukalipa kiasi kinachostahili watoto wakapata bima zao!
Upo sahihi kwa pvt,
Mzee gvt wazazi wanarusha ngumu kisa buku ya msosi, leo uanze kuwaambia 50 ya bima? Na ujue waTz wenyewe hawana imani kubwa na bima, unataka mwalimu aanze kupata stress ya kuchangisha hio pesa ?
 
Inabidi wazazi wa shule za serikali wapewe elimu kuhusu bima ya afya na wahamasishwe kuchangia huduma hiyo .
Wenyewe watafanya kazi yao shida inakuja kwa hawa watoaji ndio kipengele, me nafikiri hii huduma isiwe mpaka uwe na watoto 100 mdio muwaunganishe kwenye Bima hapo napinga, iwe kama mzazi anaona umhimu wa bima kwa mtoto wake amkatie bima siyo kimakundi hivyo ibaki kama zamani.

Kwanza watapata idadi kubwa sana ya wachangiaji maana familia iko radhi iuze hata mpunga ili ikate bima kwa watoto wao wakubwa Wenyewe huwa hawajijali sana kama wanavyowajali watoto wao.
 
Back
Top Bottom