RC Makalla aiagiza NHC kufanya kazi usiku na mchana kukamilisha machinjio ya Vingunguti

Suley2019

JF-Expert Member
Oct 7, 2019
1,817
4,566
MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Amos Makalla ameliagiza Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) kufanya kazi usiku na mchana ili hadi kufikia Agosti 1, 2021 machinjio ya kisasa ya Vingunguti ianze kutumika.

1625816990935.png


Makalla ametoa agizo hilo jana Julai 8, 2021 wakati alipotembelea machinjio hayo na kukuta bado hayajaanza kutumika huku Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam, Jumanne Shauri akisema ujenzi wake umekamilika kwa asilimia 96.

Ujenzi huo ulio chini ya Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) na Mshauri Mwelekezi M/Scons Africa Limited na FB Consultant ulipaswa kukamilika Desemba 31, 2019.

Baada ya ukaguzi, Makalla amesema, “Tumeambizana mchana kweupe sasa hiyo Agosti 1,2021 kazi ianze na mimi nitakuwepo hapa nikiangalia namna mnavyofanya hiyo kazi rasmi. Naomba iwe hivyo, sasa kazi zilizobaki zifanywe usiku na mchana.”
 
Ila huyu jamaa anapiga kazi buana, kinachonifariji ni jinsi anavyohamisha machinga bila virungu wala fujo.
 
Back
Top Bottom