#COVID19 RC Kigoma: Mkoa una wagonjwa 12 wa Wimbi la tatu la ugonjwa wa COVID-19

Cannabis

JF-Expert Member
Jan 20, 2014
8,966
25,353
images (87).jpeg

Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Thobias Andengenye athibitisha mkoa wake kuwa na wagonjwa 12 wa CoVID-19, RC Andengenye amesema kuwa miongoni mwao 6 wanatibiwa hospitalini na wengine wamejitenga nyumbani.

====

Mkoa wa Kigoma umeripotiwa kuwa na wagonjwa 12 wa Corona ambapo wengine wamejitenga majumbani na wengine wanaendelea kupatiwa matibabu katika vituo vilivyoandaliwa maalumu kwa ajili ya kulazwa wenye Corona.

Akisoma taarifa ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo mbele ya Kamati ya CCM, RC wa Kigoma, Thobias Andengeye amesema kanuni na taratibu za kiafya zinaendelea kufuatwa na kutoa tahadhari kwa wakazi wa Mkoa huo.

“Tuna wagonjwa 12 ambapo 6 wamelazwa na 6 wapo Majumbani wamejitenga na wanaendelea vizuri na matibabu,” amesema RC Andengeye.
 
Kutangaza hiyo idadi kunasaidia Nini? Hata angesema wagonjwa wapo inatosha, maana tulishaambiwa tuzoe tu kuishi nayo kama Malaria ambavyo tunaishi nayo, na inaua wengi zaidi kuliko mafua ya wazungu.

Kwa vile unalinda kibarau ungetangaza wengi zaidi I'li umfurahishe aliyekuteua.

Sasa hivyi Kila mkuu wa mkoa atajitahidi kutangaza Visa hata Kama wagonjwa hawapo I'li kulinda kibarua.

Na kwenye taarifa ya habari hakikisheni habari zenu ziwe za kuanziwa I'li mkuu afurahi.

Kazaneni ila mjue Kila kitu kina mwisho.

Hukumu ya Mungu hamtaikwepa kwa kile kimejificha mnachokitafuta.
 
Sasa siku zote walikuwa wanaficha nini yani hadi watangaziwe pesa ndio watoe takwimu wakati ugonjwa kweli upo zaidi ya mwaka sasa na watu wanakufa.

Toka ugonjwa uanze mapema mwaka jana Kenya wameshapokea zaidi ya dola bilioni 5, Uganda dola bilioni 1.5 na Rwanda dola 240 milioni.

Tanzania kiburi cha marehemu Magufuli cha ubabe wa kijinga wa kuficha uhalisia wa huu ugonjwa haijapata chochote cha maana.

Hizi fedha mkisha kopeshwa mnazitumia kwa matumizi mbalimbali yanayolenga kuwanufaisha wananchi wenu na sio lazima zilenge ugonjwa wenyewe moja kwa moja na mataifa yote yaliyo kopeshwa yamefanya hivyo.

Mnaweza mkanunua dawa mkajaza kwenye mahospitali na vifaa mkanunua, mkaboresha mashule, barabara sambamba na huduma ya maji, sasa kwa hii sera ya Magufuli ya kuficha ukweli, tumepoteza pakubwa mno.
 
Toka ugonjwa uanze mapema mwaka jana Kenya wameshapokea zaidi ya dola bilioni 5, Uganda dola bilioni 1.5 na Rwanda dola 240 milioni.
Kuhusu hizo pesa za mkopo pointi yako ni ipi.? Kama zingekuwa za bure bc ndugu mwendazake angekuwa amekosea
 
Corona bado sana Tz, labla tuone watu wakifa barabarani ndo tutakuwa serious. Sir God naomba usitunyooshe 🙏🙏🙏
Na haiwezi kufikia hatua hiyo!!ni kweli covid 19, ipo lakini kwa sasa wameshaanza kupika data ili kupata pesa za kufanyia mambo mengine, lakini kwa wananchi wengi ni kama hawana habari nayo, kwani wameishi nayo mwaka na zaidi sasa na maisha yanasonga mbele, hivyo basi hakuna haja ya kutiana hofu.Nikiangalia maisha ya DAR, hasa kwenye vyombo vya usafiri vya umma ni Mungu tu
 
Na haiwezi kufikia hatua hiyo!!ni kweli covid 19, ipo lakini kwa sasa wameshaanza kupika data ili kupata pesa za kufanyia mambo mengine, lakini kwa wananchi wengi ni kama hawana habari nayo, kwani wameishi nayo mwaka na zaidi sasa na maisha yanasonga mbele, hivyo basi hakuna haja ya kutiana hofu.Nikiangalia maisha ya DAR, hasa kwenye vyombo vya usafiri vya umma ni Mungu tu
Hata Samia hana muda na Corona ndo maana kwenye mechi ya simba alikuwepo, Tz hakuna mtu aliye serious na corona
 
Sasa siku zote walikuwa wanaficha nini yani hadi watangaziwe pesa ndio watoe takwimu wakati ugonjwa kweli upo zaidi ya mwaka sasa na watu wanakufa...
Wabongo hamna jema,ni wanafiki na muchknow sana,walimlaumu JK nchi haina Ndege,,Jpm akaja akanunua ndege,wakamlaumu sana na kumlaani,

Wakamlaumu JPM eti hataki kutaja wagonjwa wa corona,amekuja SSH anataja wagonjwa tena wanalaumu.

Hii nchi instaka Rais dictator ndio tunaelewana vizuri
 
Hata Samia hana muda na Corona ndo maana kwenye mechi ya simba alikuwepo, Tz hakuna mtu aliye serious na corona
Wao watoe takwimu zao ili kuwafurahisha hao , wawape pesa ila sisi watuache na maisha yetu kama kawaida tu, tahadhari zile za kawaida ambazo wimbi la kwanza, na la pili yalivyopita na hili litapita, tusitishane tu!

Kwani kwa maisha yetu haya !!hata kenya ni kama usanii tu toka asubuhi yaani wako lundo mtaani kwenye mikutano ya kisiasa eti ikifika saa tatu ndio hutakiwi kuwa nje, utafikiria giza la kuamzia saa nne, ndio lenye virus!!
 
Wao watoe takwimu zao ili kuwafurahisha hao , wawape pesa ila sisi watuache na maisha yetu kama kawaida tu, tahadhari zile za kawaida ambazo wimbi la kwanza, na la pili yalivyopita na hili litapita, tusitishane tu!!kwani kwa maisha yetu haya !!hata kenya ni kama usanii tu toka asubuhi yaani wako lundo mtaani kwenye mikutano ya kisiasa eti ikifika saa tatu ndio hutakiwi kuwa nje, utafikiria giza la kuamzia saa nne, ndio lenye virus!!
Hivi huko duniani wanavyosema wanaruhusu kikundi cha watu kisichozidi watu 10 hv hao watu hawawezi kuambukizana corona kama mmoja wao ana huo ugonjwa.? Mambo ya kuweka lockdown ya muda fulani mpaka fulani ni ujinga mtupu bora waachiwe tuu
 
Wabongo hamna jema,ni wanafiki na muchknow sana,walimlaumu JK nchi haina Ndege,,Jpm akaja akanunua ndege,wakamlaumu sana na kumlaani,
Wakamlaumu JPM eti hataki kutaja wagonjwa wa corona,amekuja SSH anataja wagonjwa tena wanalaumu..
Hii nchi instaka Rais dictator ndio tunaelewana vizuri
Watu wanasema Magufuli alikuwa dikteta lkn mm nilikuwa namuona wa kawaida sana,

Tz ya sasa hakuna anayejua vita, njaa wala udikteta.
 
Kutangaza hiyo idadi kunasaidia Nini? Hata angesema wagonjwa wapo inatosha, maana tulishaambiwa tuzoe tu kuishi nayo kama Malaria ambavyo tunaishi nayo, na inaua wengi zaidi kuliko mafua ya wazungu...
Magufuli wako alificha maradhi nadhani uliona matokeo yake. Hivi nyie team legacy mnawaza kwa kutumia nini?
 
Back
Top Bottom