Serikali: Sehemu zenye maambukizi ya ugonjwa wa malaria kwa wingi ndizo ambazo pia zina wagonjwa wengi wa Seli Mundu

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,814
11,991
Fuatilia yanayojiri kwenye Bunge la 12, Mkutano wa 13, Kikao cha 8, leo Novemba 8, 2023.


Kwa mujibu wa takwimu za Mfumo wa Taarifa za Uendeshaji wa Huduma za Afya (MTUHA), jumla ya wagonjwa 86,990 wa Sickle Cell walihudumiwa kwa mwaka 2022. Aidha, takribani watoto 11,000 kwa mwaka huzaliwa nchini wakiwa na ugonjwa wa Selimundu unaohusisha kurithi vinasaba toka kwa wazazi. Hivyo basi, takribani watu 200,000 Nchini wana ugonjwa wa Sickle Cell.

Haya yamesemwa Bungeni leo, Novemba 8, 2023 na Naibu Waziri wa Afya Dkt. Godwin Mollel wakati akijibu Swali la Fatma Hassan, Mbunge wa Viti Maalum aliyetaka kufahamu ni Watanzania wangapi wenye tatizo la Sickle cell na ni Mikoa mingapi imeathiriwa sana na ugonjwa huu.

Aidha, Mikoa iliyoathiriwa zaidi na ugonjwa wa Sickle Cell ni Mwanza, Tabora, Kigoma, Mara, Dar es Salaam na Pwani. Tafiti pia zinaonyesha, sehemu zenye maambukizi ya ugonjwa wa malaria kwa wingi ndizo ambazo pia zina wagonjwa wengi wa Sickle Cell.

===

SIMBACHAWENE: KAMA 5-1 IMETOKANA NA RUSHWA, SIMBA MKARIPOTI TAKUKURU
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, George Simbachawene amesema kama Klabu ya Simba inaamini kupoteza kwa magoli 5-1 dhidi ya Yanga kumechangiwa na mazingira ya rushwa basi taarifa hiyo ikaripotiwe Ofisi ya TAKUKURU Temeke, Dar es Salaam.

Awali, Mbunge Festo Sanga alihoji mpango wa Serikali kukabiliana na rushwa baada ya kuwa na tetesi za madai ya rushwa katika mchezo huo wa Ligi Kuu Bara uliopigwa kwenye Uwanja wa Mkapa.
 
Watu hatuna mzuka na bunge la majizi ya kura. Hata usipoleta habari zao hakuna atakayezimisi.
 
Back
Top Bottom