Jembe Jembe
JF-Expert Member
- Jun 9, 2016
- 757
- 1,822
Mkuu wa mkoa wa Arusha,Mrisho Gambo ametengua maamuzi ya Mkurugenzi wa jiji la Arusha, aliyoyatoa ya kusitisha kibali cha ujenzi wa jengo la Mahakama katika mahakama kuu jijini hapa ,akidai kuwa ujenzi huo uendelee na hakuna MTU wa kuzuia.
Gambo alitua kama Mwewe katika eneo la ujenzi akitokea wilayani Ngorongoro alikokuwa ziarani ,ambapo alidai kwamba Mara baada ya mchakato wa ujenzi wa jengo hilo kuanza ,halimashauri ya jiji la Arusha ilitoa kibali cha ujenzi tarehe 18, desemba/2019 .
"Lakini tarehe 11/3/2020 halmashauri hiyohiyo iliandika barua nyingine kwa jaji mfawidhi ikimtaka kusitisha ujenzi wa jengo la Mahakama kwa madai kwamba jengo hilo lipo karibu na Ikulu ndogo hivyo kuwa na usalama mdogo"
Gambo amesema kuwa kimsingi Mahakama hii sio mpya ni jengo ambalo lipo miaka yote nashughuli za Mahakama zilikuwa zinafanyika hapa na Mahakama sio taasisi ya MTU binafsi ni taasisi ya umma.
"Mimi kama mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama ya Mkoa natambua kuwa hii Mahakama haijawahi kuwa tishio la usalama hivyo nimeona kuwa barua iliyoandikwa na Mkurugenzi wa jiji la Arusha, Dkt Maulid Madeni haina mashiko hivyo kwa mamlaka niliyonayo naifuta rasmi na kuagiza ujenzi uendelee na hakuna MTU yoyote atakaye kuja kuzuia ujenzi wa jengo la Mahakama" amesema Gambo
Mkuu huyo wa mkoa alimhakikishia jaji mfawidhi kama kuna MTU yoyote atakuja hapa kuzuia ujenzi huo atoe taarifa Mara moja ili akamatwe na awekwe ndani kama kutakuwa na lawama yoyote Mimi ndio nitahangaika nayo