Cannabis
JF-Expert Member
- Jan 20, 2014
- 8,938
- 25,282
MKUU wa Mkoa wa Mwanza, Albert Chalamila, amewataka wakazi wa mkoa huo kunywa pombe kwa kuwa inachangia kukuza uchumi wa nchi kupitia kodi za serikali.
Chalamila ameyasema hayo jana jijini Mwanza alipozungumza na uongozi wa Mamlaka ya Mapato (TRA).
Alisema watu wakiacha kunywa pombe maana yake mapato ya serikali yatapungua kwa sababu unywaji pombe unaongeza kodiza serikali.
Kuhusu baadhi serikali ya baa kupiga kelele za muziki, Chalamila alisema hapo ndiyo mahala pake, kwa kuwa asingetegemea sehemu kama hizo ziwe na utulivu.
Aidha, alitaka TRA kukusanya mapato ya serikali kwa “kuwafinya kidogo” wafanyabiashara wasiotaka kulipa kwa hiari.
Alisema licha ya Rais Samia Suluhu Hassan kuagiza TRA kutumia busara na akili, lakini wakati mwingine lazima wawe wakali kwa wafanyabiashara wasiotaka kulipa kwa hiari.
Kuhusu wafanyabiashara kutoa risiti halali wanapouza bidhaa zao, Chalamila alitaka TRA kusimamia hilo.
Aidha, Chalamila alisema wafanyabiashara wengi hawatoi risiti za mashine wakati wa kuuza bidhaa zao, hatua ambayo inaikosesha mapato serikali na kuagiza TRA kuweka mkazo katika eneo hilo.
Mkuu wa huyo wa mkoa baada ya kukabidhiwa ofisi, alianza ziara ya kutembelea taasisi mbalimbali za serikali na kuzungumza na watumishi.