RC Chalamila awataka wakazi wa Mwanza kunywa pombe ili kuchangia ukuaji wa uchumi wa nchi, asema baadhi ya baa kuwa na kelele za muziki ni sawa

Cannabis

JF-Expert Member
Jan 20, 2014
8,906
25,180
imgonline-com-ua-twotoone-Y3CdGG4GrNxs.jpg

MKUU wa Mkoa wa Mwanza, Albert Chalamila, amewataka wakazi wa mkoa huo kunywa pombe kwa kuwa inachangia kukuza uchumi wa nchi kupitia kodi za serikali.

Chalamila ameyasema hayo jana jijini Mwanza alipozungumza na uongozi wa Mamlaka ya Mapato (TRA).

Alisema watu wakiacha kunywa pombe maana yake mapato ya serikali yatapungua kwa sababu unywaji pombe unaongeza kodiza serikali.

Kuhusu baadhi serikali ya baa kupiga kelele za muziki, Chalamila alisema hapo ndiyo mahala pake, kwa kuwa asingetegemea sehemu kama hizo ziwe na utulivu.

Aidha, alitaka TRA kukusanya mapato ya serikali kwa “kuwafinya kidogo” wafanyabiashara wasiotaka kulipa kwa hiari.

Alisema licha ya Rais Samia Suluhu Hassan kuagiza TRA kutumia busara na akili, lakini wakati mwingine lazima wawe wakali kwa wafanyabiashara wasiotaka kulipa kwa hiari.

Kuhusu wafanyabiashara kutoa risiti halali wanapouza bidhaa zao, Chalamila alitaka TRA kusimamia hilo.

Aidha, Chalamila alisema wafanyabiashara wengi hawatoi risiti za mashine wakati wa kuuza bidhaa zao, hatua ambayo inaikosesha mapato serikali na kuagiza TRA kuweka mkazo katika eneo hilo.

Mkuu wa huyo wa mkoa baada ya kukabidhiwa ofisi, alianza ziara ya kutembelea taasisi mbalimbali za serikali na kuzungumza na watumishi.
 
Point wacha tu tunywe maisha yenyewe mafupi hivi jiwe tumemzika hata urais ajaufaidi vizuri.

Wacha tulewe tu maisha ni mafupi sana pesa tumeshatafuta na tunaendelea kutafuta halafu tufe tuziache ..

Kelele maana yake ulichagua mwanza kuna maeneo mengi sana yasiyo na usumbufu wa kelele

Kama Kiseke, Buswelu usagala, Nyasaka,Kiloleli, Nyamongoro na maendeo mengine mengi

Uza kwenye kelele kajenge kwenye utulivu.

Yupo sahihi 100%.
View attachment 1800253
 
Atleast leo kaongea kitu..ila swala la kelele kwa bar zilizokaribu na makazi ya watu ni za kuangaliwa.

Watu wanywe BEER..
Swala la kelele wakiliingiza tutaingia hadi haya makanisa ya uswahili yanayokesha.
 
Kama kanyongeza ka mshahara na posho ni hadi kukunjana mashati, nani atakuwa na jeuri ya kuweka kikao hata cha nusu saa bar......ndo maana tunashuhudia bar zimebaki viti vitupu na hii imeenda kuua ajira za wahudumu wa bar na wajasiriamali wengine kama supu na nyama choma.
 
Point wacha tu tunywe maisha yenyewe mafupi hivi jiwe tumemzika hata urais ajaufaidi vizuri.

Wacha tulewe tu maisha ni mafupi sana pesa tumeshatafuta na tunaendelea kutafuta halafu tufe tuziache ..

Kelele maana yake ulichagua mwanza kuna maeneo mengi sana yasiyo na usumbufu wa kelele

Kama Kiseke, Buswelu usagala, Nyasaka,Kiloleli, Nyamongoro na maendeo mengine mengi

Uza kwenye kelele kajenge kwenye utulivu.

Yupo sahihi 100%.
View attachment 1800253
Huyu anafaa sana kuwa RC wa Kilimanjaro
 
View attachment 1800234
MKUU wa Mkoa wa Mwanza, Albert Chalamila, amewatakavwakazi wa mkoa huo kunywa pombe kwa kuwa inachangia kukuza uchumi wa nchi kupitia
kodi za serikali.

Chalamila ameyasema hayo jana jijini Mwanza alipozungumza na uongozi wa Mamlaka ya Mapato (TRA).

Alisema watu wakiacha kunywa
pombe maana yake mapato ya
serikali yatapungua kwa sababu
unywaji pombe unaongeza kodi
za serikali.

Kuhusu baadhi serikali ya baa kupiga kelele za muziki, Chalamila alisema hapo ndiyo mahala pake, kwa kuwa asingetegemea sehemu kama hizo ziwe na utulivu.

Aidha, alitaka TRA kukusanya
mapato ya serikali kwa “kuwafinya kidogo” wafanyabiashara wasiotaka kulipa kwa hiari.

Alisema licha ya Rais Samia Suluhu Hassan kuagiza TRA kutumia busara na akili, lakini wakati mwingine lazima wawe wakali kwa wafanyabiashara wasiotaka
kulipa kwa hiari.

Kuhusu wafanyabiashara kutoa risiti halali wanapouza bidhaa zao, Chalamila alitaka TRA kusimamia hilo.

Aidha, Chalamila alisema wafanyabiashara wengi hawatoi
risiti za mashine wakati wa kuuza bidhaa zao, hatua ambayo inaikosesha mapato serikali na kuagiza TRA kuweka mkazo katika eneo hilo.

Mkuu wa huyo wa mkoa baada
ya kukabidhiwa ofisi, alianza
ziara ya kutembelea taasisi mbalimbali za serikali na kuzungumza na watumishi.
Wewe na chalamila akili zenu zinafana!! ona hata ulivyoandika!!
 
8 Reactions
Reply
Back
Top Bottom