RC Mongela awashukia Wafanyabiashara waliogeuza Mkoa wa Arusha uchochoro wa bidhaa bandia

Jembe Jembe

JF-Expert Member
Jun 9, 2016
749
1,797
Na Joseph Ngilisho ARUSHA

MKUU wa Mkoa wa Arusha John Mongela ameagiza kuchukuliwa hatua Kali kwa wafanyabiashara wasiowaaminifu ambao bado wanaendekeza tabia ya kuingiza bidhaa bandia mkoani humo kwa lengo la kujipatia faida zaidi huku wakihatarisha Afya za walaji.

Akiongea wakati akifungua mkutano wa siku moja wa walipa kodi wa sekta mbalimbali pamoja na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) wenye lengo la kuboresha ukusanyaji bora wa mapato na utatuzi wa changamoto zinazowakabili wadau hao,Mongela alisema mkoa huo umegeuzwa kichochoro cha bidhaa feki jambo ambalo halikubaliki.

Alisema kuingizwa kwa bidhaa bandia mkoani humo kunachangia kurudisha nyuma uzalishaji viwandani na kufifisha uchumi wa Taifa ikiwemo kukosekana kwa mapato ya Serikali.

"Katika hili naonya wahusika acheni mara moja vinginevyo atakayeendelea na mchezo huu hatutamchelea tukimpata tutamchukulia hatua kali,"alisema

Aidha aliwaasa wafanyabiashara kujenga uchumi wa nchi kwa amani kupitia ulipaji kodi wa hiari.

Alisema vema baadhi ya mfanyabiashara wakaacha ujanja ujanja wa kulipa kodi hadi kusukumwa kwani haileti tija kwa nchi.

Pia ameiomba TRA kuhakikisha wanatatua changamoto ya ukosefu wa mashine za EFDs ambako hutumiwa na baadhi ya wafanyabiashara kukwepa kodi.

"Ukimfuata mfanyabiashra anakuambia nimeenda nimeambiwa mtandao unasumbua mara hazipatikani kwa sasa hivyo nimeruhusiwa kufa biashara kwa wiki hizi bila mashine, hii sio sawa maana inachangia kupotea kwa mapato ya serikali tutatue hili zipatikane kirahisi,"alisema.

Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Alphayo Kidata amewaagiza wafanyabiashara kuzingatia utunzaji wa kumbukumbu za biashara zao ili kuwezesha maofisa wake kukadiria kodi halali.

Aidha ameagiza uzingatiaji wa matumizi sahihi wa mashine za kielekroniki (EFDs) na TRA itafanya ukaguzi ili kubaini wanaokwepa kuzitumia.

"Mtakapotunza kumbukumbu mtawezesha maofisa wetu TRA kukadiria kodi sahihi isiyozua manung'uniko hivyo muhimu mkatunza vizuri kumbukumbu za biashara zenu,"alisema.

Aidha alisisitiza kwa kila anayenunua bidhaa kudai risiti za WFDs na anayeuza kuzingatia anazitoa ili kukwepa adhabu kali kwao isiyo ha lazima.

"Katika hili tutakagua ili kubaini wajanja wanaokwepa kuzitumia na adhabu za kisheria zipo wazi zitachukuliwa dhidi yao,"alisema.

Mmoja wa baadhi ya wafanyabiashara wa sekta ya maua na mbogamboga (TAHA)Kelvin Remen ameshukuru TRA kushirikiana na wadau wa kodi kuwatia moyo, kwani awali sekta hiyo ilikumbana na changamoto mbalimbali na kurudisha nyuma ukusanyaji wa mapato.

IMG_20210714_105821_999.jpg
IMG_20210714_105837_049.jpg
IMG_20210714_105805_707.jpg
 
Mheshimiwa tumeletewa Rozi Roisi bandia, ikipita Arusha ikamate🤣🤸🐒
 
Back
Top Bottom