Influenza
JF-Expert Member
- Jul 1, 2018
- 1,445
- 3,403
Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila, amewatakia kila la heri wafuasi wa CHADEMA waliokutana maeneo ya Mbezi Mwisho stendi ya Magufuli kwa ajili ya kuanza maandamano ya amani na kuwataka kuulinda uwekezaji uliopo ndani ya Jiji hilo wasiuharibu na badala yake wafikishe ujumbe walioukusudia siku ya leo.
"Mnatakiwa kufikisha ujumbe pale mlipokusudia, serikali tuko na nyie na tunawatakia kila la heri, ninyi na mimi ni wana Dar es Salaam penye mzunguko mkubwa wa pesa, penye hospitali kubwa na uwekezaji mkubwa, maandamano yetu yanapaswa kulinda uwekezaji wote huo, Rais Samia na viongozi wote wamesema wacha watu waandamane," amesema Chalamila