RC Arusha ampongeza jaji aliemvua ubunge Godbless Lema...

RC Arusha ampongeza jaji aliemvua ubunge Godbless Lema...

Mungi.
Sheria ni taaluma lazima tujenge utamaduni wa kuheshimu kazi za watu, kama wewe ni mfanyabiashara wa korosho utaheshika na kazi yako, kama wewe unatoa mahindi Mbeya utaheshimika na kazi yako, kila mtu aheshimu kazi ya mwenzake.

Ritz, wewe umesomea sheria hebu tuambie hivyo vifungu alivyosema Mungi hapo juu vilitumika sawasawa katika kesi ya Lema?
 
Sina mashaka kabisa na wakaazi wa ar town huyo rc nadhani angetulia na kujifunza yaliowapata wenzake,anaacha kushughulikia msongamano wa mahabusu na wafungwa gerezani yeye anampongeza jaji kwa kesi ya lema mbona kesi kibao huyo jaji ameshindwa kuzimaliza mapema na zipo chini yake? huu ni ujinga wa kishabiki wa wazi kabisa inasikitisha kuona mteule wa rais hajui majukumu yake
 
Jana RC wa Arusha (Magesa) aliwashukuru majaji kwa kazi waliyoifanya, imesaidia kurudisha amani Arusha na alisema wale wasioridhika waende kwenye ngazi inayofata na siyo kulalamika na kunyooshea watu vidole kwani haisaidii kwani imeshafanyika na na maamuzi tayari yameshatoka…..
Magesa nilini amani Arusha ilitoweka na ni nani aliitoa amani, je amani inaletwa mahakama na kuajiri polisi wengi nchini…..
Asubiri maamuzi ya rufaa apongeze tena majaji wa mahakama ya rufaa, ila swala la ccm hapa arusha itabaki story.
 
Hapa kazi ipo, jaji anapongezwa!! hapa kulikuwa na namna!
 
Unajua huyu bwana kabla ya kupewa zawadi ya urc na bwanake ambaye hivi sasa yuko usa alikuwa huko kwao bwanake kama dc sasa alishughulikiwa vizuri huko nyuma alipokuwa pwani huu urc ni kama pongezi!
 
Ufinyu wa mawazo na kutojua uongozi. Tena kauli yake inadhihirisha hukumu ina mkono wa mtu na ilipangwa.
 
huyo RC hajui hapo alipo anaongoza 20% ya watu wa Arusha ambao ni CCM na 80% ni CDM. asitarajie kupata mafanikio yeyote au kukubalika na wananchi wa Arusha na isitoshe huu mwanzo anaouonyesha ni mbaya sana pia hii inaonyesha kabisa katika nchi yetu hakutakiwi kuwa na vyeo kama hivi kwani hakuna majukumu ya maendeleo wanayofanya hawa watu isipokuwa ni kulinda maslahi ya CCM
 
Jana RC wa Arusha (Magesa) aliwashukuru majaji kwa kazi waliyoifanya, imesaidia kurudisha amani Arusha na alisema wale wasioridhika waende kwenye ngazi inayofata na siyo kulalamika na kunyooshea watu vidole kwani haisaidii kwani imeshafanyika na na maamuzi tayari yameshatoka…..
Magesa nilini amani Arusha ilitoweka na ni nani aliitoa amani, je amani inaletwa mahakama na kuajiri polisi wengi nchini…..


Sijui lini utakuja leta hoja ya maana kwani siku zote ww ni mtu wakulalamika lalamika tu. Na kama uko hivyo na kwenye familia yako nawaonea huruma
 
Unajua huyu bwana kabla ya kupewa zawadi ya urc na bwanake ambaye hivi sasa yuko usa alikuwa huko kwao bwanake kama dc sasa alishughulikiwa vizuri huko nyuma alipokuwa pwani huu urc ni kama pongezi!

Halafu nyie ndio mnataka kuongoza dola kwa mawazo mgando nammna hii. Nchi hii mtaiona hivi hivi na katu dola ham to ipata
 
Jamani JF tupunguze kulalamika kila siku. Alichokisema RC ndo mwisho wa upeo wake wa kufikiri. Cha kufanya ni kumsaidia kwa kulirudisha jimbo hilo kwa M4C then atarudi bafuni kwake asugue kichwa kwa gunzi ili aweze kufikiri kwa umakini zaidi
 
Chadema hawaishi kulalamika kesi zote zinazowapa ushindi wao wanasifia Majaji na kuwaita wasomi, lakini kwenye kesi wanazoshindwa wanawaita majaji wapumbavu...siku wakichukuwa nchi sijui itakuaje kwenye suala la uhuru wa Mahakama.
Kuna vitu vingine huhitaji kushirikisha akili yako yote kugudua uozo...nakuomba ushirikishe angalau robo ya ubongo wako kama unao utagudua nini kilifanyika kwenye kesi ya Arusha zidiya Lema...
 
Jamani JF tupunguze kulalamika kila siku. Alichokisema RC ndo mwisho wa upeo wake wa kufikiri. Cha kufanya ni kumsaidia kwa kulirudisha jimbo hilo kwa M4C then atarudi bafuni kwake asugue kichwa kwa gunzi ili aweze kufikiri kwa umakini zaidi
Sijaona kidude cha Like.....
 
Halafu nyie ndio mnataka kuongoza dola kwa mawazo mgando nammna hii. Nchi hii mtaiona hivi hivi na katu dola ham to ipata
MasaburiBrain, Kwani wewe ni nani mpaka uwasemee watanzania, mwaka 2014 Chadema kinaanza kuiongoza nchi hii na mwaka 2015 CCM kitakuwa chama cha upinzani.
 
Sijui lini utakuja leta hoja ya maana kwani siku zote ww ni mtu wakulalamika lalamika tu. Na kama uko hivyo na kwenye familia yako nawaonea huruma
Kwani Mama MasaburiBrain alisha kulalamikia....!?
 
Ritz, wewe umesomea sheria hebu tuambie hivyo vifungu alivyosema Mungi hapo juu vilitumika sawasawa katika kesi ya Lema?

Jaji Gabriel Rwakibarila, alimtia hatiani Lema kwa makosa mawili kati ya manne aliyokuwa akikabiliwa nayo, huku akitupa mawili kwa kukosa ushahidi.
 
Ritz,
Mahakama ilimtia hatiani Lema kwa kifungu na.108
Rwakibarila akamhukumu Lema kwa kifungu na.114.Je, huu si upumbavu wa Rwakibarila?

108.-(1) The election of a candidate as a member shall not bequestioned save on an election petition.
(3) The election of a candidate as a member shall be declared void on
any of the following grounds which are proved to the satisfaction of the
court, namely-

(b) that, during the election campaign, statements were made by the
candidate, or on his behalf and with his knowledge and consent
or approval with intent to exploit tribal, racial or religious issues
or differences pertinent to the election or relating to any of the
candidates or, where the candidates are not of the same sex, with
intent to exploit such difference:
Provided that no petition may be presented on the grounds set out
in this paragraph without the consent in writing of not less than
one of the supervisory delegates appointed for the relevant election;

114.-(1) At the conclusion of the trial petition, the court shall also
report in writing to the Director of Elections-
(a) whether any corrupt of illegal practice has not been proved to have
been committed by or with the knowledge and consent or approval
of any candidate at the election. and the nature of such practice,
if any and
(b) the names and descriptions of all persons, if any, who have been
proved at the trial to have been guilty of any such practice.

Mungi.

Jaji Rwakibiria alimtia Lema, hatiani kwa kosa la 'Illegal Campaign' kwa kutoa kauli za kumbagua kijinsia Dr Burian.

Kwa mujibu wa sheria za uchaguzi makosa yote yaliyokuwa yanamkabili Lema, makosa mawili yanaangukia kwenye kifungu cha 108, kifungu kidogo cha pili aya 'A' ambayo huruhusu aliyevuliwa ubunge kukombea kwenye uchaguzi mdogo.

Kifungu cha 114 cha sheria ya uchaguzi kinazungumzia 'Illegal' kwa hiyo Jaji alitoa hukumu sahihi.
 
Jana RC wa Arusha (Magesa) aliwashukuru majaji kwa kazi waliyoifanya, imesaidia kurudisha amani Arusha na alisema wale wasioridhika waende kwenye ngazi inayofata na siyo kulalamika na kunyooshea watu vidole kwani haisaidii kwani imeshafanyika na na maamuzi tayari yameshatoka…..
Magesa nilini amani Arusha ilitoweka na ni nani aliitoa amani, je amani inaletwa mahakama na kuajiri polisi wengi nchini…..

Halafu tukianza kupost post code zake kama walivyofanya mashabiki wa Man kwa Tevez watu wataanza kupiga kelele. huu ni uchokozi wa wazi kabisa!
 
Sidhani hii kauli ni ya kupuuza, Lema alikuwa hapendi haki idhulumiwe na yuko tayari kuadhibiwa kwa ajili ya haki, ndiyo maana RC amefurahia ili waendelee kuwanyanyasa, kuwaibia, kuwadhulumu na kuwakandamiza watu wa Arusha. Wamemwaga damu na kuwaua raia wasio na hatia kwa kuwa walikuwa wanadai haki zao, hiyo laana hawatapona. Shame on them.

Mshaurini magesa afanye ufisadi utakamtosheleza mpaka siku ya kufa maana kuanzia 2015 atakuwa jobless maana RC na DC siyo sera ya cdm
 
Back
Top Bottom