RC Arusha ampongeza jaji aliemvua ubunge Godbless Lema... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

RC Arusha ampongeza jaji aliemvua ubunge Godbless Lema...

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Crashwise, May 18, 2012.

 1. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #1
  May 18, 2012
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  Jana RC wa Arusha (Magesa) aliwashukuru majaji kwa kazi waliyoifanya, imesaidia kurudisha amani Arusha na alisema wale wasioridhika waende kwenye ngazi inayofata na siyo kulalamika na kunyooshea watu vidole kwani haisaidii kwani imeshafanyika na na maamuzi tayari yameshatoka…..
  Magesa nilini amani Arusha ilitoweka na ni nani aliitoa amani, je amani inaletwa mahakama na kuajiri polisi wengi nchini…..
   
 2. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #2
  May 18, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,672
  Trophy Points: 280
  Crashwise,
  Wewe ulikuwa unataka RC wa Arusha afanyaje?
   
 3. Mvaa Tai

  Mvaa Tai JF-Expert Member

  #3
  May 18, 2012
  Joined: Aug 11, 2009
  Messages: 6,174
  Likes Received: 2,175
  Trophy Points: 280
  Awape pole wana Arusha kwa yaliyotokea, kwani haikutegemewa kwamba wana Arusha watamkosa mbunge wao mpenzi
   
 4. Kirode

  Kirode JF-Expert Member

  #4
  May 18, 2012
  Joined: Mar 25, 2011
  Messages: 3,573
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Kwani we ritz ulitaka rc afanyeje
   
 5. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #5
  May 18, 2012
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,194
  Likes Received: 134
  Trophy Points: 160
  Majaji hawapongezwi,Kutoa hukumu ni sehemu ya kazi Yao. Mkuu wa mkoa anasyndrome ya kuvalishwa mashada ya maua shingoni. Ukivalishwa shada la maaua wakati wa kuapishwa ni dalili ya mapungufu.
   
 6. F

  FJM JF-Expert Member

  #6
  May 18, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145

  Aliye juu mngoje chini. Huyu RC anaweza kuwafurahisha wakubwa zake lakini miaka miwili na nusu kutoka sasa mambo yanaweza kuwa tofauti sana. Busara ndogo tu ingemsaidia kuchunga ulimi wake.
   
 7. Mzee wa Rula

  Mzee wa Rula JF-Expert Member

  #7
  May 18, 2012
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 8,177
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Magesa Malongo bana!!!!! Hakutakiwa kusema hivyo ni mapema mno kuonyesha ushabiki wa wazi namna hiyo.
   
 8. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #8
  May 18, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Huyu RC ni MPYA alijuaje mabaya ya Mbunge wa Arusha Mjini? aliyasikia kama sisi tu? Hii ndio inaonyesha upungufu wa Uongozi nchini kwetu kuwa na sura mbili na kubobea kulamba lamba wakuu miguu ili kupewa Vyeo tu na sio Kufanya kazi

  Nchi yetu kila mtu ili upata Uongozi ni kulamba miguu ya wakuu wako au uwe mtoto wa kigogo period. wengine tokeni Jasho
   
 9. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #9
  May 18, 2012
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,194
  Likes Received: 134
  Trophy Points: 160
  Awaulize wenzie CCM damu, wameanza kujitayarisha kuwa wapinzani.

  Wamesoma alama za nyakati, belatedly though!!!!!!
   
 10. Angel Msoffe

  Angel Msoffe JF-Expert Member

  #10
  May 18, 2012
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 6,797
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Huyo RC katumwa
   
 11. N

  Naytsory JF-Expert Member

  #11
  May 18, 2012
  Joined: Nov 3, 2011
  Messages: 1,590
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Sidhani hii kauli ni ya kupuuza, Lema alikuwa hapendi haki idhulumiwe na yuko tayari kuadhibiwa kwa ajili ya haki, ndiyo maana RC amefurahia ili waendelee kuwanyanyasa, kuwaibia, kuwadhulumu na kuwakandamiza watu wa Arusha. Wamemwaga damu na kuwaua raia wasio na hatia kwa kuwa walikuwa wanadai haki zao, hiyo laana hawatapona. Shame on them.
   
 12. CHUAKACHARA

  CHUAKACHARA JF-Expert Member

  #12
  May 18, 2012
  Joined: Jun 3, 2011
  Messages: 12,213
  Likes Received: 3,822
  Trophy Points: 280
  Very right, unampongeza jaji kwa vile amepindisha haki. kama ametoa haki hupashwi kumpongeza maana ilibidi haki iwe hivyo! Kwa hiyo jaji alifanya mambo!!!
   
 13. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #13
  May 18, 2012
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  CHADEMA TUTUMIE 'OPERESHENI VUA GAMBA VAA GWANDA' KUKAMATA UONGOZI MASHINANI KWA ZAIDI YA ASILIMIA 80 % KABLA YA 2015

  CDM, malengo ya 'Operesheni Vua Gamba Vaa Gwanda' yawe ni kushika asilimia 80% ya
  (1) Uwenyekiti wa viti vya vijiji,

  (2) Viti vya Udiwani pamoja,na

  (3) Ubalozi wa Nyumba 10 kote nchini.

  Pindi tutakapofikia malengo magumu kama hayo ndipo tutakapoweza kusema tukiwa kifua mbele kwamba CDM Nguvu ya Umma kweli kwa kuegemea malengo yanayopimika kisayansi kama hayo hapo juu.

  Hakika tukifikia malengo hayo hapo juu basi kwa njia hii, hata MAFISADI wafanyeje 2015 lazime tuwashike.

  Isitoshe, malengo haya ni ya muhimu sana kwetu kuweza kuweka pamoja nguvu ya umma kuandika KATIBA MPYA YA WANANCHI na kukataa hayo mabadiliko ya kuweweseka ambayo CCM kinaonekana kuanza kupendekeza kwenye vikao vyake hivi sasa.
   
 14. A

  AlamaZA NYAKATI JF-Expert Member

  #14
  May 18, 2012
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 274
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Huyu sasa ngoja tumwonyeshe M4C hapa AR ndo atambue
   
 15. Fredrick Sanga

  Fredrick Sanga JF-Expert Member

  #15
  May 18, 2012
  Joined: Jan 27, 2011
  Messages: 3,148
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Hizi sindio zile nafasi ambazo hazina tija, RC, DC zifutwe kwenye katiba mpya. Wakafundishe primary, au shule za kata. Tunapoteza kudi bure tu. Nafasi hizi zilikuwa kwa ajili ya wakoloni kukandamiza wananchi. Sasa tunahitaji viongozi wa kuchaguliwa sio kuteuliwa. Peoples power.
   
 16. Kiganyi

  Kiganyi JF-Expert Member

  #16
  May 18, 2012
  Joined: Apr 30, 2012
  Messages: 1,244
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Huyo **** na cheo cha bure linanikera kishenzi!

  Bonge la mlamba kiatu!
   
 17. Fredrick Sanga

  Fredrick Sanga JF-Expert Member

  #17
  May 18, 2012
  Joined: Jan 27, 2011
  Messages: 3,148
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Akafundishe shule ya kata moja huko kawe. Huko hamna kazi. Hukumsikia Dk Rwaitama akichambua vitu. Hawa walikuwa na maana kwa watawala wa kikoloni. Ndio maana kazi ya kujikombakomba. Hawajibiki kwa wananchi.
   
 18. P

  Precise Pangolin JF-Expert Member

  #18
  May 18, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 12,197
  Likes Received: 1,978
  Trophy Points: 280
  Badala ya kusikitika chaguo la wananchi limetolewa anafurahia! Jamani wana bodi angalieni jinsi viongozi wa nchi hii wasivyokuwa na mapenzi kwa wananchi wao ngoja tuu siku zinakaribia
   
 19. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #19
  May 18, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,672
  Trophy Points: 280
  Mahakama imefanya kazi yake kwa mujibu wa sheria za nchi Lema, kakutwa na hatia tujenge utamaduni wa kuheshimu sheria...RC katoa pongezi kwa Jaji kwa kusimamia sheria za nchi hakuna ubaya wowote...mbona Mbowe, alitoa pongezi kwa Jaji kule Singida kwenye kesi ya Tundu Lissu.
   
 20. MNYISANZU

  MNYISANZU JF-Expert Member

  #20
  May 18, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 7,056
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  I hate Mulongo more than .... Go to hell Mulongo.
   
Loading...