Ratiba yako ya kwenda 'Site' ni ipi?

Nimepanga kupaua mjengo kwa bati ya msouth Versatile, nimeshapeleka mafundi wa kupaua watatu tofauti kupima na kufanya estimation ya gharama za material + ufundi, estimation zao hazipishani average ni = 17M...
Utatoboa kaka kama nia ipo. Hata hivyo ukiweza kuishi bila kujali mitazamo ya wengine utafurahia maisha. Kama bati za kawaida zitafanya maisha yako yawe mepesi weka tu hizo hizo halafu ndani unaweka gypsum board ya maana!
 
Mimi nilikuwa naenda site kila jumapili jioni,kumbe bhana kuna watu wakaniona na wakaja kumwambia bosi wangu kuwa najenga,dah!yani haka kajumba kalinitesa sana na bado nusu nifukuzwe kazi,hyo nazungumzia miaka 6 iliyopita.

Sent from my Infinix X5515 using JamiiForums mobile app
Kwamba hawakutaka kuona unapiga hatua za kimaisha kupitia pato lako? Kazi gani hiyo ilikuwa mkuu au kiwandani wakahisi unawaibia? teh
 
Nimepanga kupaua mjengo kwa bati ya msouth Versatile, nimeshapeleka mafundi wa kupaua watatu tofauti kupima na kufanya estimation ya gharama za material + ufundi, estimation zao hazipishani average ni = 17M...
Naimani ukiweka kufaulu mbele utatoboa sabab kila kitu kwenye haya maisha kipo ndani ya uwezo wetu so nikuamua sababu unaweza mimi nakuamini
 
daa mm naendaga kucheck kokote na tofari maana unaweza kuta vumbi wakiiba ila mawe,michanga sio rahisi kuibwa
Hivi matofali yanaweza kukaa muda gani kabla ya kujengwa? Maanake kuna nyumba naziona zimeachwa mpaka matofali yanaanza kulika.
 
Hivi matofali yanaweza kukaa muda gani kabla ya kujengwa? Maanake kuna nyumba naziona zimeachwa mpaka matofali yanaanza kulika.
Inategemeana na udongo uliotumika kufyatulia,kama ni ule mfinyanzi mweusi yakichomwa yanakuwa mekundu au meupe hizo tofari hata zikikaa miaka 20 bado hakuna tatizo haziathiriwi na mvua wala nini.

Ukikuta tofari iliyochomwa inalia kama chuma yaani hiyo ni kiboko huwa ni ngumu sana,hizo tofari zinapatikana zaidi Mkoa wa Songwe,Njombe na baadhi ya maeneo ya Mkoa wa Rukwa.Huenda zipo maeneo mengine lakini kwa maneo niliyopita na kuishi nafahamu zaidi huko.

Lakini kuna zingine zikichomwa zinzkuwa nyekundu nazo ni nzuri ila zina ugumu wa kati,hizi ziko maeneo mengi kama Mkoa wa Arusha,Kigoma,Ruvuma na maeneo mengine yasiyo na mchanag mwingi.Tofauti na hapo ni tofari zenye ugumu wa chini ,hizi ni kila mkoa zipo na ndio huwa zikiwa exposed na mvua/unyevu na weather chini ya miaka 2 zinapukutika kwa hiyo hata ukizijengea hakikisha unapiga plaster ukuta wako.
 
Inategemeana na udongo uliotumika kufyatulia,kama ni ule mfinyanzi mweusi yakichomwa yanakuwa mekundu au meupe hizo tofari hata zikikaa miaka 20 bado hakuna tatizo haziathiriwi na mvua wala nini...
Nauliza hizi sa saruji na mchanga.
 
Mimi nilishakuwa nimeandaa madirisha yangu na milango ya nyumba nzima kabla sijaanza ujenzi, na kumpa fundi vipimo vyake, walipoanza walikosea ukubw akidogo ila sababu kila jioni ninaenda nikawa ninajua mapema tukairekebisha kabla ya kuta kuanza kupanda, hilo moja ninalokumbuka kwa haraka.
Kuta kupanda inakuwaje sijaelewa
 
Kama kawaida yetu. Ikifika siku za wikiendi tunakumbushana kwenda site.

Wangapi leo mnaenda tujuane? Mnaweza kutupigia tukazungumza kidogo.

Namba zetu 0782425190
 
Back
Top Bottom