Mkuu umeandika mambo ya msingi sana, lakini tatizo linabaki kwa watanzania tu, hiyo level bado mkuu.
Bado sana watz kifikra, kitamaduni, kiujasiri na pia kiuelewa.
Watz siku ya CAG anazungumza wanashindwa kujaa kwenye Tv na kuangalia kinachoendelea, tv is very simple lakini siku hiyo watu wanafanya yao.
Ila siku ya yanga na simba wanajaa saaaaanaaaa.
Mentality ile ile inayowafanya wasijae kuangalia CAG anasema nini basi ndio mentality hiyo hiyo itakayowwafanya wao wasiandamane live.
Kwenye keyboard haya maandamano yamefanikiwa kwa 200000% ila kwenye real life ndio NTITI.
tunahitaji wenye muamko wa kufuatilia yanayoendelea serikalini kama ambavyo wana muamko wa kufiatilia yanayoendelea simba na yanga...
No, sio hivyo,ushawahi kufikiria otherwise?
Mfano hata mimi sioni mantiki ya kusikiliza hotuba ya CAG ilihali najua wazi kabisa hakuna hatua za uwajibikaji zitazochukuliwa kwa hao watao onekana kufuja pesa za kodi zetu.
Hiyo hotuba kama haitakuwa na impact ya uwajibikaji kuwafanya watawala waogope kufuja pesa, then why should I waste my time watching it?
Mimi nayapima zaidi haya maandamano kupitia upande wanaojaribu kuyazuia, resistense wanayoionesha inaonesha wazi kabisa hiki kitu ni real.
Wameziweka media zote mifukoni mwao wakidhibiti zisitangaze content yoyote kuhusu maswala ya maandamano isipokuwa zile content zenye kutishia waandamanaji.
Wamenunua viongozi wa dini, wanaharakati, wasanii, influencers na public figures wengine ili wajaribu kuwahimiza wananchi wasiandamane.
Na jana nimeona hadi media za Kenya nazo zimelipwa ili kuwatisha waandamanaji.
Mkuu wa majeshi anazunguka kila mkoa kuwataka wanajeshi wasiungane na wananchi watao andamana.
Na kuna tetesi pia kuwa kuna wanajeshi kutoka UG wamekodiwa kwa ajili ya kuzuia maandamano kufuatia kauli ya Captain Tesha aliyodai wanajeshi wapo upande wa wananchi.
So, mimi siwezi kufikiria kuwa hayo yote yanaweza kufanywa na mtu ambaye anajua uhalisia kuwa hakuna lolote litafanyiika, watanzania ni waoga, maandamano yataishia mtandaoni.