ila sisi wa misa ya kwanza saa 12 hatujasomewa, sijapendaUnaweza kujiuliza kwanini TEC wakachagua kuusoma waraka wa kupinga kugawa bandari za Tanganyika kwa DPW kwa wiki sita na si pungufu ama zaidi?
Hili limekaa kiroho na kihesabu zaidi.. Dunia inaendeshwa na tarakimu na hesabu kupitia kanuni maarufu ya MAGAZIJUTO (BODIMUS)!
Mara sita inawakilisha siku sita za uumbaji, yaani siku sita za wiki.. Jumatatu mpaka Jumamosi! Kwahiyo ilipaswa waraka usomwe kila siku kwa siku sita mfululizo, lakini wanaosomewa ni waumini na waamini kanisani na siku pekee ya kuweza kuwasomea katika wingi wao ni siku ya ibada ambayo ni Jumapili
Kwahiyo ndio maana zikatengwa Jumapili sita mfululizo za kusomewa waraka husika, na leo hii ni Jumapili ya tatu
Waraka mpaka sasa umeonesha mafanikio makubwa sana! Dondoo zilizoandaliwa kisomi na kwa weledi mkubwa hazikutoka nje ya mstari wa katiba ya taifa
Zimejitokeza taasisi, vikundi na watu binafsi waliojaribu kuukosoa na kuupinga waraka lakini wakashindwa vibaya sana, kwakuwa badala ya kukosoa ama kupinga kilichomo kwenye waraka husika, wao wakaishia kutoa shutuma, kutuhumu na kukejeli watu binafsi, taasisi iliyoandaa waraka, imani ya waandaaji nk
Hawa wote walikuwa na haki kamili ya kufanya hivyo kwa mujibu wa katiba yetu, kakini kuna kila dalili kwamba hawakusukumwa na uzalendo na dhamira njema bali kwa maelekezo maalum na kwa malipo! Mbaya zaidi wakakurupuka sana na kuongea ujinga mtupu kisha haoo wakasepa zao kukinga mikono!
TEC hawakutetereka kwenye hilo na wala hawakuthubutu kunyanyua mdomo kujibizana nao! Walibaki na focus yao kukamilisha ratiba.. Na wanatambua wazi kwamba debe tupu haliishi kutika..!
Waraka wenye manufaa kwa watanganyika wote bila kujali
Itikadi zao
Imani zao
Makabila yao
Kipato chao nk nk unaendelea kusomwa leo kwa mara ya tatu, na ili kukamilisha ratiba bado mara zingine tatu. Wanaotumwa kuujibu kwa malipo wajitahidi kuujibu kwa hoja na si vioja
Watanganyika sio wapumbavu! Tunajitambua!!!!View attachment 2737210