RATIBA: Baada ya Mwanza Kongamano la Katiba Mpya lielekee Ikungi -Singida

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
117,651
218,131
Ikumbukwe kwamba siku ya Jumamosi ya 17/7/2021 lile Kongamano kubwa kabisa la Katiba mpya litafanyika Jijini Mwanza , Tunawashukuru Chadema na wadau wote waliowezesha Makongamano haya kufanikiwa .

Sina haja sana na kongamano hili ambalo halijafanyika bado , Bali ninachotaka kuwaomba viongozi wanaoratibu kongamano hili , baada ya kutoka Mwanza walielekeze Singida , na hasa Wilaya ya Ikungi . Nimetaka liende Ikungi ili tuone huo uchafu alioropoka DC mzigo wa Wilaya hiyo anayeitwa Jerry Muro kama ataweza kuufanya .

Jerry Muro mtu duni aliyeokotwa kutoka Yanga na kupachikwa kwenye Ukuu wa Wilaya kama bakshishi baada ya kumhujumu Yusuph Manji ( sitafafanua ) , ametangaza kwamba ni marufuku kwa mtu yeyote kujadili umuhimu wa katiba mpya kwenye Wilaya anayoongoza , Ukweli ni kwamba Jerry Muro hana mamlaka hayo aliyojipa , na hakuwahi kuwa nayo na wala hatokuja kuwa nayo hadi anaingia kaburini .

Ndio maana tunawaelekeza Chadema kubadili ratiba ya kongamano la Katiba mpya na kulielekeza Ikungi ili tuone hiyo jeuri ya Jerry Muro itakakoishia .

2845513_u765tfc12.png
 
Mda ukifika itakuwa,ila siyo kwa ushauri ulioutoa.kufanya hivyo nisawa nakushindana na mjinga anayetamka ovyoovyo tu.
Muro ukame wa singida unamsumbua
sometimes watu wa namna hii wanapaswa kudhibitiwa mapema kabla hawajaanza ubakaji
 
Hakika kuna kila sababu ya kuwa na Kongamano la Katiba huko Ikungi, kwa kuwa DC Murro, ameonyesha jeuri na vitisho kwenye nchi inayofuata mfumo wa Vyama vingi vya siasa. Mamlaka ya Uteuzi inapaswa kumwagalia na kufuatilia nyendo zake, vinginevyo yatatokea yaliyotokea Wilayani Hai enzi za DC Sabaya.
 
Anaweza akawadhibiti kwa kuwanyima vibali,kwanza Ikungi kumbi ni chache na hivyo mtabaniwa hapo hapo
 
Chadema hawana muda na mambo yanayowagusa wananchi.

Wao wanapambania tu namna wanaweza tawala ,

Wana dai Katiba na tume huru maswala ya Kodi sijui nini hayawahusu
 
Yeyote anaezuia mkusanyiko wa watu wa kutoa maoni yao ni anajifanya kuwa juu ya katiba,na yeyote anaejifanya kuwa yuko juu ya katiba ni Kima aliechangamka🐒🐒🐒

u765tfc12.png
 
Ikumbukwe kwamba siku ya Jumamosi ya 17/7/2021 lile Kongamano kubwa kabisa la Katiba mpya litafanyika Jijini Mwanza , Tunawashukuru Chadema na wadau wote waliowezesha Makongamano haya kufanikiwa .

Sina haja sana na kongamano hili ambalo halijafanyika bado , Bali ninachotaka kuwaomba viongozi wanaoratibu kongamano hili , baada ya kutoka Mwanza walielekeze Singida , na hasa Wilaya ya Ikungi . Nimetaka liende Ikungi ili tuone huo uchafu alioropoka DC mzigo wa Wilaya hiyo anayeitwa Jerry Muro kama ataweza kuufanya .

Jerry Muro mtu duni aliyeokotwa kutoka Yanga na kupachikwa kwenye Ukuu wa Wilaya kama bakshishi baada ya kumhujumu Yusuph Manji ( sitafafanua ) , ametangaza kwamba ni marufuku kwa mtu yeyote kujadili umuhimu wa katiba mpya kwenye Wilaya anayoongoza , Ukweli ni kwamba Jerry Muro hana mamlaka hayo aliyojipa , na hakuwahi kuwa nayo na wala hatokuja kuwa nayo hadi anaingia kaburini .

Ndio maana tunawaelekeza Chadema kubadili ratiba ya kongamano la Katiba mpya na kulielekeza Ikungi ili tuone hiyo jeuri ya Jerry Muro itakakoishia .
Ikungi tunataka maendeleo, Katiba pelekeni huko Kaskazini walipo endelea.
 
Hao ma DC hizo nguvu za kutoa matamko yanayopingana na sheria wanazitoa wapi? na kwanini hawalalamikiwi na mamlaka yao ya uteuzi au tuseme wameagizwa kutamka hayo?
 
Ikumbukwe kwamba siku ya Jumamosi ya 17/7/2021 lile Kongamano kubwa kabisa la Katiba mpya litafanyika Jijini Mwanza , Tunawashukuru Chadema na wadau wote waliowezesha Makongamano haya kufanikiwa .

Sina haja sana na kongamano hili ambalo halijafanyika bado , Bali ninachotaka kuwaomba viongozi wanaoratibu kongamano hili , baada ya kutoka Mwanza walielekeze Singida , na hasa Wilaya ya Ikungi . Nimetaka liende Ikungi ili tuone huo uchafu alioropoka DC mzigo wa Wilaya hiyo anayeitwa Jerry Muro kama ataweza kuufanya .

Jerry Muro mtu duni aliyeokotwa kutoka Yanga na kupachikwa kwenye Ukuu wa Wilaya kama bakshishi baada ya kumhujumu Yusuph Manji ( sitafafanua ) , ametangaza kwamba ni marufuku kwa mtu yeyote kujadili umuhimu wa katiba mpya kwenye Wilaya anayoongoza , Ukweli ni kwamba Jerry Muro hana mamlaka hayo aliyojipa , na hakuwahi kuwa nayo na wala hatokuja kuwa nayo hadi anaingia kaburini .

Ndio maana tunawaelekeza Chadema kubadili ratiba ya kongamano la Katiba mpya na kulielekeza Ikungi ili tuone hiyo jeuri ya Jerry Muro itakakoishia .

View attachment 1856101

La ikungu litapendeza kulihudhuria.

Hawa mabwana ifike mahali tuwataarifu kwa vitendo kuwa tumewachoka.
 
..kongamano likienda Ikungi focus itakuwa malumbano na dc muro.

..dc muro anataka watu waanze kumjadili yeye badala ya kuelimisha na kuhamasishana kuhusu katiba mpya.

..suala la katiba mpya linahitaji FOCUS ya hali ya juu.
 
Chadema hawana muda na mambo yanayowagusa wananchi.

Wao wanapambania tu namna wanaweza tawala ,

Wana dai Katiba na tume huru maswala ya Kodi sijui nini hayawahusu
Lini mlihitaji msaasa wa chadema imeanza lini?? 🤣🤣🤣Mama anaupiga mwingi. Kila mtu ashinde mechi zake
 
Jaji Mfawidhi na mwanaharakati huru na pia M-Tanganyika mwenye asili ya Singida.

Nilishakuita majina mabaya sana na umedhihirisha hilo tena hapa. Eti “mwanaharakati” - hizo harakati zako huru unazifanyia wapi kama unazuia na wengine wenye zao wasizifanye?? Eti “mtanganyika”. Hutaki muungano? Na umeruhusiwa hapa kujiita hivo na maoni yako yanasikilizwa!! Sasa unasema unasema wasije Ikungi, unawachagulia sehemu na kitu cha kufanya! Huo sio uhuru - subirini wavunje sheria!! Tope katika fuvu!!
 
Back
Top Bottom