Katiba i copy sheria ya CHINA juu ya rushwa
Uko sahihi lakini kumbuka tunatengeneza kitu cha kudumu kwa miaka mingi ijayo! Kwa hiyo kuna uwezekano mkubwa sana ku-reform na ku-restructure taasisi hii na ikaweza kutekeleza kazi zake kwa ufanisi!Hao walioko kwenye TAKUKURU kwa sasa, hawana moral standing ya kutetea uwepo wa chombo chao kikatiba. Kwa kukubali kusafisha wapokea rushwa wakubwa serikalini, wamethibitisha hawafai. Tutawasikilizaje watu kama hao? Waache wakose kazi.
​Ndiyo sababu tunataka iwe ndani ya katiba mpya ili kuepuka kuwa chombo cha kulinda chama tawala!
Kama suala la chombo cha kupambana na rushwa Katiba iko kimya, basi tume ya Warioba haikusikiliza maoni yetu; mimi nilitoa maoni juu ya rushwa na kutaka chombo huru cha kupambana na ufisadi kitachowajibika kwa Bunge.
Hizi idara zingine bwana tabu tuu!! Kwanza ajira zake haziko clear
Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
Hii inakuwa kama ni Mchezo wa kuigiza maana aliye propose kuanzashwa kwa PCB ilikuwa ni tume ya WARIOBA aliyependekeza Katiba ni yeye na kuisahau TAKUKURU ni tume iliyoongozwa na WARIOBA.Sijua kama viongozi wa Serikali ya Shirikisho watachunguzwa na chombo kipi kama suala la Rushwa halijawekewa msisitizo katika katiba ya Jamhuri sijui katiba za Washirika wa Muungano zitakuwaje na ni nani au chumbo kipi kitakuwa na mamlaka ya kufuatilia Rushwa katika Serikali ya Muungano