Mzee Murangira,
Hakuna la kuongeza, ninajiuliza one question watu wenye busara kama wewe mlikuwa wapi siku zote, na ubarikiwe bro!
CV ya RO kama ni muhimu at this point inapaswa kuletwa na wale wanaompalilia, mimi siwezi kuitafuta hiyo CV kwa sababu sikuja hapa kumtetea na kumpalilia tuuu kama kipofu, sasa tunampalliaaje mtu ambaye hata CV yake hatuna? Badala yake tunadai hatuna CV, lakini kila siku tunaitoa hiyo hiyo CV kwa ujanja na kuigeuza geuza, wakati watu wenye akili hapa tumeshajua kuwa mnayo ila tu mnachagua ya kuweka hapa,
Tunaangalia mambo na objectivity, ndio maana ninasema so far mmeniongezea 15%, jumla imekuwa 25%, in the last three days nimeingia uvunguni na kumfukua kikamilifu huyo mzee RO, tena kwa undani sana ninasema tuliyosema yametosha na sitaongeza tena, tumesema ya kutosha sasa kama RO ni mtu mwenye busara ni wakati wa kuyarekebisha mabovu na kuongeza mazuri,
ajifunze kuwa hapo alipoingia ni taifa sio London tena na mambo ya Papaaa na Njenje, maisha na usalama wa kuanzia raia, mpaka viongozi wetu yamo mikononi mwake, JK hawezi kufanya yote yaani urais na usalama, HAPANA! Tuchape kazi na tuache unafiki, tunajua kuwa kuna viongozi ambao tukiwa kwenye uchaguzi walikuwa ni sumu ya Mtandao, lakini sasa uchaguzi umeisha tunaangalia mbele na kuwa taifa moja,
Waandishi wetu wameenda likizo, tunayoyafanya hapa yalitakiwa kufanywa na magazeti yetu na redio, pamoja na TV, sasa kwa sababu wamesafiri wananchi tumeamua kuchukua hili jukumu sisi wenyewe mikononi mwetu, hatuwezi kunyamazishwa hata watumwe watu mia moja humu kutuhadaaa, we are not sleeping, tutaendele a kuja hapa na majina yetu ya bandia na kuuliza tusipoelewa, na tutawauliza viongozi wakubwa sio wadogo!
Tumechoka kuchezewa, kuonewa na kunyonywa, na wengine bado wanajaribu kuja hapa kutunyanyasa, tunasema ENOUGH! Fanyeni kazi tutawapa heshima kwa kazi yenu kwa wananchi, lakini sio kuwanunua waandishi na kututumia watu wenu hapa kutuhadaa na maneno mengi ya ulaghai, na tutaendelea kuwachimba ili kuhakikisha kuwa mnafuata sheria kama mnavyotaka sisi tuzifuate yaani wananchi,
Mambo yenu yote tunayaona tena waziiii, nafikiri na nyinyi wenyewe mmeona hapa tunavyomwaga ukweli, manapeleka watoto wenu hukoooo tunawaona, wengine mnawadai wahindi rushwa tunawaona na tuna-record kila kitu, hizi porojo hapa hazizuiii kitu chochote, tunawaangalia kwa macho mawili,
Mzee RO, ninasema tena kuwa Kombe aliwafikisha mahali wazee wa huko usalama wakawa wanasafiri na viongozi bila per-diem, wakati yeye anaenda London na dola laki tatu-mpaka nne, M16 wakaingia hotelini mwake akiwa hayupo na kuzikuta na kuwafahamisha wakubwa wetu na kuzirudisha bongo, wananchi wakashitaki kwa wakubwa mwisho wakachoka, maana walikuwa wanakula naye kwa hiyo jibu likawa "....wananchi tutachunguza....", wananchi wakaamua kuchukua sheria mikononi mwao, Boom! Boom! Boom, Bang! mchezo ukaisha,
wewe ni kijana tena mtoto wa mjini sasa fanya mambo tofauti, na huyu Mzee wetu JK lazima uwe mkali naye na hasa hawa marafiki zake, kisheria wewe huchukui amri kutoka kwake, alipokuapisha tu alikabidhi usalama wake na familia yake na serikali nzima mikononi mwako, kwa hiyo mchezo uishe tunataka mabadiliko na maendeleo,
Sisi wananchi ni wepesi sana kusahau ya nyuma, kama ya sasa yanakubalika!