Rangi za moshi hutokeaje baada ya Papa (Pope) mpya kuchaguliwa?

Rangi za moshi hutokeaje baada ya Papa (Pope) mpya kuchaguliwa?

The Dictator

JF-Expert Member
Joined
Jul 20, 2018
Posts
4,426
Reaction score
12,161
Vatikan huweka kemikali ya inayotoa moshi mweupe au mweusi wakati wa kuchoma karatasi za kura katika uchaguzi wa Papa mpya. Mfano:

MOSHI MWEUSI (ishara kwamba hakuna Papa mpya amechaguliwa bado) hutokana na kuchoma karatasi za kura zilizochanganywa na kemikali kama perchlorate, potassium nitrate, na anthracene
images (3).jpeg



MOSHI MWEUPE (ishara kwamba Papa mpya amechaguliwa) hutengenezwa kwa kuchoma karatasi za kura pamoja na kemikali kama Lactose, Chlorate, Na Pine Rosin au mchanganyiko mwingine unaotoa moshi mweupe kabisa.
images (2).jpeg


Huchoma karatasi zote kwa pamoja (si moja moja) baada ya kila raundi ya upigaji kura. Mchakato huu hufanywa kwenye jiko maalum (stove) lililo ndani ya Sistine Chapel, ambalo limeundwa kuchoma karatasi hizo pamoja na mchanganyiko wa kemikali unaotegemea matokeo ya kura.

Soma Pia: Papa Francis amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 88


Hivi ndivyo hufanyika:

Kila baada ya raundi ya kura (mara mbili asubuhi, mara mbili jioni), makadinali hukusanya na kuweka karatasi zote za kura kwenye jiko hilo.

Kama hakuna aliyechaguliwa kuwa Papa (yaani kama hakuna aliyevuka theluthi mbili ya kura), wataongeza kemikali za kutoa moshi mweusi kabla ya kuwasha moto.

Kama Papa amepatikana, wataongeza kemikali za kutoa moshi mweupe.


Kiasi cha kemikali kinapimwa ili kuhakikisha rangi ya moshi inaonekana wazi kwa watu wanaosubiri nje ya kanisa.

Mfumo huu wa kuchoma karatasi zote kwa pamoja kwa kutumia kemikali maalum husaidia kutoa ishara moja kwa moja kwa umma bila mkanganyiko.

Njia hii imekuwa ikifanyika tangu mwaka 1963.
 
Ni hatari sana. Kwa nini wasitangaze matokeo kwa maneno pasi na kuwasha mimoshi kuchafua mazingira?
Moshi unaonekana hata ukiwa mbali. Sasa chukulia miaka hiyo ya 60 kabla teknolojia haijakua kiasi ilivyo leo. Wangeweza kufanya hivyo ila ingechukua muda gani taarifa kusambaa?
 
Ni hatari sana. Kwa nini wasitangaze matokeo kwa maneno pasi na kuwasha mimoshi kuchafua mazingira?
Mkuranga mikaa inachomwa, moshi wa kupata gunia moja ni sawa na moshi wa kuchagua Papa mara 10
 
Back
Top Bottom