Ramani, makadirio, Elimu na ushauri kuhusu Ujenzi

Siku hizi wanatumia zile single nazo zinaivo vipimo?
Ndio ndg, hapo nilikuwa nazungumzia single wire, twin wire sana sana inatumika kwenye surface wiring (waya unakuwa unalazwa kwenye ukuta na kubanwa na clamp) lakini kama waya zinapita kwenye conduit, basi tunatumua single wire.
Kwenye picha hapo, ni single wire na hiyo 1.5mm² ndio size ya wire
20250718_203114.jpg
 
Naona Fensi kuna stail ya kuweka nguzo ya tofali. yaan baada ya meter kazaa tofali mbili zinawekwa kwa mfumo wa kwenda ndan hii imekaaje
 
Safari ya ujenzi ni ndefu, kuna vipengele vingi mpaka nyumba inakuja kukamilika. Nunua ramani kwa mtu ambaye baadae utaweza tena kumtafuta na kumuomba ushauri bila kukuchaji gharama za ziada.

Ramani, Makadirio au Ushauri tuwasiliane
 
Pia haina shida, ni moja ya mbinu za kupunguza gharama lakini kiubora siku zote tofali haiwezi ikaizidi zege
mfano sehemu ya meters 35 unaweza ukaweka za zege 3 then za tofali kunakobaki? yaan kwenye kona inakaa ya zege alaf zinazofata mbili za tofali then zege.. hivo mpaka mwisho
 
Unaweza ukafanya hivyo pia, yote ni katika kupunguza gharama. Ila nguzo zinazobeba geti la kuingilia ni vizuri zikawa ni nguzo za zege
 
haka kasentensi umekaandika kwa uchungu [emoji1787][emoji1787]
[emoji846][emoji846] kwenye ujenzi hata Tsh 500 inabidi tuiheshimu sana, maana Tsh 500 mara 1000 tayari inakuwa ni nusu milioni. Wapo watu wanaoishia njiani japo kuwa matarajio yao ilikuwa wamalize na kuhamia ili wakimbie kodi lakini imeshindikana.
 
1. Kabla ya kumwaga zege katika nguzo zako, hakikisha box zako za nguzo ziko wima pande zote mbili (kusini kuelekea kaskazini, na mashariki kuelekea magharibi). Ukiangalia upande mmoja tu, itakupoteza na matokeo yake ndio kama inavyoonekana kwenye picha

2. Hakikisha umepigilia vizuri support za kushika box zako ili katika purukushani za kumimina zege juu ya box zisiweze kuhamisha box zako na kufanya nguzo ziiname.

Ramani, Makadirio au Ushauri tuwasiliane. Una site yako mahali na unahitaji kutembelewa kwa lengo la kuangalia marekebisho pia usisite kunitafuta.
20250725_153146.jpg
 
Jana nìpo zangu duka la vifaa vya umeme kuulizia kifaa flani, mara akaja jamaa mmoja akawa anaulizia kifaa cha kucontrol taa zijiwashe na kujizima zenyewe pindi giza linapoingia (Photocell).

Muuzaji akamuambia yule jamaa kwamba hicho kifaa kipo bei yake 50,000/=, jamaa akatoa pesa akalipia then akaondoka zake. Nilimuangalia yule muuzaji mara mbili mbili (bila yeye kuniona), wakati huo nasubiri wanitafutie kifaa changu niondoke

Hivi ndivyo maboss wengi wanavyopigwa huko hardware kwa kutojua bei halisi, bei aliyolipia jamaa ni zaidi ya mara 3 ya bei halisi na hii yote ni kwa sababu ya kutojua. Wauzaji wengi wa hardware sio wamiliki wa hizo hardware, wengi wameajiriwa kwa hivyo kwa situation kama hii muuzaji anaweka pesa ya boss pembeni (bei halisi), iliyobaki yote ni ya kwake.

Hakikisha kabla hujaenda mahali kununua kitu, uwe tayari unajua bei yake halisi maana wauzaji huwa wanataja bei kulingana na muonekano wa mtu jinsi ulivyo (wakiona umenawiri nawiri ndio wanakupiga vizuri zaidi, lakini wakiona hueleweki eleweki wanatakujia bei ya kawaida maana wanajua wakikutajia bei ya juu utakimbia)

Ni kweli kabisa bei yake kawaida huwa shingap
 
Safari ya ujenzi ni ndefu, kuna vipengele vingi mpaka nyumba inakuja kukamilika. Nunua ramani kwa mtu ambaye baadae utaweza tena kumtafuta na kumuomba ushauri bila kukuchaji gharama za ziada.

Ramani, Makadirio au Ushauri tuwasiliane
Mil 25 napaua nyumba ya two bedroom?
 
[emoji846][emoji846] kwenye ujenzi hata Tsh 500 inabidi tuiheshimu sana, maana Tsh 500 mara 1000 tayari inakuwa ni nusu milioni. Wapo watu wanaoishia njiani japo kuwa matarajio yao ilikuwa wamalize na kuhamia ili wakimbie kodi lakini imeshindikana.
Vipi gharama zako za kusimamia mjengo?
 
Mil 25 napaua nyumba ya two bedroom?
Kwa nyumba ya two bedrooms, milioni 25 itakuvusha kwenye hiyo hatua ya upauaji. Kama kuisha, itaisha hatua za mwishoni mwishoni kutegemeana na nyumba yenyewe jinsi ilivyo (ukubwa) na aina ya finishing utakayoamua kutumia
 
Back
Top Bottom