Ramani, makadirio, Elimu na ushauri kuhusu Ujenzi

Hechy Essy Naomba muongozo wa wataalam.
Kati ya tofali za udongo za kuchoma na hizi za block (cement+mchanga) ni zipi imara zaidi? Na endapo unajengea tofali za udongo za kuchoma ni vyema kutumia cement ama tope la udongo?
Tofali za udongo ni imara zaidi ukilinganisha na tofali za mchanga na cement. Hii inategemea pia na namna hizo tofali zilivyotengenezwa.
Ikumbukwe pia katika utengenezaji wa cement, moja ya malighafi zilizotumika ni pamoja na udongo (clay)
 
Kabla ya kupandisha kuta za boma, hakikisha unajaza kwanza kifusi kwenye msingi. Kwanini? Ukijenga kuta za boma kabla ya kujaza kifusi, maana yake kuna sehemu zingine hutoweza kurusha kifusi ukiwa nje ya nyumba hivyo itamlazimu mtu anayejaza kifusi asombelee kifusi kwa ndoo kutoka nje na kuingia nacho ndani

Katika ujenzi ukiruka step moja wapo au ukabadilisha mtiririko wa kazi, huko mbele kuna uwezekano mkubwa ukaingia gharama zaidi
ni wakati gani sahihi wa kumwaga jamvi..?nimeshaanza kupandisha tofali juu ya lenta,kinachonikera ni mimea kuota ndani
 
Muda sahihi wa kumwaga jamvi ni baada ya kumaliza kujenga kuta za msingi.
Baada ya kumaliza kujenga kuta za msingi, unajaza kifusi, unasuka nondo za mkanda pamoja na kupanga mawe juu ya kifusi, unafunga box kuzunguka nyumba kisha unamwaga zege katika eneo lote la nyumba. Hii itafanya kazi ya jamvi kuwa nyepesi zaidi tofauti na kumwaga zege baada ya kupandisha boma.

Hapo kwa kesi yako, maliza kwanza kupaua ndipo uweke hiyo rough floor
 
asante,kuna changamoto nikifanya hili zoezi sasa(kabla ya kupaua)?,ukizingatia upauaji unahitaji hela yote kwa pamoja,hofu yangu ni kukaa muda mrefu na ndani kuota mimea
 
Mimea kuota ni kawaida ndg, hiyo inaonesha kwamba kifusi chako kina plant nutrients zinazosupport ukuaji wa mimea.
Kitu cha kuzingatia wakati wa kumwaga rough floor yako ni kung'oa mimea yote na kukwangua tabaka la juu kuhakikisha na mizizi yote inatolewa, kushindilia vizuri na Compactor, kujaza mchanga na kumwagia maji ili kutenganisha udongo na zege kisha ndipo utamalizia na kumwaga zege
 
Grid lines katika ramani ni muhimu sana hivyo hata kama utachorewa na mchoraji mwingine, msisitize aweke hizo grid lines kama inavyoonekana kwenye picha ili kurahisisha zoezi la kuset msingi. Pia vipimo viwe vinaonekana vizuri bila kuingiliana digits
IMG-20250514-WA0010.jpg
 
Muda sahihi wa kumwaga jamvi ni baada ya kumaliza kujenga kuta za msingi.
Baada ya kumaliza kujenga kuta za msingi, unajaza kifusi, unasuka nondo za mkanda pamoja na kupanga mawe juu ya kifusi, unafunga box kuzunguka nyumba kisha unamwaga zege katika eneo lote la nyumba. Hii itafanya kazi ya jamvi kuwa nyepesi zaidi tofauti na kumwaga zege baada ya kupandisha boma.

Hapo kwa kesi yako, maliza kwanza kupaua ndipo uweke hiyo rough floor
Na vipi kama ukitaka kuweka lile DPM gumu, unaliweka juu ama chini ya nini kabla ya kumwaga jamvi?.
 
Kabla ya kupandisha kuta za boma, hakikisha unajaza kwanza kifusi kwenye msingi. Kwanini? Ukijenga kuta za boma kabla ya kujaza kifusi, maana yake kuna sehemu zingine hutoweza kurusha kifusi ukiwa nje ya nyumba hivyo itamlazimu mtu anayejaza kifusi asombelee kifusi kwa ndoo kutoka nje na kuingia nacho ndani

Katika ujenzi ukiruka step moja wapo au ukabadilisha mtiririko wa kazi, huko mbele kuna uwezekano mkubwa ukaingia gharama zaidi
Na kifusi kinajazwa baada ya muda gani baada ya kumaliza ujenzi wa msingi? As in niache muda gani mpaka tofali za msingi zimewe zimeshikana vizuri?

Na je, baada ya kifusi nilazima kupanga mawe kabla ya kumwaga jamvi kwa nyumba ya kawaida ambayo sio ghorofa?
 
Mawe ni muhimu lakini kwa hizi nyumba za kawaida haina ulazima sana, ni optional (ukiweka sawa, usipoweka sawa)

Kifusi unajaza baada ya msingi kukomaa vizuri, almost baada ya siku 7 na kuendelea
 
Kitchen verandah tayari inanguzo 2(1.3*2.25)mtrs,mpango ni kuweka slab juu kwa kuextend kidogo ili walau tank la 2m3 likae.
Nimeambiwa hitaji
Nondo 12mm (5pcs)
'Mirunda 18ft(9pcs)
Cement 5no
Misumari 4"~2kg
Binding wire 1no
Mchanga mweusi(upo tayari)
Labour 180K
ukitoa mchanga ambao upo tayari,gharama za material kwa huku hazifiki 300K,
kwa uzoefu wako,hiyo labour charge iko fair?
cc Hechy Essy
 
Labour charge inategemea na vitu vingi ndg, wakati mwingine unakuta fundi mpaka afike site tu anaweza akatumia nauli zaidi ya Tsh 5000 (kama wapo wanne maana yake nauli tu wanatumia 20,000/=, hapo bado chakula) kwahivyo analazimika ataje bei ya juu ili kufidia hizo gharama

Kama ndio bei ya kwanza amekutajia, bado una nafasi ya kubargain nae ikawa chini ya hapo maana hiyo ni kazi ya siku moja tu, fundi mmoja na vibarua wake watatu wanatosha
 
Katika zoezi la upachikaji wa switch box katika kuta, kama kuna switch box zaidi ya moja na zipo karibu karibu basi acha nafasi ya angalau nchi moja kati ya box moja na box lingine vinginevyo itakuwa ngumu kufunga switch/socket katika hizo box hivyo itamlazimu fundi atindue hizo box na kuziset upya.

Ramani, Makadirio au Ushauri tuwasiliane
 
DPM unaweka kabla ya kumwaga jamvi, ila DPC unaweka wakati wa kuinua kuta za boma (juu ya mkanda wa msingi)
Na kwa upande wa sehemu ya kuwekea choo cha kuchuchumaa, hiyo DPM inachanwa ama inawekwa vipi?.

Kuna ulazima wa kuweka DPC ikiwa umeweka DPM, na kwa upande mwingine, DPC inazuia vipi unyevu usipande juu kwa kupitia kwenye plasta?.
 
Hapana, hauichani. Kadiria kina cha uwazi utakaouacha kwa ajili ya sink, wakati wa kutandika DPM yako, DPM itaingia chini kwenye huo uwazi bila ya kuichana. Hakikisha unaweka kingo katika huo uwazi ili utakapomwaga zege, zege isizibe hiyo sehemu vinginevyo utakuja kupata shida ya kutindua zege baadae ambapo inaweza kusababisha nyufa katika hiyo jamvi
 
Back
Top Bottom