Ramadhan Special Thread

Assalaam Alaykum

Ndugu zangu Waislam
Allah awabaarik sana popote mlipo


TANBIH FUPI
Mwezi huu wa Rajab,ni Katika Miezi Mitukufu
Ila Baadhi ya Watu wanaojiita ni Masheikh,Wanawafundisha Watu na kuwasisitiza kuhusu kufanya Ibada mbalimbali katika miongoni mwa Ibada za Sunna

Jambo ambalo si sahihi kisheria
Hakuna Ibada Maalum ndani ya mwezi huu(Rajab),ambayo Mtume wa Allah Sala na Salamu ziwe juu yake ametufundisha

Bali
Ibada nyingi watu wamezua ndani ya Mwezi huu

Kuna Watu
Wanafanya Umra ndani ya mwezi huu(Rajab)Wakidhani kufanya hivi,wanapata Ujira zaidi

Kuna Watu
Wanaswali swala maalum( صلاة الرغائب)ambayo haina asili katika Dini yetu

Kuna watu
Wanafanya Ibada maalum usiku wa Nusu Rajab( صلاة النصف من رجب ),Hili nalo halina asili katika Sheria yetu tukufu

Kuna Watu
Wanaswali tarehe 27,na kusema ndio siku ya Miiraaj( صلاة ليلة المعراج ),Hili nalo halipo katika Dini

Kiujumla
Meengi yamezushwa na Watu kwa ujinga au kwalengo ambalo wao wanajua zaidi

Ikhwah
Tuwe makini sana ndani ya Miezi hii
Tusomeni Dini yetu,ili tujue yaliyosahihi kisheria

Shukran sana
جزاكم الله خيرا

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ubarikiwe
 
Funga haikubaliki bwa somo.

Ukiwa hausali funga yako haikubaliki.

Na hii ndio kauli yenye nguvu katika hoja.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Shahada inayokusudiwa ni kumpwekesha Allah na sio kutamka tu,mana kama kutamka tu basi hata mkristo aanaweza kutamka na bado akawa anaenda kanisani,itamfaa shahada..?

Kwa hyo shahada ni kuacha shriki na kumuabudu Allah pekee.

Kama funga na sala ni tofauti basi pia shahada na sala ni tofauti

Yaani mtu akisali sala yake inakubaliwa hata kama hajjatamka shahada ?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…