Ramadhan Special Thread

Kwa wenye matatizo ya kiafya au walio safarini wameruhusiwa kula ila matatizo yao yatakapoondoka wanatakiwa walipe funga zao. Je wewe ulieuliza hili swali utafunga?!

Ndio niataman kufunga, sema nahofia matatizo yangu kiafya!!
Ndio nikawa najiuliza ikiwa nahofia matatizo yangu kucharuka nikifunga natakiwa nifanyeje. Nasikia eti kuna kutoa fidia kwa masikini, yatima ni kweli??
 
Kuna matatizo ya aina mbili kiafya

Kuna tatizo,lenye kuondoka
Mfano
Malaria nk

Hili,
Unaruhusiwa kula mchana,kisha baada ya Ramadhan kwisha,utakuja kulipa funga ulizoziacha

TATIZO LA PILI
Ni Ugonjwa wa Kudumu,usiotibika au kuondoka(Labda kwa Qudra za Allah tu),Na Madaktari wakathibitisha hili
Huyu,
atatakiwa kulipa Kibaba kila siku katika masiku ya Ramadhan

Allah anajua zaidi
 
Ikiwa mtu ana tatizo la kiafya,na Madaktari wamethibitisha kuwa hawezi kufunga

Basi
Sheria itamtaka atoe Kibaba,
Yaani Kilo Moja na Nusu ya Chakula(Kipendwacho hapo mji anamoishi)
Kwa kumpa Maskini kila siku ndani ya Mwezi wa Ramadhan

Allah akufanyie wepesi popote ulipo,na akuondolee kila aina ya tatizo

Kaka, asante. Na kuna vigezo vyovyote katika mtu (huyo masikini) anaetakiwa kupewa?
Je ni lazima awe muislamu, awe anafunga, je akiwa hafungi ama sio muislamu??

Je ikiwa naona kazi kuwatafuta masikini (mid sio mwenyeji sana mtaa ninaoishi sasa hivi) nina haki ya kumpa mtu yeyote nayeona ni masikini ama niende msikiti wa jirani niwe nakabidhi mzigo naondoka wao watajua wa kumpa!!!
 
Maskini Bora ni yule mwenye kumtambua Mola wake,na akashikamana na yale aliyoamrishwa na kuachana na yale aliyokatazwa,Huyu ni Bora kupewa

Ama kinyume na hivyo
Hakuna tatizo kumpa sadaka au kafara yako,na kama una nafasi,mpe nasaha juu ya Mola wake

Unahaki ya kumpa Yeyote unaemuona ww Maskini,ila awe maskini kwamaana yake kamili

Na kama utashindwa kutokana na ugeni au muda
Unaweza kumpa mtu unaemuamini,ili akutafutie maskini na amkabidhi Kafara au sadaka yako

Na si mbaya
Hata kama utapeleka Msikitini kwa lengo la Kafara au Sadaka
 
Kaka, asante. Na kuna vigezo vyovyote katika mtu (huyo masikini) anaetakiwa kupewa?
Je ni lazima awe muislamu, awe anafunga, je akiwa hafungi ama sio muislamu??

Je ikiwa naona kazi kuwatafuta masikini (mid sio mwenyeji sana mtaa ninaoishi sasa hivi) nina haki ya kumpa mtu yeyote nayeona ni masikini ama niende msikiti wa jirani niwe nakabidhi mzigo naondoka wao watajua wa kumpa!!!
Huu uungwana nimeupenda sana tunaylizana kwa heshima na adabu kwa lengo la kujifunza.

Mola akubariki dada yangu.
 
HII NDIO SWAUM YA SAWASAWA

Amesema Mtume wa Allah swallah Allah alaih wasalam

ليس الصِّيامُ من الطَّعامِ والشَّرابِ

Si mwenye kufunga ( kwa kujizuia tu) kutokana na kula na kunywa

إنَّما الصِّيامُ من اللَّغوِ والرَّفثِ

*Hakika Funga ( ya sawasawa) ni kujizuia kutokana na Upuuzi na madhambi*

فإن سابَّكَ أحدٌ أو جهِلَ عليكَ فقل إنِّي صائمٌ إنِّي صائمٌ.

basi ikiwa atakutusi (atakutukana) yeyote au kukufanyia jambo la kijinga basi sema : *HAKIKA MIMI NI MWENYE KUFUNGA*

Hadith imepokewa na imaam Ibn Hibbaan na Haakim


Nimesema:

Upuuzi : *Ni kila kauli au matendo ambayo hayana manufaa ,si katika akili wala katika mwili*

Kila kauli au matendo ambayo hayaongezi Utambuzi katika akili wala hayaongezi chochote katika mwili ni Upuuzi

Hivyo mwenye kufunga anatakiwa kujiweka mbali na michezo isiyo na faida katika akili wala mwili kama vile KUCHEZA GAMES katika Simu au Kompyuta yake , michezo kama vile DRAFT , KERAM , KARATA, KUSIKILIZA MIZIKI, KUANGALIA MOVIES AU SERIES , KUTOKUWA NA STARA, KUWA FARAGHA NA WANAWAKE AJINABI,UONGO nk katika hali ya kufunga kwake,
Hivyo vyote hupunguza ujira wa funga

*Na kila Upuuzi na madhambi yanapokithiri hupelekea kupungua kwa thawabu na kumalizika kabisa thawabu*

Na inaweza kupelekea hali aliyoieleza Mtume wa Allah swallah Allah alaih wasalam:

رُبَّ صَائِمٍ لَيْسَ لَهُ مِنْ صِيَامِهِ إِلا الْجُوعُ

*Huenda mwenye kufunga hana katika funga yake isipokuwa (kushinda na) Njaa*
*Watu tusome Quraan kwa Wingi*

Mfasiri: Abuu Fat'hiyya Khamisi Kiza (Allah amuhifadhi), Dodoma Tanzania

*Usibadili Chochote*
 
HII NDIO SWAUM YA SAWASAWA

Amesema Mtume wa Allah swallah Allah alaih wasalam

ليس الصِّيامُ من الطَّعامِ والشَّرابِ

Si mwenye kufunga ( kwa kujizuia tu) kutokana na kula na kunywa

إنَّما الصِّيامُ من اللَّغوِ والرَّفثِ

*Hakika Funga ( ya sawasawa) ni kujizuia kutokana na Upuuzi na madhambi*

فإن سابَّكَ أحدٌ أو جهِلَ عليكَ فقل إنِّي صائمٌ إنِّي صائمٌ.

basi ikiwa atakutusi (atakutukana) yeyote au kukufanyia jambo la kijinga basi sema : *HAKIKA MIMI NI MWENYE KUFUNGA*

Hadith imepokewa na imaam Ibn Hibbaan na Haakim


Nimesema:

Upuuzi : *Ni kila kauli au matendo ambayo hayana manufaa ,si katika akili wala katika mwili*

Kila kauli au matendo ambayo hayaongezi Utambuzi katika akili wala hayaongezi chochote katika mwili ni Upuuzi

Hivyo mwenye kufunga anatakiwa kujiweka mbali na michezo isiyo na faida katika akili wala mwili kama vile KUCHEZA GAMES katika Simu au Kompyuta yake , michezo kama vile DRAFT , KERAM , KARATA, KUSIKILIZA MIZIKI, KUANGALIA MOVIES AU SERIES , KUTOKUWA NA STARA, KUWA FARAGHA NA WANAWAKE AJINABI,UONGO nk katika hali ya kufunga kwake,
Hivyo vyote hupunguza ujira wa funga

*Na kila Upuuzi na madhambi yanapokithiri hupelekea kupungua kwa thawabu na kumalizika kabisa thawabu*

Na inaweza kupelekea hali aliyoieleza Mtume wa Allah swallah Allah alaih wasalam:

رُبَّ صَائِمٍ لَيْسَ لَهُ مِنْ صِيَامِهِ إِلا الْجُوعُ

*Huenda mwenye kufunga hana katika funga yake isipokuwa (kushinda na) Njaa*
*Watu tusome Quraan kwa Wingi*

Mfasiri: Abuu Fat'hiyya Khamisi Kiza (Allah amuhifadhi), Dodoma Tanzania

*Usibadili Chochote*
Mkuu kwa nini nisibadili chochote?
 
*•══༻◉••﷽••◉༺══•* *●▬▬▬ஜ۩۞۩ஜ▬▬▬●*

*🌙LEO KATIKA FUNGA🌙*
*{ 1 }*



*Allah ﷻ Anasema:*

*{يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا كُتِبَ عَلَيْكُمُ الصِّيَامُ كَمَا كُتِبَ عَلَى الَّذِينَ مِنْ قَبْلِكُمْ لَعَلَّكُمْ تَتَّقُونَ}*
*Enyi mlio amini! Mmeandikiwa Saumu, kama waliyo andikiwa walio kuwa kabla yenu ili mpate kuchamngu.* (2:183)
==================

*TUNAMSHUKURU ALLAH MTUKUFU KUTJAALIA KUFIKIWA NA MWEZI HUU WA RAMADHANI, HII NI NEEMA KUBWA KUTOKANA NA WENGI MIONGONI MWETU HAWAPO TENA HAPA DUNIANI, NA WENGINE WAPO LAKINI NI WAGONJWA.*

*ALLAH AWASAMEHE NDUGU ZETU WALIYOTANGULI MBELE YA HAQQI, NA AWAPONYE WAGONJWA WETU, PIA ATAQABBAL FUNGA ZETU. AAMIN YAA RABBAL AALAMIN.*

*🔁 TUINGIE KATIKA DARSA YETU FUPI KABISA INAYO HUSU FUNGA:*

*IBADA YA FUNGA NI IBADA ADHIMU KABISA MIONGONI MWA IBADA.*
*HIVO KUNA BAADHI YA MAMBO YATUPASA KWANZA TUYAFAHAMU.*

*♦ KWANZA KABISA.*

*١- كم مرَّةً ذكر الصيام في القرآن الكريم؟*
*1- MARA NGAPI IMETAJWA FUNGA NDANI YA QUR'ANI?*

*🔷 JAWABU LAKE.*

*ذكر الله الصيام في القرآن الكريم أربع عشرة مرَّة، سبْع مرَّات في سورة البقرة وحدها، ومرَّة في سورة النِّساء، ومرَّتين في سورة المائدة، ومرَّة في سورة مريم، ومرَّتين في سورة الأحزاب، ومرَّة في سورة المجَادَلة.*

*ALLAH ATAKUAFU AMEITAJA IBADA YA FUNGA NDANI YA QUR'ANI MARA 14.*
*MARA SABA KATIKA SURATUL BAQARA PEKEE, NA MARAMOJA KATIKA SURATU NISAA, MARAMOJA KATIKA SURATUL MAAIDAH, MARAMOJA TENA KATIKA SURATU MARYAM, NA MARAMOJA KATIKA SURATUL MUJAADALAH AU MUJADILAH.*

*♦ JAMABO LA PILI.*

*TUFAHAMU KWA UFUPI NENO RAMADHANI.*
*(رمضان )*
*Neno Ramadhani limejengwa kwa herufi 5 ambazo ni hizi zifuatazo.*

*♢ الراء ، والميم ، والضاد، واﻷلف، والنون.*
*1-Raau. 2-Miimu, 3- Dhadu, 4-Alifu, 5-Nuuni.*

*Baadhi ya wanachuni wamelitafsiri neno hili kwa tafsiri mbalimbali.*

*KWA UFUPI.*

*♢ ﻗﻴﻞ ﺇﻧﻤﺎ ﺳﻤﻲ ﺭﻣﻀﺎﻥ ﻷﻧﻪ ﻳﺮﻣﺾ ﺍﻟﺬﻧﻮﺏ ﺃﻱ ﻳﺤﺮﻗﻬﺎ ﺑﺎﻷﻋﻤﺎﻝ ﺍﻟﺼﺎﻟﺤﺔ.*
*Yaelezewa kwamba: Hakika imeitwa Ramadhani kwa sababu huyayusha madhambi kwa maana huyaunguza kutokana na amali njema.*

*♢ رمضان إسم من الرمض أى ﺷِﺪَّﺓُ الحرِّ*
*Ramadhan ni jina lililo tokana na ramdhi kwa maana joto kali (Lenye kuunguza)*

*Ramadhani huunguza madhambi, Pia vilevile huyayusha mafuta mwilini na hua sababu ya kumkinga mfungaji juu ya vitu vyoote vyenye madhara.*

*Asema Mtume (ﷺ)*

*"الصَّوْمُ جُنَّةٌ، فَإِذَا كَانَ أَحَدُكُمْ صَائِمًا فَلاَ يَرْفُثْ وَلاَ يَجْهَلْ، وَإِنِ اِمْرُؤٌ قَاتَلَهُ أَوْ شَاتَمَهُ فَلْيَقُلْ: إِنِّي صَائِمٌ".*

*☪ MAANA YAKE.*

*“Funga ni kinga, ikiwa mmoja wenu atakuwa amefunga, basi asiseme maneno machafu, na wala asifanye mambo ya kijinga, na akitokea mtu akagombana nae, au akamtukana, aseme, “Mimi nimefunga”.*

*■ FUNGA HUMZUIA MFUNGAJI KUTOFANYA MADHAMBI*.

*■ FUNGA HUMKINGA MFUNGAJI KUTOKANA NA MARADHI MBALIMBALI...*

*■ KADHALIKA HUONDOA SUMU MBALIMBALI KATIKA MWILI WA MWANAADAMU*

*⤴HII NI MAANA FUPI YA NENO RAMADHANI.*

*Tazama Video fupi ifuatayo ili uone faida ya funga kwa afya yako.*


*🌹 ALLAH MTUKUFU: TWAKUAOMBA UZIKUBALI FUNGA ZETU NA QIYAMU ZETU, PIA NA BAKI YA IBADA ZETU.*

✍🏽By:
*Mrisho Othman.*

*"Jiunge Leo Upate Chakula Cha Roho"*
📲+255655559911
 
*•══༻◉••﷽••◉༺══•* *●▬▬▬ஜ۩۞۩ஜ▬▬▬●*

*🌙LEO KATIKA FUNGA🌙*
*{ 2 }*


*Allah ﷻ Anasema:*

*{يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا كُتِبَ عَلَيْكُمُ الصِّيَامُ كَمَا كُتِبَ عَلَى الَّذِينَ مِنْ قَبْلِكُمْ لَعَلَّكُمْ تَتَّقُونَ}*
*Enyi mlio amini! Mmeandikiwa Saumu, kama waliyo andikiwa walio kuwa kabla yenu ili mpate kumchamungu.* (2:183)
"""""""""""""""""""""""""""""""""""""""

*NDUGU ZANGU: AYA HII AMBAYO IMEKUJA KWA LENGO LA SISI KUFARADHISHIWA IBADA YA FUNGA, IMEKUJA KWA NAMNA KUWAKHUSISHA WAUMINI TU, JE KWANINI IMEWAHUSU WAUMINI PEKEE?*

*♡ يا أيها الذين آمنوا، لم يقُل: يا أيُّها الناس، ولم يقل: يا عبادي كتب عليكم الصيام.*
*ALLAH MTUKUFU AMESEMA: ENYI MLIYO AMINI, NA HAIKUSEMA: ENYI WATU, PIA HAIKUSEMA: ENYI WAJA WANGU, MMEFARADHISHIWA JUU YENU KUFUNGA.*

*♡ إنما خاطب المؤمنين بالذات.*
*KWA HAKIKA WALA SI VINGINEVYO, ALLAH AMEWALINGANIA WAUMINI KWA DHATI KABISA.*

*♡ لأنَّ الذي يستجيب لأمر الله هو المؤمن، عندما يسمع الله ينادي عليه يقول: لبَّيك ربي.*
*KWA SABABU YULE AMBAE HUITIKIA AMRI YA ALLAH MTUKUFU NI MUUMINI, ZAMA AMSIKIAPO ALLAH AKIMLINGANIA YEYE HUSEMA NIMEITIKIA EWE MOLA WANGU MLEZI.*

*■ NA HAPA NDIPO UTAKAPOJIFUNZA NA PENGINE KUPATA JAWABU LAKO LA SUALA AMBALO, HUENDA MUDA MREFU UMEKUA UKIJIULIZA: KWANINI BAADHI YA WAISILAMU HAWAFUNGI TENA BILA UDHURU WOWOTE?. HAWAFUNGI KWA SABABU YA KUKOSA IMANI.*

*MAANA SI SIFA YA MUUMINI KUTOITIKIA WITO WA ALLAH MTUKUFU.*

*Allah ﷻ Anasema:*

*{وَمَا كَانَ لِمُؤْمِنٍ وَلَا مُؤْمِنَةٍ إِذَا قَضَى اللَّهُ وَرَسُولُهُ أَمْرًا أَنْ يَكُونَ لَهُمُ الْخِيَرَةُ مِنْ أَمْرِهِمْ ۗ وَمَنْ يَعْصِ اللَّهَ وَرَسُولَهُ فَقَدْ ضَلَّ ضَلَالًا مُبِينًا}*
```Haiwi kwa Muumini mwanamume wala Muumini mwanamke kuwa na khiari katika jambo, Mwenyezi Mungu na Mtume wake wanapo kata shauri katika jambo lao. Na mwenye kumuasi Mwenyezi Mungu na Mtume wake basi hakika amepotea upotofu ulio wazi.```
(33:36)

*■ HII NDIO HEKMA YA ALLAH MTUKUFU KUWAITA WAUMINI KATIKA AYA YA FUNGA.*

*♡ فلماذا جاء الصيام بين الإيمان والتقوى؟*
*JE, KWANINI IMEKUJA FUNGA BAINA YA IMANI NA TAQWA?*

*♡ الإيمان أوَّلاً، والصيام ثانيًا، والتقوى ثالثا*
*KWANZA IMANI, PILI FUNGA, TATU TAQWA. JE KWANINI?*

*IN SHA ALLAH TUTAANGALIA KATIKA DARSA YETU SEHEMU YA TATU.*
______________________

*🌹 ALLAH MTUKUFU: TWAKUAOMBA UZIKUBALI FUNGA ZETU NA QIYAMU ZETU, PIA NA BAKI YA IBADA ZETU.*


✍🏽By:
*Mrisho Othman.*

*"Jiunge Leo Upate Chakula Cha Roho"*
📲+255655559911
 
*•══༻◉••﷽••◉༺══•* *●▬▬▬ஜ۩۞۩ஜ▬▬▬●*

*🌙LEO KATIKA FUNGA🌙*
*{ 3 }*

*Allah ﷻ Anasema:*

*{يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا كُتِبَ عَلَيْكُمُ الصِّيَامُ كَمَا كُتِبَ عَلَى الَّذِينَ مِنْ قَبْلِكُمْ لَعَلَّكُمْ تَتَّقُونَ}*
*Enyi mlio amini! Mmeandikiwa Saumu, kama waliyo andikiwa walio kuwa kabla yenu ili mpate kuchamngu.* (2:183)
"""""""""""""""""""""""""""""""""""""""

*LEO KATIKA FUNGA YAKO, TUNAENDELEA NA DARSA YETU SEHEUMU YA TATU IN SHA ALLAH.*

*♡ فلماذا جاء الصيام بين الإيمان والتقوى؟*
*JE, KWANINI IMEKUJA FUNGA BAINA YA IMANI NA TAQWA?*

*♡ الإيمان أوَّلاً، والصيام ثانيًا، والتقوى ثالثا*
*KWANZA IMANI, PILI FUNGA, TATU TAQWA. JE KWANINI?*

*♢ ولكي نُجيب عن هذا السؤال لا بدَّ لنا أن نسأل سؤالين اثنين:*
*NA ILI TUWEZE KUJIBU SUALA HILI, BASI HAPANA BUDI KWANZA KUJIULIZA MAS ALA MAWILI.*

*♢ ما هو الإيمان؟ وما هي التقوى؟*
*NINI IMANI? NA NINI TAQWA?*

*♢ ثم نسأل سؤالاً ثالثًا: ما محلّ الإيمان وما محل التقوى؟*
*KISHA TUJIULIZE SUALA LA TATU: WAPI MAHALA PA IMANI?*

*♢ أمَّا الإيمان فهو أن نؤمن بكل ما جاء به نبيُّنا محمَّد - صلَّى الله عليه وسلَّم.*
*AMA IMANI NI- KUAMINI YOOTE ALIYO KUJA KWAYO MTUME WETU MUHAMMAD(ﷺ)*

*♢ وكلِمة الإيمان هنا معناها التَّصديق.*
*NA NENO IMANI HAPA, MAANA YAKE NI KUSADIKI.*

*JE KUSADIKI NINI?*

*♢التَّصديق بكل ما جاء به سيِّد الرسل؛ أن نؤمِن بالله وملائكته وكتُبه ورسله واليوم الآخر، وبالقدر خيره وشره، هذا هو الإيمان.*
*KUSADIKI YOOTE ALIYO KUJA KWAYO BWANA WA MITUME.*
*TUMUAMINI ALLAH, MALAIKA WAKE, VITABU VYAKE, MITUME WAKE, NA SIKU YA MWISHO, NA QADAR- KHERI ZAKE NA SHARI ZAKE.*
*■ HII NDIO MAANA YA IMANI.*

*Allah ﷻ Anasema:*

*﴿ آمَنَ الرَّسُولُ بِمَا أُنْزِلَ إِلَيْهِ مِنْ رَبِّهِ وَالْمُؤْمِنُونَ كُلٌّ آمَنَ بِاللَّهِ وَمَلائِكَتِهِ وَكُتُبِهِ وَرُسُلِهِ لا نُفَرِّقُ بَيْنَ أَحَدٍ مِنْ رُسُلِهِ وَقَالُوا سَمِعْنَا وَأَطَعْنَا غُفْرَانَكَ رَبَّنَا وَإِلَيْكَ الْمَصِيرُ ﴾*
```Mtume ameamini yaliyo teremshwa kwake kutoka kwa Mola Mlezi wake, na Waumini vile vile. Wote wamemuamini Mwenyezi Mungu, na Malaika wake, na Vitabu vyake na Mitume wake. Hatutafautishi baina ya yeyote katika Mitume wake, na (Waumini) husema: Tumesikia na tumet'ii. Tunakutaka maghfira Mola Mlezi wetu! Na marejeo ni kwako.``` [البقرة: 285]

*♢ ومحل الإيمان - القلب.*
*NA MAHALA PA IMANI NI MOYONI.*

*Allah ﷻ Anasema:*

*{لَا تَجِدُ قَوْمًا يُؤْمِنُونَ بِاللَّهِ وَالْيَوْمِ الْآخِرِ يُوَادُّونَ مَنْ حَادَّ اللَّهَ وَرَسُولَهُ وَلَوْ كَانُوا آبَاءَهُمْ أَوْ أَبْنَاءَهُمْ أَوْ إِخْوَانَهُمْ أَوْ عَشِيرَتَهُمْ ۚ أُولَٰئِكَ كَتَبَ فِي قُلُوبِهِمُ الْإِيمَانَ وَأَيَّدَهُمْ بِرُوحٍ مِنْهُ ۖ وَيُدْخِلُهُمْ جَنَّاتٍ تَجْرِي مِنْ تَحْتِهَا الْأَنْهَارُ خَالِدِينَ فِيهَا ۚ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُمْ وَرَضُوا عَنْهُ ۚ أُولَٰئِكَ حِزْبُ اللَّهِ ۚ أَلَا إِنَّ حِزْبَ اللَّهِ هُمُ الْمُفْلِحُونَ}*
```Huwakuti watu wanao muamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho kuwa wanawapenda wanao mpinga Mwenyezi Mungu na Mtume wake, hata wakiwa ni baba zao, au watoto wao, au ndugu zao, au jamaa zao. Hao ameandika katika nyoyo zao Imani, na amewapa nguvu kwa Roho itokayo kwake. Na atawaingiza katika Mabustani yapitayo mito kati yake. Humo watakaa daima. Mwenyezi Mungu awe radhi nao, na wao wawe radhi naye. Hao ndio Hizbullahi, Kundi la Mwenyezi Mungu. Hakika Kundi la Mwenyezi Mungu ndilo lenye kufanikiwa.``` (58:22)

*HII NDIO MAANA YA IMANI NA MOYONI NDIO MAHALA PAKE.*
*☆☆☆☆☆☆☆☆☆☆*

*JE NINI TAQWA NA WAPI MAHALA PAKE.?*

*TUTAENDELEA SEHEMU YA NNE IN SHA ALLAH.*
____________________

*🌹 ALLAH MTUKUFU: TWAKUOMBA UZIKUBALI FUNGA ZETU NA QIYAMU ZETU, PIA NA BAKI YA IBADA ZETU.*


✍🏽By:
*Mrisho Othman.*

*"Jiunge Leo Upate Chakula Cha Roho"*
📲+255655559911
 
*•══༻◉••﷽••◉༺══•* *●▬▬▬ஜ۩۞۩ஜ▬▬▬●*

*🌙LEO KATIKA FUNGA🌙*
*{ 4 }*


*Allah ﷻ Anasema:*

*{يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا كُتِبَ عَلَيْكُمُ الصِّيَامُ كَمَا كُتِبَ عَلَى الَّذِينَ مِنْ قَبْلِكُمْ لَعَلَّكُمْ تَتَّقُونَ}*
*Enyi mlio amini! Mmeandikiwa Saumu, kama waliyo andikiwa walio kuwa kabla yenu ili mpate kuchamngu.* (2:183)
""""""""""""""""""""""""""""""""""""""

*BAADA YA KUFAHAMAU NINI IMANI NA WAPI MAHALA PAKE, LEO KWA UWEZO WAKE ALLAH MTUKUFU TUFAHAMU PIA NINI TAQWA NA WAPI MAHALA PAKE.*

*♡ فما هي التقوى؟*
*TAQWA NI NINI?*

*♡ "التقوى: هي الخوف من الجليل، والعمل بالتنزيل، والرضا بالقليل، والاستعداد ليوم الرحيل"*

*TAQWA NI - KUMKHOFU ALLAH, NAKUTENDA KWA MUJIBU WA QUR'ANI, NAKURIDHIA KIDOGO CHA HALALI, PIA KUJIANDAA NA SAFARI (MAUTI)*

*HII NDIO MAANA YA TAQWA KWA UFUPI SANA.*

*♡ محل التقوى- القلب.*
*MAHALA PA TAQWA NI MOYONI.*

*♡ الإيمان تصديق بالقلب، والتقوى محلُّها القلب.*
*■ KUMBUKA: IMANI NI KUSADIKI KWA MOYO (MAHALA PAKE NI MOYONI) TAQWA PIA MAHALA PAKE NI MOYONI.*

*♡ أشار النبي - صلَّى الله عليه وسلَّم - إلى صدره وقال: ((التقوى هاهنها))*

*ALIASHIRIA MTUME (ﷺ) KIFUANI NA AKASEMA: TAQWA IPO HAPA (NDANI YA KIFUA YANI MOYONI)*

*SASA TAZAMA HAPA.*

*♡ الإيمان محلُّه القلب، والتقوى محلها القلب والإيمان في القلب، وكذلك الصيام سر بينك وبين ربِّك لا يعلمه إلاَّ هو.*
*■ IMANI MAHALA PAKE NI MOYONI, TAQWA PIA MAHALA PAKE NI MOYONI, KADHALIKA FUNGA NI SIRI BAINA YAKO NA MOLA WAKO MLEZI, HAKUNA ANAE IJUA FUNGA YAKO ILA ALLAH PEKEE.*

*♡ إذا تستطيع أن تأكل وتشرب بعيد عن عيون الناس وتدعى أنك صائم.*
*HIVO BASI, WAWEZA KULA NA UKANYWA MBALI NA MACHO YA WATU, KISHA UKADAI UMEFUNGA.*

*● LAKINI KWA SABABU FUNGA NI IBADA YA SIRI, BILA SHAKA SIRI HIYO AIJUA ALLAH MTUKUFU NA YEYE KWAKE HAKIFICHIKI KITU.*

*♡ فإذا كان الإيمان أمرًا سريًّا، وكانت التقوى أمرًا سريًّا، وكان الصيام أمرًا سريًّا.*
*SASA BASI, IKIWA IMANI NI JAMBO LA SIRI. NA PIA TAQWA IKAWA NI JAMBO LA SIRI. NA HATA FUNGA NAYO IKAWA NI JAMBO LA SIRI.*

*♡ فناسب ذلك أن يأتي الصيام بين الإيمان والتقوى.*
*NDIO IKAWA SABABU YA MNASABA KWA HILO KUJA IBADA YA FUNGA BAINA YA IMANI NA TAQWA.*

*♡ لأنَّ الثلاثة أمورٌ سرّيَّة لا يطَّلع عليها إلا علام الغيوب.*
*KWA SABABU HAYA MAMBO MATATU NI MAMBO YA SIRI AMBAYO HAKUNA WA KUYAONA ILA MJUZI WA YALIYO JIFICHA (ALLAH MTUKUFU)*


*♡ ولذلك اسمع إلى قول مولانا في الحديث القدسي يؤكد سرّيَّة الصيام، فيقول:*
*KWA AJILI HIYO, SIKILIZA KAULI YA ALLAH MTUKUFU KATIKA HADITHIL QUDSIY ATILIA NGUVU SIRI YA IBADA YA FUNGA KWA KUSEMA*

*"ﻛُﻞُّ ﻋَﻤَﻞِ ﺍﺑْﻦِ ﺁﺩَﻡَ ﻳُﻀَﺎﻋَﻒُ ﺍﻟْﺤَﺴَﻨَﺔُ ﻋَﺸْﺮُ ﺃَﻣْﺜَﺎﻟِﻬَﺎ ﺇِﻟَﻰ ﺳَﺒْﻌﻤِﺎﺋَﺔ ﺿِﻌْﻒٍ ﻗَﺎﻝَ ﺍﻟﻠَّﻪُ ﻋَﺰَّ ﻭَﺟَﻞَّ ﺇِﻟَّﺎ ﺍﻟﺼَّﻮْﻡَ ﻓَﺈِﻧَّﻪُ ﻟِﻲ ﻭَﺃَﻧَﺎ ﺃَﺟْﺰِﻱ ﺑِﻪِ ﻳَﺪَﻉُ ﺷَﻬْﻮَﺗَﻪُ ﻭَﻃَﻌَﺎﻣَﻪُ ﻣِﻦْ ﺃَﺟْﻠِﻲ ﻟِﻠﺼَّﺎﺋِﻢِ ﻓَﺮْﺣَﺘَﺎﻥِ ﻓَﺮْﺣَﺔٌ ﻋِﻨْﺪَ ﻓِﻄْﺮِﻩِ ﻭَﻓَﺮْﺣَﺔٌ ﻋِﻨْﺪَ ﻟِﻘَﺎﺀِ ﺭَﺑِّﻪِ ﻭَﻟَﺨُﻠُﻮﻑُ ﻓِﻴﻪِ ﺃَﻃْﻴَﺐُ ﻋِﻨْﺪَ ﺍﻟﻠَّﻪِ ﻣِﻦْ ﺭِﻳﺢِ ﺍﻟْﻤِﺴْﻚِ"* متفق عليه.
*MAANA YAKE:*

*"Kila amali njema ya mwanaadamu inalipwa mara kumi na inaongezewa thawabu kutoka kumi hadi mia saba. Na Allah ﷻ Anasema: Isipokuwa Swawm, kwani hiyo ni kwa ajili Yangu na Mimi Ndiye Nitakayemlipa. Ameacha matamanio yake na chakula chake kwa ajili Yangu. Kwa aliyefunga swawm atapata furaha mbili; furaha anapofuturu na furaha atakapoonana na Mola wake, harufu inayotoka kinywani mwa aliyefunga ni nzuri mbele ya Allaah kuliko harufu ya misk"*

*■ HII NDIO HEKIMA YA KUJA IBADA YA FUNGA BAINA YA IMANI NA TAQWA, KWA SABABU HIVYO VITU VITATU VYOOTE NI VITU VYA SIRI NA NDIO MAANA VIMEAMBATANA.*
*♢♢ والله أعلم*
_____________________

*🌹 ALLAH MTUKUFU: TWAKUOMBA UZIKUBALI FUNGA ZETU NA QIYAMU ZETU, PIA NA BAKI YA IBADA ZETU.*

✍🏽By:
*Mrisho Othman.*

*"Jiunge Leo Upate Chakula Cha Roho"*
📲+255655559911
 
*MAFUNDISHO YA KISLAMU KUPITIA CHUO CHA KIIBADHI*
*HISTORIA*🌴098🌴

B. *WAKUU WA KIARABU WALIOKUWA WAKIJA KWA MTUME (S.A.W.) KUSILIMU*

Tumekwisha kuona ya kuwa Mtume (s.a.w.) hakupigana tena vita vikubwa na Waarabu baada ya vita vya Hunayn. Bali alisalia katika mji wa Madina anatengeneza mambo ya miji aliyoiteka na anayoazimia kuiteka kwa salama bila ya vita. Watu wake aliowapeleka kwenye miji hiyo waliyoiteka ili wafundishe dini walikuwa mahodari sana, wakajitahidi kuzitia kwenye dini ya Kiislamu kila kabila zilizokuwa hazikusilimu bado. Kila kabila moja ikisilimu wakichagua baadhi ya wakubwa wake wakiwapeleka Madina ili kuonana na Mtume (s.a.w.) na kujifundisha zaidi mambo ya Uislamu, ili wapate kuja wafundisha wenziwao. Basi muda wa miaka miwili Mtume (s.a.w.) alikuwa katika mji wa Madina tu akiwapokea kila wakubwa wa kabila hizo zilizokuwa zikisilimu. Palitengenezwa mahala makhsusi pa kufikia watu hao wanaokuja, na zikatafutwa njia maalum za kupatikana chakula cha kuwalisha watu hao, muda wa kuwapo huko Madina mpaka kwenda zao makwao.

Baadhi ya mabwana hao waliokuwa wakija walikuwa ni wale wale ambao Mtume (s.a.w.) aliwaambia waingie katika dini hii wakakataa katakata, bali walimtukana na kumpiga pia. Lakini ulimwengu umegeuka, sasa wanakuja wenyewe kusilimu bila ya kulazimishwa wala kushikiliwa.

Baada ya mwaka mmoja kwisha tangu kutekwa Makka, kabila nyingi za kiarabu zilikuwa zimekwisha kusilimu, lakini nyengine zilikuwa bado zinaendelea na dini yao ya kikafiri. Siku za hija zikasonga sasa, Mtume (s.a.w.) akapenda kwenda kuhiji, lakini aliona vibaya kwenda kuchanganyika na makafiri katika kuhiji, kwani alijua kwamba makafiri watakuja kuhiji kama ada yao, kwa hivyo alimwamrisha Sayyidna Abubakr ende akahijishe Waislamu wanaotaka kuhiji. Akatoka Sayyidna Abubakr na watu 300, wakenda zao Makka kuhiji.


Jiunge kwa kusave namba hii +96896117092, kisha tuma kwa whatsapp neno *" MAFUNDISHO YA KIIBADHI"*

*30 - Shaban - 1440H*
*06 - May - 2019M*
 
*HUYU NDIE ALIE FUNGA*

*-----••-----*

ﻗـﺎﻝ الإمام ﺍﺑﻦ ﺍﻟﻘﻴِّﻢ ﺭﺣﻤﻪ ﺍﻟﻠﻪ :
Amesema ibn qayyim Allah amrehem:


ﻭﺍﻟﺼﺎﺋﻢ ﻫﻮ ﺍﻟﺬﻱ :
Aliefunga ni yule ambae :


صامَت ﺟﻮﺍﺭﺣﻪ ﻋﻦ ﺍﻵﺛﺎﻡ ،
Vimefunga viungo vyake kutokana na madhambi


ﻭﻟﺴﺎﻧﻪ ﻋﻦ ﺍﻟﻜﺬﺏ ، ﻭﺍﻟﻔُﺤﺶ ، ﻭﻗﻮﻝ ﺍﻟﺰُّﻭﺭ ،
Na umefunga ulimi wake kutokana na uongo , na maneno machafu na maneno ya uongo


ﻭﺑﻄﻨﻪ ﻋﻦ ﺍﻟﻄﻌﺎﻡ ﻭﺍﻟﺸﺮﺍﺏ
Na limefunga tumbo lake kutokana na chakula na kinywaji

ﻭﻓﺮﺟﻪ ﻋﻦ ﺍلرَّفث ،
na umefunga utupu wake kutokana tendo la ndoa ( mchana wa Ramadhani)


ﻓﺈﻥْ ﺗﻜﻠﻢ ﻟﻢ يتكلم ﺑﻤﺎ ﻳﺠﺮﺡ ﺻﻮﻣﻪ ،
ﻭﺇﻥ ﻓﻌﻞ ﻟﻢ ﻳﻔﻌﻞ ﻣﺎ ﻳﻔﺴﺪ صومه ،
akizungumza hazungumzi yale yanayo haribu funga yake , na akifanya hafanyi yale yatakayo haribu funga yake


ﻓﻴﺨﺮﺝ ﻛﻼﻣﻪ ﻛﻠُّﻪ ﻧﺎﻓﻌًﺎ ﺻﺎﻟﺤًﺎ ، ﻭﻛﺬﻟﻚ ﺃﻋﻤﺎﻟﻪ : ﻓﻬﻲ ﺑﻤﻨﺰلة ﺍﻟﺮﺍﺋﺤﺔ ﺍﻟَّﺘﻲ ﻳﺸﻤُّﻬﺎ ﻣَﻦ ﺟﺎﻟﺲ ﺣﺎﻣِﻞ ﺍﻟﻤﺴﻚ ،
*( Mfungaji ) hutoka maneno yake yote yakiwa mazuri na yenye manufaa , na pia matendo yake , mfungaji ni kama mfano wa harufu anayoinusa atakae kaa na muuza manufako*


ﻛﺬﻟﻚ ﻣَﻦ ﺟﺎﻟﺲ ﺍﻟﺼﺎﺋﻢ :
ﺍﻧﺘﻔﻊ ﺑﻤﺠﺎﻟﺴﺘﻪ ، ﻭﺃَﻣِﻦ ﻓﻴﻬﺎ ﻣﻦ ﺍﻟﺰُّﻭﺭ ﻭﺍﻟﻜﺬﺏ ، ﻭﺍﻟﻔﺠﻮﺭ ﻭﺍﻟﻈُّﻠﻢ ،
Na pia vile vile atakae kaa na aliefunga : hunufaika na kukaa nae na husalimika na uzushi na uongo na uovu na dhulma


ﻫﺬﺍ ﻫﻮ ﺍﻟﺼَّﻮﻡ ﺍﻟﻤﺸﺮﻭﻉ ؛ ﻻ ﻣﺠﺮَّد ﺍﻹﻣﺴﺎﻙ ﻋﻦ ﺍﻟﻄَّﻌﺎﻡ ﻭﺍﻟﺸَّﺮﺍﺏ ،
*hii ndio funga yakisheria , si mujarad wa kujizuia na kula na kunywa*


ﻓﺎﻟﺼﻮﻡ ﻫﻮ ﺻﻮﻡ ﺍﻟﺠﻮﺍﺭﺡ ﻋﻦ ﺍﻵﺛﺎﻡ ، ﻭﺻﻮﻡ ﺍﻟﺒﻄﻦ ﻋﻦ ﺍﻟﺸﺮﺍﺏ ﻭﺍﻟﻄﻌﺎﻡ ،
Funga ni kufunga viungo kutokana na madhambi na kufunga tumbo kutokana na kula na kunywa


ﻓﻜﻤﺎ ﺃﻥَّ ﺍﻟﻄﻌﺎﻡ ﻭﺍﻟﺸﺮﺍﺏ ﻳﻘﻄﻌﻪ ﻭﻳﻔﺴﺪه ؛
Kama ilivyo chakula na kinywaji huiharibu na kuikata funga


ﻓﻬﻜﺬﺍ ﺍﻵﺛﺎﻡ ﺗﻘﻄﻊ ﺛﻮﺍﺑَﻪ ، ﻭﺗﻔﺴﺪُ ﺛﻤﺮﺗَﻪ ، ﻓﺘُﺼَﻴِّﺮه ﺑﻤﻨﺰﻟﺔ ﻣﻦ ﻟﻢ ﻳﺼُﻢ .
*hivyo hivyo Madhambi hukata thawabu zake , na huaribu Matunda yake , na humfanya mfungaji kana kwamba hakufunga*

ﺍﻟﻮﺍﺑﻞ ﺍﻟﺼﻴِّﺐ : (٣١/٣٢)
Al-waabil As-swayyib 31/32

*------••-----*

```MFASIRI: ABUU FAT'HIYAH KHAMIS KIZA, ALLAH AMUHIFADHI```

 
Back
Top Bottom