Ramadhan Special Thread


YANAYOHUSIANA NA FUNGA YA RAMADHANI (NO. 17)


حـكـم مـا يـخـرج مـن الـمعـدة إلـى الـحلـق أثنـاء الـصيـام ؟

Hukumu ya kile kinachotoka tumboni mpaka (kikafika) kooni wakati wa funga ?


قال ابن عثيميــن - رحمـہ الله -

Amesema Ibn 'Uthaimin - Allah amrahamu -


يـحـدث ڪثـيراً مـع النـاس إذا امـتلأت الـمـعـدة بـالطعـام،

Hutokea (jambo hili) kwa watu wengi pindi tumbo linapojaa chakula,


فـإن الإنسـان إذا تجشـأ،

Basi bila shaka mwanadamu (muislamu) atakapocheua (rudisha chakula),


وخـرج الهـواء مـن معدتـه،

Na kukatoka hewa kutoka tumboni kwake,


قـد يخـرج شيء مـن الطعـام،

Huenda kukatoka chochote katika chakula,


أو مـن المـاء،

Au katika maji,


فـإذا لـم يصـل إلـى الفـم،

Basi kama hakijafika kinywani,


وابتلعـه،

Na akakimeza,


فـلا شيء عليـه.

Basi hakuwajibiki lolote juu yake.


لـقـاء الـبـاب الـمفتـوح (20)

[ Liqaau l-baabi l-maftuuh ]


Maelezo kutoka kwa mfasiri - Allah amuhifadhi

Sheikh - Allah amrahamu - amezungumzia ikiwa hakijafika kinywani na akakimeza funga yake haiharibiki,

Ama kikifika kinywani na kisha akakimeza kwa kusudi na hali ya kuwa anakumbuka na anajua basi funga yake itakuwa imeharibika na anawajibika kuilipa siku hiyo na haruhusiwi kula bali ajizuie.


Mfasiri: Abuu Thurayyaa Ismail Seiph Mbonde - Allah amuhifadhi
Dar es salaam, Tanzania
Kiunganishi: https://t.me/fawaidussalafiyatz
Jiunge nasi upate faida mbalimbali.

| Jivunie ujira wa kusambaza faida hizi, sambaza kama ulivyopokea bila kubadilisha chochote |

Kupata faida nyingi jiunge na channel yetu ya Telegram kwa Link hii: ⇩


Pia jiunge nasi katika Instagram, Twitter, facebook na you tube:
@fawaidussalafiyatz

•┈┈┈┈••✦✿✦••┈┈┈┈•
 

*SABABU ZA KUPUNGUA IMANI*

Amesema sheikh ibn Uthaimin Allah amrehem :

و الخلاصة ان سبب نقصان الإيمان ثلاثة :

Na ufupisho, hakika sababu za kupungua imani ni tatu :

الاول : الإعراض عن التفكر في آيات الله الكونية أو الشرعية .

Ya kwanza : *Kupuuza kufikiria Alama za Allah za kiulimwengu au kisheria*

و الثاني : ترك الطاعات .

Ya pili: *Kuacha kufanya Twaa ( ibada )*

الثالث : فعل المعاصي .

Ya Tatu : *Kufanya Maasia ( madhambi )*

التعليق على صحيح مسلم المجلد الاول (ص٢٦٣)
At-taliiq A'alaa swahiih Muslim Juzuu 1 Uk 263


Nimesema :

Allah subhaanah wataala katika ulimwengu huu ametuwekea katika yale alioyaumba kuna mambo lau tutayafikiria Itakuwa ni sababu ya kuongezeka Imani zetu

Lakini pia miongoni mwa sababu za kushuka na kupungua Imani ni kutoshughulika na kujifunza Dini *kwa maana hiyo ujinga wa mambo ya kisheria ni sababu ya kushuka kwa imani*

Mfasiri: Abuu Fat'hiyya Khamisi Kiza (Allah amuhifadhi), Dodoma Tanzania

*Usibadili Chochote*
 
Zipo kauli za Baadhi ya Vijana wa Dodoma
wamesema kwamba wameuona kwa macho yao,na kutoa kiapo

Na Audio zinatambaa katika Magroup ya WatsApp

Ama kuhusu Saudia
Ni kweli

Na baadhi ya nchi za Kiarabu
Naskia mwezi umeandama sudia kweli?
 
Uganda wametangaza pia
Kwa taarifa hii
IMG-20190603-WA0066.jpeg
 
Waislam wafuatilie hili kwa umakini,hususan wale ambao leo wana 28

Ili kujipa uhakika katika Ibada yao

تقبل الله منا ومنكم
 
Hata mimi nimeipata taarifa ya huyo jamaa kwenye watsap lakini sasa hata jina hakutaja,hatujui kama alifikisha taarifa vyombo husika ama hakufikisha.
Zipo kauli za Baadhi ya Vijana wa Dodoma
wamesema kwamba wameuona kwa macho yao,na kutoa kiapo

Na Audio zinatambaa katika Magroup ya WatsApp

Ama kuhusu Saudia
Ni kweli

Na baadhi ya nchi za Kiarabu
 
Back
Top Bottom