Ramadhan Special Thread

1710857950288.png
 
Tusome kisa juu ya Kumwamini Allah

Kutoka kwa Shuaib amesema Mtume swalallahu alayh wassalam

Kulikuwa na Mfalme ambaye alikuwa na mchawi wake, ikafikia kipindi yule mchawi akamwambia mfalme,hakika sasa nimekuwa mzee nitafutie kijana wa kumfundisha uchawi.

Mfalme akamtafuta kijana mmoja awe anaenda kwa mchawi kujifunza uchawi, wakati kijana akiwa njiani kwenda kwa mchawi alikuwa anakutana na mtawa mmoja anasiikiliza mazungumzo yake kisha anaenda kwa mchawi,kijana akawa anavutiwa sana na yale mazungumzo ya mtawa mpaka akawa anachelewa kwenda kwa mchawi na hivyo kuchapwa.

Akaja kulalamika kwa mtawa, basi mtawa akamwambia mwambie mchawi kuwa watu wako wanakushughulisha ndio maana unachelewa, na ukiogopa watu wako nao waambie kuwa mchawi anakuchelewesha.

Siku Moja wakati kijana anaenda kule kwa mchawi njiani kuna kiumbe kikubwa sana kiliingia barabarani na watu wakawa wanaogopa kupita.

Yule kijana akasema leo nataka nione maneno gani ni ya kweli kati ya mchawi na yule mtawa. Basi akachukua jiwe na kusema Ewe Allah ikiwa vitendo vya mtawa vinakupendeza zaidi kuliko vya yule mchawi basi muue kiumbe hiki, kijana akarusha jiwe na kile kiumbe kikafa.

Yule kijana akawa na uwezo wa kuponyesha vipofu wa kuzaliwa, na watu wenye Maradhi ya ngozi na mengineyo, kuna mshauri mmoja wa mfalme alikuwa kipofu aliposikia habari za kijana yule basi, alitafuta zawadi na kumletea kijana yule na kumwambia basi niponye ntakupa zawadi hizi, kijana akajibu mimi sio mponyaji ila anayeponya ni Allah, ikiwa unataka kuponywa basi mkubali Allah na umuamini kisha atakuponya.

Basi yule bwana akakubali na kuponywa, akarejea kwa mfalme,baada ya mfalme kumuona akamuuliza nani amekuponya upofu wako? Akajibu ni Allah. Mfalme akasema kwahiyo una Mungu mwingine badala yangu? Akajibu Allah ndio Mungu wako na Mungu wangu, basi akateswa mpaka akamtaja yule kijana.

Mfalme akasema kijana aletwe, nae akaulizwa inamaana umejifunza uchawi mpaka umefikia kiwango cha kuponya watu upofu na maradhi mengine? Kijana akajibu anayeponya ni Allah,naye akateswa mpaka akamtaja Mtawa, hapo awali baada ya tukio lile la kumwambia Allah kama unapendezewa na vitendo vya mtawa kuliko mchawi basi muue kiumbe hichi. Alienda kumpa habari mtawa, na mtawa akasema hakika leo umenishinda hata mimi ila hivi karibuni utapata majaribu lakini usije kunitaja.

Lakini kutokana na mateso ikabidi tu amtaje mtawa, basi mtawa aliletwa mbele ya mfalme akaambiwa ikane imani yako la sivyo atauwawa, mtawa akakataa basi mfalme akaagiza msumeno na kumkata mtawa vipande viwili.

Kisha mshauri wa mfalme akaambiwa aikane imani yake nae akakataa, naye akakatwa na msumeno, kisha mfalme akamwambia kijana aikane imani yake akakataa.

Mfalme akasema mchukueni huyu kijana nendeni nae juu ya kilele cha mlima, akikataa kuikana imani yake basi mrusheni kutoka huko, walipofika kileleni akasema Ewe Allah naomba uniokoe kwa namna yoyote unayopenda, basi mlima ukatingishika na wale watu wa mfalme wakaanguka na kujifia, kisha kijana akarudi kwa mfalme.

Mfalme akauliza imekuaje kuhusu watu wangu, akajibu Allah ameniokoa. Mfalme akaagiza watu wake waende na kijana katikati ya bahari, akikataa kuikana imani yake basi wamtumbukize baharini, akasema Ewe Allah naomba uniokoe kwa namna yoyote unayotaka, basi boti zikazama na wale watu wakafa, kisha kijana akarudi kwa mfalme.

Mfalme akauliza kama awali akajibiwa Allah ameniokoa, sasa kijana akamwambia huwezi kuniua ila mpaka utumize sharti langu, mfalme akasema sharti gani hilo?

Akamwambia wakusanye watu katika ardhi yenye mwinuko kisha nifunge kwenye mti halafu chukua mshale na useme kwa uwezo wa Allah mola wa huyu kijana nitakuua!

Basi akaachia mshale na kumpiga yule kijana katika paji la uso na yule kijana akanyanyua mikono yake na kugusa pale alipopigwa na kufa.

Watu wakaanza kupaza Sauti na kusema Tunamwamini Allah mola wa huyo kijana, basi mfalme akaamuru uchimbwe mtaro mkubwa pembeni ya barabara, kisha ndani ya mtaro pakawashwa moto, kisha mfalme akasema yoyote ambaye haikani imani yake atatumbukizwa mtaroni.

Watu wakawa radhi kuingizwa mtaroni kuliko kuikana imani yao juu ya Allah, basi kulikuwa na mwanamke mmoja ana mtoto mdogo, akawa anasita kuingia mtaroni, yule mtoto mdogo Kabisa akamwambia Mama usiogope kuwa miongoni mwa wenye subira imani yako ni ya kweli, basi akajirusha na kuwa miongoni mwa mashahidi walioingia peponi.

(sahihi Muslim, hadith no. 7148)
 
slogan_mobile.png

Ukurasa Wa Kwanza

Ukurasa Wa Kwanza /Makosa Yafanywayo Na Wenye Swawm Katika Mwezi Wa Ramadhwaan

Makosa Yafanywayo Na Wenye Swawm Katika Mwezi Wa Ramadhwaan​

Ramadhaan-Swawm

Makosa Yafanywayo Na Wenye Swawm Katika Mwezi Wa Ramadhwaan

Alhidaaya.com

Yafuatayo ni makosa ambayo yameonekana yakitendeka katika mwezi wa Ramadhwaan ima wanapokuwa Waislamu katika Swawm au baada ya kufuturu na katika Swalah za Qiyaamul-Layl. Hivyo inapasa tuyazingatie na kujiepusha nayo ili tubakie katika usalama wa Swawm zetu, Swalah zetu na mengine yote yanayohusu mwezi huu mtukufu:

1. Kutia Niyyah Kwa Kutamka:

Baadhi wanaamini kuwa niyyah usipoitamka basi haijawa niyyah. Na pia huwafunza watoto kutamka maneno ya kutia niyyah, au kuwaamrisha wasikose kwenda kunuizwa Msikitini na mashekhe. Itambulike kuwa niyyah mahali pake ni moyoni na kutamka ni uzushi.

2. Kufunga bila kuswali:

Baadhi ya watu wanafunga bila ya kuswali au kutimiza Swalah ipasavyo. Watu kama hawa Swawm zao hazifai kwani Swalah ni nguzo ya Dini ya Kiislamu.

3. Kudhani kwamba Swalah ya Taraawiyh inaanzwa siku ya kwanza ya Ramadhwaan:
Hali inaanza usiku ule unaoandama mwezi. Sunnah ni Waislamu waanze kuswali usiku huo na si baada ya kufunga siku ya kwanza.

4. Kuchelewa Kufuturu/Kufutari:
Baadhi ya watu husubiri hadi adhana imalizike na wengine husubiri hadi kiza kiingie na hali tumehimizwa tukimbilie kufuturu. Matokeo yake ni kukiuka Sunnah ya Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na pia huenda kufanya hivyo wakachelewa Swalah ya Magharibi. Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) anasema:

لا تزال أمتي بخير ما عجَّلوا الإفطار - رواه الإمام أحمد
Ummah wangu utabakia katika khayr watakapokimbilia kufuturu. [Imaam Ahmad]

5. Kuomba Du'aa Zisizo Sahihi Wakati Wa Kufuturu:
Wengi wameizoea du’aa hii na kuisoma wakati wa kuanza kufuturu, ingawa ni du’aa yenye mapokezi dhaifu yasiyo sahihi:
اللَّهمَّ! لك صُمتُ، وعلى رِزقك أفطرتُ
Allaahumma Laka Swumtu wa 'alaa Rizqika aftwartu.

Wanachuoni wa Hadiyth wanaeleza kuwa hakuna du’aa yoyote iliyothibiti wakati wa kufuturu.

7. Kufuturu Kwa Vitu Vya Haraam Kama Kuvuta Sigara N.k.
Wanakosa kutambua kwamba hii fursa kubwa kwa waliozoea kuvuta sigara kuacha moja kwa moja kuanzia mwezi wa Ramadhwaan, kwani ikiwa wameweza kufunga siku nzima na kujizuia kuvuta, vipi washindwe kujizuia na usiku?

8. Kula Futari Kupita Kiasi:
Utakuta mtu akifuturu huwa anafanya kisasi, anataka ale kulipiza ile njaa ya siku nzima, matokeo yake anashiba kiasi kushindwa hata kwenda kuswali Taraawiyh.

9. Kukithirisha Michezo na Upuuzi:
Utakuta watu wakati uingiapo mwezi wa Ramadhwaan, ndio wanaanza kutoa ile michezo waliyoiweka pembeni mwaka mzima, au kwenda kununua michezo mipya kama karata, carrum (keram), drafti, domino (dhumna) n.k. wakicheza mchana kutwa ili kupitisha muda uende haraka. Na kisha ifikapo usiku badala ya kwenda kuswali Taraawiyh.
Wanakesha kwa kuangalia televisheni, filamu na mipira.

Na wengine wakiyaambatanisha hayo kwa kula mirungi na kuvuta sigara. Hayo ni mambo ya haramu na yenye kuwapotezea fadhila na ujira upatikanao katika Ramadhwaan, wakati ambapo wangeutumia mchana wao kuchuma kwa kusoma Qur-aan sana na kuhudhuria darsa za Dini au kusoma vitabu vya Dini, kusikiliza mawaidha, Qur-aan n.k. Na ifikapo jioni wangeutumia muda wao kusimamisha Swalah za usiku (Taraawiyh), na pia kupumzika ili waweze kuwahi Swalah ya Alfajiri. Gumzo lisilokuwa katika mas-ala ya Dini jambo lililochukizwa na Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kama usimulizi ulivyopokelewa kutoka kwa ‘Abdullaah bin Mas-uwd (Radhwiya Allaahu 'anhu):

عن عبد الله بن مسعود: ((لا سمر إلا لمصل أو مسافر)) السلسلة الصحيحة - المحدث: الألباني
Hakuna kupiga gumzo la usiku isipokuwa kwa mwenye kuswali au msafiri. [As-Silsilat Asw-Swahiyhah – Al-Muhaddith Al-Albaaniy]

وعن أبي برزة "أن رسول الله صلى الله عليه وسلم كان يكره النوم قبل العشاء والحديث بعدها" رواه البخاري، ومسلم
Na kutoka kwa Abu Barzah kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akichukia kulala kabla ya 'Ishaa na gumzo baada yake) [Al-Bukhaariy na Muslim]

10. Kusengenya, Kudanganya, Kupiga Porojo Na Kukaa Mabarazani Kupoteza Wakati:
Wanajisahau wengi wetu kwa kupiga soga zisizo na maana na pia kusema wenzao, kutukana, kulaani na kuongea mambo ya uongo n.k. Pia wengi wetu wakifunga huwa na khasira sana. Huko kunapelekea mtu kupoteza ujira wa funga yake na pia hata kuibatilisha (kwa maoni ya ‘Ulamaa wengine), Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) anasema: Ambaye hatoacha maneno ya uongo na matendo yake, basi ajue kwamba Allaah hana haja ya yeye kuacha chakula chake na kinywaji chake. [ameisimulia Imaam al-Bukhaariy]

11. Kuwachukua watoto wadogo Misikitini ambao wanafanya fujo na kusababisha kushawishi Imaam na Maamuumiyn (wanaoswali) washindwe kupata khushuu (unyenyekevu) katika Swalah.
Kuwazoesha watoto Msikiti ni jambo zuri kabisa, lakini panapoonekana kuna matatizo kama hayo, basi ni bora kuwaepusha ili wasiharibu Swalah za wengi.

12. Kutokukamalisha Swalah ya Taraawiyh na Imaam ili kupata fadhila za Qiyaamul-Layl kwani Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:

((مَنْ قَامَ مَعَ الإِمَامِ حَتَّى يَنْصَرِفَ كَتَبَ اللَّهُ لَهُ قِيَامَ لَيْلَةٍ)) رواه الترمذي وصححه الألباني في صحيح الترمذي
Atakayesimama (kuswali) na Imaam hadi amalize ataandikiwa (fadhila za) Qiyaamul-Layl. [Imesimuliwa na at-Tirmidhiy na kaipa daraja ya Swahiyh al-Albaaniy katika Swahiyh at-Tirmidhiy]

13. Kushika Mus-haf na Kumfuatiliza Imaam Anaposwalisha:
Kufanya hivyo, kunamkosesha mtu kuipata Sunnah ya kufunga mikono yake na pia kupoteza fadhila za kuisikiliza Qur-aan kutoka kwa Imaam ambayo tumeamrishwa kuisikiliza inaposomwa, Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

وَإِذَا قُرِىءَ الْقُرْآنُ فَاسْتَمِعُواْ لَهُ وَأَنصِتُواْ لَعَلَّكُمْ تُرْحَمُونَ
Na inaposomwa Qur-aan, basi isikilizeni kwa makini na bakieni kimya (mzingatie) ili mpate kurehemewa. [A'raaf:204]

14. Kusoma Tasbiyh Fulani Kila Baada Ya Rakaa Nne Ya Mapumziko:
Hakuna dalili ya kufanya hivyo. Lililothibiti ni kusoma tasbiyh mwisho kabisa unapomaliza Swalah ya Witr kwa kusema mara tatu:
سُبْحَانَ الْمَلِكِ الْقُدُّوسِ
Subhaanal-Malikul-Qudduus

(Kisha ya tatu utaivuta na kuisema kwa sauti ya juu)

15. Kuharakisha kula Daku:
Utakuta baadhi ya watu wanawahisha Daku na kuila saa sita za usiku au hata baada tu ya Taraawiyh, ima kwa kutaka walale moja kwa moja hadi Alfajiri au kwa sababu ya uvivu wa kuamka kwa ajili ya Daku. Kufanya hivyo ni makosa kwa sababu kunakwenda kinyume na mafunzo ya Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam), na pia kunapelekea kuikosa ile baraka iliyojaaliwa kwenye Daku. Na Daku si lazima kula mlo mzito, japo tende au maji yatosha. Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) anasema:

((عجلوا الإفطار، وأخروا السحور)) صحيح الجامع - صححه الآلباني
Harakisheni kufuturu na chelewesheni daku [Swahiyh al-Jaami' na kaipa daraja ya Swahiyh Shaykh Al-Albaaniy]

16. Kudhani Mwisho Wa Kula Daku Ni Dakika Kumi Kabla Ya Adhana Ya Alfajiri:
Hivyo mtu akichelewa kula daku na ikawa karibu na dakika chache tu kabla ya Alfajiri hujinyima daku kwa khofu kuwa Swawm yake itabatilika. Wengine wameweka mipaka ya dakika kumi, hivyo si sawa. Mtu anaweza kula daku hadi karibu na Alfajiri hata kunapoadhiniwa. Na pindi Muadhini akiadhini ndipo unapoanza kufunga na Swawm yako inasihi. Na hata Muadhini akiadhini na kama una tonge au fundo la maji mdomoni usiliteme, kamilisha kulimeza kisha ndio uanze kufunga. Haya yamethibiti katika Sunnah kama inavyoonyesha Hadiyth ifuatayo:

Kutoka kwa Sufyaan bin ‘Uyaynah kutoka Az-Zuhriy, naye kutoka kwa Saalim naye kutoka kwa baba yake, kwamba Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) anasema: ((Hakika Bilaal anaadhini usiku (adhana ya mwanzo), basi kuleni na mnywe hadi aadhini Ibn Ummi Maktuwm)) [At-Tirmidhiy]

17. Kudhani Kwamba Mtu Anapoamka Na Janaba Huwa Swawm Yake Haifai:
Dhana hiyo si sahihi, bali sahihi ni kuwa mtu anaweza kujitwaharisha hata baada ya kuingia Alfajiri mradi tu aiwahi Swalah ya Alfajiri isije kumpita. Na Swawm yake ni sahihi.

18. Kufunga ukiwa safarini:
Walioko safarini kujikalifisha na kujitia katika mashaka ya kufunga na kuacha kuchukua rukhsa iliyotolewa kufuturu; si jambo jema kufanya hivyo kama ilivyo dalili ya Hadiyth:

عن جابر بن عبد الله أن رسول الله صلى الله عليه وسلم رأى رجلا يظلل عليه والزحام عليه فقال: ((لَيْسَ مِنَ الْبِرِّ الصِّيَامُ فِي السَّفرَ)) صحيح أبي داود
Kutoka kwa Jaabir bin 'Abdillaah ambaye amesema: "Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alimuona mtu akiwa amewekwa chini ya kivuli hali yake taabani baada ya kudhoofika kutokana na Swawm akamwambia: ((Sio katika wema (Kumcha Allaah) kufunga katika safari)) [Swahiyh Abiy Daawuud]. Lakini ikiwa hakutokuwa na taklifa wala mashaka, mtu anaruhusiwa kufunga.

19. Kutokujua Hukmu za Swawm:
Baadhi ya watu hawajui Hukmu sahihi za funga kisha huwa hawaulizi, ima kwa kuona hayaa au wakidhani wanajua. Ni vizuri mtu aulize lile asilo na hakika nalo kwa wale wenye elimu, ile asije akakosa fadhila na khayr hizi zipatikanazo kwa nadra mno. Na hali ya kutokujua Fiqh ya Swawm, kama kujua mambo yenye kufunguza na yale yasiyofunguza, kunaweza kumpelekea mtu kushinda na njaa bure huku Swawm yake ishabatilika, au kumfanya mtu afungue na hali Swawm yake bado ni sahihi. Mfano wa mambo yasiyobatilisha Swawm ni; kudungwa sindano, kung'oa jino, kujipulizia dawa ya pumu, wanawake kufanyiwa ukaguzi sehemu zao za siri na daktari (gynaecology checkup) - mtu ahakikishe anampata daktari wa kike na akiwa Muislam ndio bora zaidi, na akikosa kabisa hapo ni dharura tena na halaumiwi - na hili si katika Ramadhwaan tu, bali ni wakati wowote mwanamke anapokwenda Hospitali awe anafanya jitihada na kuuliza apatiwe daktari wa kike.

20. Kumjua Allaah Katika Ramadhwaan Pekee:
Baadhi ya watu humkumbuka Allaah katika mwezi huu tu, utakuta wanafunga na kuswali katika Ramadhwaan kisha baada ya Ramadhwaan kila kitu kinasimama kana kwamba Allaah Hayupo tena! Ni vyema watu wajue kuwa Allaah ni wa miezi yote na si mwezi wa Ramadhwaan pekee.

21. Kutamani Ramadhwaan Iishe:
Baadhi ya watu wanahesabu masiku na wakiwa wanaomba Ramadhwaan imalizike upesi ili warejee katika hali yao ya kawaida ambayo wanaiamini kuwa ina uhuru wa kufanya wanayoyataka. Lau angelijua mja fadhila na khayr zilizo katika mwezi huu, hakika angetamani usiishe.

Katika mwezi ambapo tendo dogo lakuingizia ujira zaidi ya maradufu. Katika mwezi huu kuna usiku ambao ni bora kuliko miezi elfu. Katika mwezi huu vishawishi na balaa za Shaytwaan vimewekwa mbali. Katika mwezi huu Malaika wametapakaa kukusanya ‘amali zako za khayr hata za udogo wa sisimizi

Tunamuomba Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa Atuongezee elimu ya Dini Yake Tukufu ili tuzidi kutoka katika kiza na kuingia katika mwanga utuongoze katika Swiraatwul-Mustaqiym.

KWA HISANI YA TOVUTI YA ALHIDAAYA. COM

lj_match
 
Narrated Abu Hurairah [radhi-yAllahu 'anhu]: The Prophet (ﷺ) said, "The one who looks after a widow or a needy person is like a Mujahid (fighter) who fights for Allah's Cause, or like him who performs prayers all the night and fasts all the day."

[Sahih Al-Bukhari, 7/5353 (O.P.265)]

Kutoka kwa Abu Hurairah (r. a) amesema Mtume swalla aallahu alayhi wassalam "Yule ambaye atamwangalia mjane au mtu mwenye uhitaji ni kama mujahidi anayepigana katika njia ya Allah au kama yule mtu anayeswali usiku Kucha na kufunga mchana kutwa.

Ndugu zangu katika imani katika kipindi hiki cha ramadhani tuzidi kuwa wakarimu zaidi kwa watu hawa.
 
Chapter 13. Abandoning of As-Salat (prayers) is disbelief.

a) Narrated Jabir bin 'Abdullah [radhi-yAllahu 'anhu]: I heard Allah's Messenger (ﷺ) saying, "Verily, between a man (i.e., a Muslim, believer of Islamic Monotheism) and between Ash-Shirk (polytheism) and Al-Kufr (disbelief) is the abandoning of As-Salat (prayers)." [Sahih Muslim, Hadith No. 82 (S.S.M. 204)]

Kutoka kwa Jabir bin Abdullah (r. a) amemsikia Mtume swalla aallahu alayhi wa sallamu akisema hakika baina ya muislamu anayemwamini Allah na mshirikina anayeamini miungu wengi na kafiri ni kuacha Salah / swala

Ndugu katika imani hakika sala ndio nguzo ya dini, tushikamane nayo ili tupate mwisho mwema
 
Skip to main content
slogan_mobile.png

Ukurasa Wa Kwanza

Search form​

Ukurasa Wa Kwanza /Fadhila Na Faida Za Qiyaamul-Layl

Fadhila Na Faida Za Qiyaamul-Layl​

Swalah

Fadhila Za Qiyaamul-Layl
(Kisimamo Cha Kuswali Usiku)

Alhidaaya.com

Muislamu anapaswa asikose Qiyaamul-Layl khasa katika mwezi wa Ramadhwaan kwa sababu ya Hadiyth ya Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam):

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: ((مَنْ قَامَ رَمَضَانَ إِيمَانًا وَاحْتِسَابًا غُفِرَ لَهُ مَا تَقَدَّمَ مِنْ ذَنْبِهِ)) رواه البخاري 37 ومسلم 759
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: (Atakayesimama kuswali Ramadhwaan kwa iymaan na kutaraji malipo, ataghufuriwa madhambi yake yaliyotangulia) [Al-Bukhaariy na Muslim]

Al-Haafidh Ibn Rajab (Rahimahu Allaah) amesema: "Tambua kuwa Muumini anajumuisha katika mwezi wa Ramadhwaan jihaad mbili kwa ajili ya nafsi yake; jihaad ya mchana ya kufunga, na jihaad ya usiku kwa kusimama (kuswali), atakayejumuisha jihaad hizi mbili atapata ujira wake bila ya hesabu".

Ibn 'Uthaymiyn (Rahimahu Allaah) amesema: "Haimpasi Muislamu kuepukana na Swalaah ya Tarawiyh katika Ramadhwaan ili apate thawabu na ujira wake, na wala asiondoke mpaka Imaam amalize Swalaah ya Witr ili apate ujira kamili wa Qiyaamul-Layl".

Ili kuipata ladha ya Ramadhwaan na kuongeza utiifu, ni muhimu Muislamu ajumuike na Waislamu wenzie kuswali Tarawiyh asikilize Qur-aan inaposomwa katika Swalaah hizi kwa sababu itampatia utulivu wa moyo na pia atajichumia thawabu adhimu zinazopatikana katika kisimamo hiki kinachofuta madhambi kama ilivyotajwa katika Hadiyth iliyotangulia.

Fadhila Nyenginezo Za Qiyaamul-Layl:

1-Qiyaamul-Layl ilikuwa ni amri ya Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) kwa Rasuli Wake (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Waumini wakatekeleza:

يَا أَيُّهَا الْمُزَّمِّلُ﴿١﴾ قُمِ اللَّيْلَ إِلَّا قَلِيلًا﴿٢﴾ نِّصْفَهُ أَوِ انقُصْ مِنْهُ قَلِيلًا﴿٣﴾ أَوْ زِدْ عَلَيْهِ وَرَتِّلِ الْقُرْآنَ تَرْتِيلًا﴿٤﴾

Ee mwenye kujigubika! Simama na uonye. Na Rabb wako mtukuze. Na nguo zako toharisha. [Al-Muzzammil 1-4]

Na pia Amemuamrisha tena Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam):

أَقِمِ الصَّلَاةَ لِدُلُوكِ الشَّمْسِ إِلَىٰ غَسَقِ اللَّيْلِ وَقُرْآنَ الْفَجْرِ ۖ إِنَّ قُرْآنَ الْفَجْرِ كَانَ مَشْهُودًا ﴿٧٨﴾ وَمِنَ اللَّيْلِ فَتَهَجَّدْ بِهِ نَافِلَةً لَّكَ عَسَىٰ أَن يَبْعَثَكَ رَبُّكَ مَقَامًا مَّحْمُودًا ﴿٧٩﴾
Simamisha Swalaah jua linapopinduka hadi kiza cha usiku na Qur-aan ya (Swalaah ya) Alfajiri. Hakika Qur-aan ya Alfajiri ni yenye kushuhudiwa. Na katika usiku, amka uswali (tahajjud) kuisoma (Qur-aan); ni ziada ya Sunnah kwako Asaa Rabb wako Akakuinua cheo kinachosifika. [Al-Israa: 78-79]

Mujaahid amesema: "Qiyaam kwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ni naafilah (Sunnah ya ziada) kwa sababu ameshafutiwa madhambi yake yaliotangulia na ya mbele. Na kwa Ummah wa Kiislamu, Swalaah ya Qiyaamul-Layl huenda pia ikamfutia mtu madhambi yake atakayotenda". [Atw-Twabariy 17:525]

Anasema tena Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

فَاصْبِرْ عَلَىٰ مَا يَقُولُونَ وَسَبِّحْ بِحَمْدِ رَبِّكَ قَبْلَ طُلُوعِ الشَّمْسِ وَقَبْلَ الْغُرُوبِ﴿٣٩﴾وَمِنَ اللَّيْلِ فَسَبِّحْهُ وَأَدْبَارَ السُّجُودِ﴿٤٠﴾

Subiri juu ya yale wanayoyasema, na sabbih kwa Himidi za Rabb wako kabla ya kuchomoza jua na kabla ya kuchwa. Na katika usiku Msabbih na baada ya kusujudu. [Qaaf: 39-40]

Na:
وَاذْكُرِ اسْمَ رَبِّكَ بُكْرَةً وَأَصِيلًا﴿٢٥﴾ وَمِنَ اللَّيْلِ فَاسْجُدْ لَهُ وَسَبِّحْهُ لَيْلًا طَوِيلًا﴿٢٦﴾

Na lidhukuru Jina la Rabb wako asubuhi na jioni. Na katika usiku msujudie na uswali kwa ajili Yake usiku mrefu. [Al-Insaan: 25-26]

2-Qiyaamul-Layl ni njia mojawapo ya kumshukuru Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

Kumshukuru Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) sio kwa kutamka tu bali kwa kukiri moyoni na kwa matendo. Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akisimama usiku kuswali mpaka miguu yake ilikuwa ikivimba:

عَنْ عَائِشَةَ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهَا: أَنَّ نَبِيَّ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ كَانَ يَقُومُ مِنَ اللَّيْلِ حَتَّى تَتَفَطَّرَ قَدَمَاهُ، فَقَالَتْ عَائِشَةُ: لِمَ تَصْنَعُ هَذَا يَا رَسُولَ اللَّهِ، وَقَدْ غَفَرَ اللَّهُ لَكَ مَا تَقَدَّمَ مِنْ ذَنْبِكَ وَمَا تَأَخَّرَ؟ قَالَ: (أَفَلاَ أُحِبُّ أَنْ أَكُونَ عَبْدًا شَكُورًا) متفق عليه

Imepokelewa kutoka kwa ‘Aaishah (Radhwiya Allaahu ‘anhaa) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akisimama usiku hadi ikivimba miguu yake, nikamwambia: “Kwa nini unafanya hivi ee Rasuli wa Allaah na hali umefutiwa madhambi yako yaliyotangulia na yatakayofuatia?” Akasema: (Je, nisiwe mja mwenye kushukuru?) [Al-Bukhaariy na Muslim]

3-Qiyaamul-Layl ni Swalaah bora kabisa baada ya Swalaah ya fardhi kwa kauli ya Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam):

(أَفْضَلُ الصَّلاةِ بَعْدَ الْفَرِيضَةِ صَلاةُ اللَّيْلِ) رواه مسلم.

((Swalaah iliyo bora kabisa baada ya fardhi ni Swalaah ya usiku)) [Muslim]

4-Qiyaamul-Layl ni kufuata na kufufua Sunnah ya Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam)

Na pia Qiyaamul-Layl ilikuwa ni desturi ya Salaf na sababu kuu ya kumzidishia Muislamu iymaan yake na kumtakasa moyo kutokana na maovu mengi; uasi, unafiki, chuki, uhasidi n.k. Pia nyoyo hupata utulivu na huelekea kwa yanayomridhisha Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa). Hadiyth ifuatayo imethibiti:

عن بلال، أن رسول الله صلى الله عليه وسلم قال: عليكُم بقيامِ اللَّيلِ ، فإنَّهُ دَأْبُ الصَّالِحينَ قبلَكُم ، و قُربةٌ إلى اللهِ تعالى ومَنهاةٌ عن الإثمِ و تَكفيرٌ للسِّيِّئاتِ ، ومَطردةٌ للدَّاءِ عن الجسَدِ

Amesimulia Bilaal (رضي الله عنه): Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Shikamaneni na Qiyaamul-Layl (kuswali usiku) kwani ni desturi za Swalihina (waja wema) kabla yenu, na kujikurubisha kwa Allaah, na inazuia madhambi, inafuta maovu na inaondosha maradhi mwilini.” [Ahmad na At-Tirmidhiy na ameisahihisha Al-Albaaniy katika Swahiyh Al-Jaami (4079)]

‘Umar (Radhwiya Allaahu 'anhu) alikuwa akipitia usiku akisikia kisomo cha Qiyaamul-Layl, akazimia siku moja yakapita masiku akiugua hadi akapona [Munswaf Ibn Abiy Shaybah]

Na yamemthibiti mengi kuhusiana na hali za Salaf kusimama kwao usiku kuswali.

5-Qiyaamul-Layl ni kujikurubisha kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

عن عَمْرُو بْنُ عَبَسَةَ، أَنَّهُ سَمِعَ النَّبِيَّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، يَقُولُ: ((أَقْرَبُ مَا يَكُونُ الرَّبُّ مِنَ العَبْدِ فِي جَوْفِ اللَّيْلِ الآخِرِ، فَإِنْ اسْتَطَعْتَ أَنْ تَكُونَ مِمَّنْ يَذْكُرُ اللَّهَ فِي تِلْكَ السَّاعَةِ فَكُنْ)) الترمذي هَذَا حَدِيثٌ حَسَنٌ صَحِيحٌ

Imepokelewa kutoka kwa 'Amru bin 'Abasah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba kamsikia Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: ((Wakati Allaah Anakuwa karibu kabisa na mja, ni wakati wa mwisho wa usiku, kwa hiyo ukiweza kuwa miongoni mwa wanaomdhukuru Allaah katika saa hiyo basi uwe)) [At-Tirmidhy ameisahihisha Al-Albaaniy katika Swahiyh At-Tirmidhiy (3579), Swahiyh Al-Jaami’ (1173)]

6-Qiyaamul-Layl ni kujikinga na maovu ya shaytwaan:

عَنْ عَبْدِ اللَّهِ بن مسعود رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ، قَالَ: ذُكِرَ عِنْدَ النَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ رَجُلٌ، فَقِيلَ: مَا زَالَ نَائِمًا حَتَّى أَصْبَحَ، مَا قَامَ إِلَى الصَّلاَةِ، فَقَالَ: ((ذَاكَ رَجُلٌ بَالَ الشَّيْطَانُ فِي أُذُنِهِ)) روى البخاري (1144) ومسلم (774) والنسائي (1608) وابن حبان (2562)

Imepokelewa kutoka kwa ‘Abdullaah bin Mas’-uwd (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba ilitajwa kwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kwamba kuna mtu alilala usiku wote hadi asubuhi bila kuswali, Akasema: ((Huyo ni mtu aliyekojolewa na Shaytwaan katika masikio yake)) [Al-Bukhaariy, Muslim, An-Nasaaiy, Ibn Hibbaan]

‘Ulamaa wamekhitilafiana kusudio la kauli: “mtu alilala usiku wote hadi asubuhi bila kuswali”. Wakataj wengine kuwa ni Swalaah ya fardhi na wengine wakaona ni Qiyaamul-Layl.

7-Wanaoswali Qiyaamul-Layl wameandaliwa Jannah:

Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Anasema:

تَتَجَافَىٰ جُنُوبُهُمْ عَنِ الْمَضَاجِعِ يَدْعُونَ رَبَّهُمْ خَوْفًا وَطَمَعًا وَمِمَّا رَزَقْنَاهُمْ يُنفِقُونَ ﴿١٦﴾ فَلَا تَعْلَمُ نَفْسٌ مَّا أُخْفِيَ لَهُم مِّن قُرَّةِ أَعْيُنٍ جَزَاءً بِمَا كَانُوا يَعْمَلُونَ ﴿١٧﴾

Mbavu zao zinatengana na vitanda, wanamuomba Rabb wao kwa khofu na matumaini, na katika yale Tuliyowaruzuku wanatoa. Basi nafsi yoyote haijui yaliyofichiwa katika yanayoburudisha macho. Ni jazaa kwa yale waliyokuwa wakiyatenda. [As-Sajdah: 16-17]

Aayah hizo tukufu zinambashiria Muumini Jannah pindi atakapojitahidi kuamka kuswali usiku pamoja na kutoa mali yake katika njia ya Allaah. Huko Jannah, kuna neema za kufurahisha zenye kudumu milele ambazo hajapatapo mtu kuona wala kusikia wala kuwaza kama ilivyotajwa katika Hadiyth Al-Qudsiy:

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ عَنْ رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: ((قَالَ اللَّهُ تَبَارَكَ وَتَعَالَى: أَعْدَدْتُ لِعِبَادِي الصَّالِحِينَ مَا لَا عَيْنٌ رَأَتْ وَلَا أُذُنٌ سَمِعَتْ وَلَا خَطَرَ عَلَى قَلْبِ بَشَرٍ)) قَالَ أَبُو هُرَيْرَةَ اقْرَءُوا إِنْ شِئْتُمْ: (( فَلَا تَعْلَمُ نَفْسٌ مَا أُخْفِيَ لَهُمْ مِنْ قُرَّةِ أَعْيُنٍ)) البخاري، مسلم، الترمذي وابن ماجه

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Allaah Tabaaraka wa Ta’aalaa Amesema: Nimewatayarishia waja Wangu wema kile ambacho jicho lolote halijapata kuona na sikio lolote halijapata kusikia na wala haijapata kupita katika moyo wa binaadamu)) Akasema Abuu Hurayrah: Kwa hivyo, soma ukitaka:
فَلَا تَعْلَمُ نَفْسٌ مَا أُخْفِيَ لَهُمْ مِنْ قُرَّةِ أَعْيُنٍ
Basi nafsi yoyote haijui yaliyofichiwa katika yanayoburudisha macho. [As-Sajdah:17] [Al-Bukhaariy, Muslim, At-Tirmidhiy na Ibn Maajah]

Na Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Ametaja pia kuhusu wanaoamka kuswali usiku:

إِنَّ الْمُتَّقِينَ فِي جَنَّاتٍ وَعُيُونٍ﴿١٥﴾ آخِذِينَ مَا آتَاهُمْ رَبُّهُمْ ۚ إِنَّهُمْ كَانُوا قَبْلَ ذَٰلِكَ مُحْسِنِينَ﴿١٦﴾ كَانُوا قَلِيلًا مِّنَ اللَّيْلِ مَا يَهْجَعُونَ﴿١٧﴾ وَبِالْأَسْحَارِ هُمْ يَسْتَغْفِرُونَ﴿١٨﴾ وَفِي أَمْوَالِهِمْ حَقٌّ لِّلسَّائِلِ وَالْمَحْرُومِ﴿١٩﴾

Hakika wenye taqwa watakuwa katika Jannaat na chemchem. Wakichukua yale Atakayowapa Rabb wao. Hakika wao walikuwa kabla ya hapo ni wahisani. Walikuwa kidogo tu katika usiku wakilala kwa raha. Na kabla ya Alfajiri wakiomba maghfirah. Na katika mali zao kuna haki maalum kwa mwenye kuomba na asiyeomba. [Adh-Dhaariyaat: 15-19]

Na pia Hadiyth ya Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam):

عَنْ عَلِيٍّ قَالَ : قَالَ النَّبِيُّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ : ((إِنَّ فِي الْجَنَّةِ غُرَفًا تُرَى ظُهُورُهَا مِنْ بُطُونِهَا، وَبُطُونُهَا مِنْ ظُهُورِهَا، فَقَامَ أَعْرَابِيٌّ فَقَالَ : لِمَنْ هِيَ يَا رَسُولَ اللَّهِ ؟ قَالَ : ((لِمَنْ أَطَابَ الْكَلامَ وَأَطْعَمَ الطَّعَامَ ، وَأَدَامَ الصِّيَامَ ، وَصَلَّى لِلَّهِ بِاللَّيْلِ وَالنَّاسُ نِيَامٌ )) وحسنه الألباني في صحيح الترمذي .

Imepokelewa kutoka kwa ‘Aliy (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Hakika katika Jannah kuna nyumba ambazo nje yake huonekana ndani na ndani yake huonekana nje)) Bedui mmoja akasimama na kusema: “Ee Rasuli wa Allaah kwa ajili ya nani hizo?”. Akasema: ((Kwa ajili ya wanaotamka maneno mazuri, wanaolisha watu chakula, wenye kudumisha swiyaam, na wenye kuswali usiku wakati watu wengine wamelala)) [At-Tirmidhiy na ameisahihisha Al-Albaaniy katika Swahiyh At-Tirmidhiy (1984)]

8-Qiyaamul-Layl ni miongoni mwa sifa za waja wa Ar-Rahmaan:

Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

وَعِبَادُ الرَّحْمَـٰنِ الَّذِينَ يَمْشُونَ عَلَى الْأَرْضِ هَوْنًا وَإِذَا خَاطَبَهُمُ الْجَاهِلُونَ قَالُوا سَلَامًا ﴿٦٣﴾ وَالَّذِينَ يَبِيتُونَ لِرَبِّهِمْ سُجَّدًا وَقِيَامًا ﴿٦٤﴾

Na waja wa Ar-Rahmaan ni wale wanaotembea katika ardhi kwa unyenyekevu na upole, na majahili wanapowasemesha, wao husema: Salaam! Na wale wanaokesha usiku kwa ajili ya Rabb wao wakisujudu na kusimama. [Al-Furqaan: 63-64]

9-Wanaoswali Qiyaamul-Layl si sawa na watu wengine.

Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

لَيْسُوا سَوَاءً ۗ مِّنْ أَهْلِ الْكِتَابِ أُمَّةٌ قَائِمَةٌ يَتْلُونَ آيَاتِ اللَّـهِ آنَاءَ اللَّيْلِ وَهُمْ يَسْجُدُونَ ﴿١١٣﴾

Hawako sawa sawa; miongoni mwa Ahlil-Kitaabi wako watu wenye kusimama (kwa utiifu) wanasoma Aayaat za Allaah nyakati za usiku na wao wanasujudu (katika Swalaah). [Aal-'Imraan: 113]

Na Anasema pia Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

أَمَّنْ هُوَ قَانِتٌ آنَاءَ اللَّيْلِ سَاجِدًا وَقَائِمًا يَحْذَرُ الْآخِرَةَ وَيَرْجُو رَحْمَةَ رَبِّهِ ۗ قُلْ هَلْ يَسْتَوِي الَّذِينَ يَعْلَمُونَ وَالَّذِينَ لَا يَعْلَمُونَ ۗ إِنَّمَا يَتَذَكَّرُ أُولُو الْأَلْبَابِ ﴿٩﴾

Je, yule aliye mtiifu nyakati za usiku akisujudu, au akisimama (kuswali), anatahadhari na Aakhirah na anataraji rahmah ya Rabb wake (ni sawa na aliyekinyume chake?). Sema: Je, wanalingana sawa wale wanaouja na wale wasiojua? Hakika wanakumbuka wenye akili tu. [Az-Zumar: 9]

10-Qiyaamul-Layl ni kughufuriwa madhambi.

Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) kwa wanaoswali thuluthi ya mwisho ya usiku:

الصَّابِرِينَ وَالصَّادِقِينَ وَالْقَانِتِينَ وَالْمُنفِقِينَ وَالْمُسْتَغْفِرِينَ بِالْأَسْحَارِ﴿١٧﴾

Wenye kusubiri na wasemao kweli, na watiifu, na watoaji mali katika njia ya Allaah na waombao maghfirah kabla ya Alfajiri. [Aal-‘Imraan: 17]

Na katika Hadiyth Al-Qudsiy:

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: ((يَنْزِلُ رَبُّنَا تَبَارَكَ وَتَعَالَى كُلَّ لَيْلَةٍ إِلَى السَّمَاءِ الدُّنْيَا حِينَ يَبْقَى ثُلُثُ اللَّيْلِ الْآخِرُ يَقُولُ: مَنْ يَدْعُونِي فَأَسْتَجِيبَ لَهُ، مَنْ يَسْأَلُنِي فَأُعْطِيَهُ، مَنْ يَسْتَغْفِرُنِي فَأَغْفِرَ لَهُ)) البخاري و مسلم

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Allaah Tabaaraka wa Ta’aalaa Huteremka (kwa namna inavyolingana na utukufu Wake) kila siku katika mbingu ya dunia inapobakia thuluthi ya mwisho ya usiku na Husema: Nani ananiomba du’aa Nimuitike? Nani Ananiomba jambo Nimpe? Nani ananiomba maghfirah Nimghufurie?)) [Al-Bukhaariy, Muslim]

11-Mwenye kuswali Qiyaamul-Layl hujaaliwa siha katika mwili wake.

Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amemsema:

((عليكُم بقيامِ اللَّيلِ ، فإنَّهُ دَأْبُ الصَّالِحينَ قبلَكُم ، و قُربةٌ إلى اللهِ تعالى ومَنهاةٌ عن الإثمِ و تَكفيرٌ للسِّيِّئاتِ ، ومَطردةٌ للدَّاءِ عن الجسَدِ))

((Shikamaneni na Qiyaamul-Layl (kuswali usiku) kwani ni desturi za waja wema kabla yenu, na kujikurubisha kwa Allaah Ta’aalaa, na inazuia madhambi, inafuta maovu na inaondosha maradhi mwilini)) [Ahmad na At-Tirmidhiy na ameisahihisha Al-Albaaniy katika Swahiyh Al-Jaami (4079)]

12-Nyakati za Qiyaamul-Layl ni nyakati za kutakabaliwa du’aa:

عَنْ جَابِرٍ قَالَ : سَمِعْتُ النَّبِيَّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يَقُولُ: ((إِنَّ فِي اللَّيْلِ لَسَاعَةً لَا يُوَافِقُهَا رَجُلٌ مُسْلِمٌ يَسْأَلُ اللَّهَ خَيْرًا مِنْ أَمْرِ الدُّنْيَا وَالْآخِرَةِ إِلَّا أَعْطَاهُ إِيَّاهُ وَذَلِكَ كُلَّ لَيْلَةٍ)) مسلم

Imepokelewa kutoka kwa Jaabir (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba kamsikia Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: ((Hakika katika usiku kuna saa ambayo mja anapomuomba Allaah kheri katika mambo ya dunia au Aakhirah ila (Allaah) Humpa kheri hizo, na hivyo ni kila usiku)) [Muslim]

13-Kuswali Qiyaamul-Layl ni utukufu wa Muumini:

عنْ سهل بن سعد الساعدي عن النَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم: ((أتاني جبريلُ ، فقال : يا مُحمَّدُ! عِشْ ما شِئتَ فإنَّك مَيِّتٌ، وأحْبِبْ من شِئتَ فإنَّكَ مُفارِقُه، واعمَل ما شِئتَ فإنَّك مَجْزِيٌّ بهِ، واعلَم أنَّ شرفَ المؤمنِ قيامُه باللَّيلِ، وعِزُّه استِغناؤُه عن النَّاسِ)) رواه الحاكم والبيهقي وحسنه المنذري والألباني

Imepokelewa kutoka kwa Sahl bin Sa’d As-Saa’idiy kutoka kwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Amenijia Jibriyl akasema: Ee Muhammad ishi upendavyo bila shaka wewe utakuwa maiti, na mpende umtakaye bila shaka utafarikiana naye, na tenda unavyopenda lakini ujue utalipwa kwa vitendo hivyo, na tambua kwamba utukufu wa Muumin ni Qiyaamul-Layl, na heshima yake ni kujitosheleza na watu)) [Hadiyth imepokelewa pia kutoka kwa Jaabir na ‘Aliy Radhwiya Allaahu ‘anhumaa - Al-Haakim na Al-Bayhaqiy, na Al Mundhiriy na Al-Abaaniy wamesema ni Hadiyth Hasan – As-Silsilah Asw-Swahiyhah (831)]

14-Qiyaamul-Layl ni kupata husnul-khaatimah (mwisho mwema)

عبدالله بن عمرو عن النبي صلى الله عليه وسلم ((من قام بعشرِ آياتٍ لم يُكتبْ من الغافلينَ ، ومن قام بمئةِ آيةٍ كُتبَ من القانتينَ ومن قام بألفِ آيةٍ كُتبَ من المُقَنْطِرينَ)) صحيح أبي داود

Amesimulia ‘Abdullaah bin ‘Amr (رضي الله عنه): Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Atakayesimama usiku kuswali na akasoma Aayah kumi, hatoandikiwa kuwa miongoni mwa walioghafilika, na atakayesimama kuswali akasoma Aayah mia, ataandikiwa ni miongoni mwa watiifu, na atakayesimama kuswali akasoma Aayah elfu, ataandikwa miongoni mwa wenye mirundi (ya thawabu).’ [Abuu Daawuwd, Al-Albaaniy ameisahihisha: Swahiyh Abiy Daawuwd (1398), Swahiyh Al-Jaami’ (6439)]

15-Nyuso za wanaoswali Qiyaamul-Layl hun’gaa kwa Nuru:

Hasan Al-Baswriy (Rahimahu Allaah) amesema:

"ما نعلم شيئًا أَشَدَّ من مكابدة اللَّيل ونفقة هذا المال" فقيل : ما بالُ المتهجِّدين من أحسن الناس وجوهًا ؟ قال : "لأنهم خلوا بالرحمن فألبسهم نورًا من نوره" إحياء علوم الدين
"Sijapata kuona ‘ibaadah iliyo nzito kama Swalaah katika kiza cha usiku na kutoa kwake mali". Akaulizwa: “Mbona wale Mutahajjudiyn (wanaoamka usiku kuswali) nyuso zao ni nzuri kabisa?” Akajibu: "Kwa sababu wamejiweka faragha na Ar-Rahmaan, basi Naye Akawavisha Nuru Yake". [Ihyaa ‘Uluwm Ad-Diyn]

Baadhi Ya Yatakayomwezesha Muislamu Qiyaamul-Layl

1-Kuwa na ikhlaasw katika ‘amali.

2-Kutafakari Hadiyth ya Al-Qudsiy kwamba Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Anateremka thuluthi ya mwisho kuwakidhia Waislamu haja zao. Nani asiyekuwa na haja, nani asiyekuwa na madhambi ya kughufuriwa? Asiyejihimiza kuamka usiku ni kama kwamba hamhitaji Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Amtakakbalie haja zake na Amghufurie dhambi zake!

3-Kutambua fadhila za Qiyaamul-Layl.

4-Kulala katika twahaarah, yaani kutia wudhuu kabla ya kulala.

5-Kusoma nyiradi za usiku na kumuomba sana Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) tawfiyq ya kuamka usiku.

6-Kulala mapema

7-Kutokula sana mpaka mtu akashiba mno.

8-Kutokujitaabisha sana mchana khasa kwa mambo ya kidunia.

9-Usiache 'Qaylulah' (kulala kidogo mchana) kwa sababu ni Sunnah na inamsaidia mtu kumpa nguvu za kuamka usiku.

10-Kutokutenda maasi kwani yanamzuia mtu kutotimiza ‘ibaadah vizuri.

11-Kuutakasa moyo kutokana na maradhi ya moyo; uhasidi, chuki, uadui, ghiybah (kusengenya), an-namiymah (kufitinisha) na kila maovu.

12-Kutafakari mauti na kutokuwa na matumaini ya umri mrefu.

WabiLLaahit-Tawfiyq

KWA HISANI YA ALHIDAAYA. COM

lj_match
 
Udhibitisho wa uwepo wa adhabu ya Kaburi

Narrated Ibn 'Abbas [radhi-yAllahu 'anhu]: Allah's Messenger (ﷺ) passed by two graves and said, "Both of them (persons in the grave) are being tortured, and they are not being tortured for a major sin. This one used not to save himself from being soiled with his urine, and the other used to go about with calumnies (among the people to rouse hostilities, e.g., one goes to a person and tells him that so-and-so says about him such and such evil things)." The Prophet (ﷺ) then asked for a green branch of a date palm tree, split it into two pieces and planted one on each grave and said, "It is hoped that their punishment may be abated till those two pieces of the branch get dried."*** [Sahih Al-Bukhari, 8/6052 (O.P.78)]

Kutoka kwa ibn Abbas (r. a) Mtume swalallahu aallahu slather wassalamu alipita Katina makaburi mawili na kusema hawa wote wanaadhibiwa na si kwa makosa makubwa. Huyu mmoja alikuwa hajizuii kurukiwa na chembe za mkojo na huyu mwingine alikuwa mfitinishaji, anatoa maneno huku na kuyapeleka huyu kwa lengo la kugombanisha watu.

Ndugu zangu adhabu ya kaburi ipo ikiwa hayo makosa madogo watu wanaadhibiwa vipi kwa wenye kufanya madhambi makubwa?

Allah anapenda watu ambao wapo tohara mda wote, wanawake kwa asili yao hawana shida kwakuwa hujisaidia wakiwa wamechuchumaa hivyo huepuka kujirushia chembe za mikojo Katika miili yao na nguo zao.

Kazi ipo kwa wanaume,,, mwanaume ili uwe salama hakikisha unachuchumaa wakati wa kukojoa na maliza mkojo ktk mrija kwa kupangusa kiganja chako toka ktk kende zako kupandisha ktk uume wako, au unaweza kujikohoza kidogo, fanya uwezavyo kuhakikisha kuwa mkojo umekata wote, usiwe na papara ya kutoka chooni haraka, wengi wetu hatuko makini na hili hatimaye hata swala zetu ni mtihani.

Wanawake wao hawana tabu baada ya kujisaidia akikaa sekunde chache mkojo unakata na kujisafisha na maji.

Wanaume kwetu tuna changamoto kidogo tulia na hakikisha umemaliza mpaka tone la mwisho kisha jisafishe na maji uwe tohara.

Uislamu ni Usafi.
 
Skip to main content
slogan_mobile.png

Ukurasa Wa Kwanza

Search form​

Ukurasa Wa Kwanza /Ramadhwaan Ni Mwezi Wa Du’aa Na Du’aa Hutakabaliwa

Ramadhwaan Ni Mwezi Wa Du’aa Na Du’aa Hutakabaliwa​

Ramadhaan-Swawm

Ramadhwaan Ni Mwezi Wa Du’aa Na Du’aa Hutakabaliwa

Alhidaaya.com

Du’aa ni ‘ibaadah kama ilivyothibiti katika Hadiyth:

عَنِ النُّعْمَانِ بْنِ بَشِيرٍ (رضي الله عنه) عَنْ النَّبِيِّ (صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ) فِي قَوْلِهِ ((وَقَالَ رَبُّكُمُ ادْعُونِي أَسْتَجِبْ لَكُمْ)) قَالَ: ((الدُّعَاءُ هُوَ الْعِبَادَةُ)) وَقَرَأَ ((وَقَالَ رَبُّكُمُ ادْعُونِي أَسْتَجِبْ لَكُمْ)) إِلَى قَوْلِهِ: ((دَاخِرِينَ))
Amesimulia Nu’maan bin Bashiyr (رضي الله عنه) kwamba Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) kuhusu kauli yake [Allaah Subhaanahu wa Ta’aalaa]:
وَقَالَ رَبُّكُمُ ادْعُونِي أَسْتَجِبْ لَكُمْ
((Na Rabb wenu Amesema: “Niombeni, Nitakuitikieni))

Amesema: ((Du’aa ndio ‘ibaadah)) kisha akasoma:

وَقَالَ رَبُّكُمُ ادْعُونِي أَسْتَجِبْ لَكُمْ ۚ إِنَّ الَّذِينَ يَسْتَكْبِرُونَ عَنْ عِبَادَتِي سَيَدْخُلُونَ جَهَنَّمَ دَاخِرِينَ﴿٦٠﴾
Na Rabb wenu Amesema: Niombeni, Nitakuitikieni. Hakika wale wanaotakabari katika kuniabudu wataingia Jahanam wadhalilike. [Ghaafir: 60] [Abu Daawuwd, At-Tirmidhiy, Ibn Maajah, Ahmad – Hadiyth Hasan Swahiyh]

Juu ya hivyo, du’aa ni ‘amali tukufu kabisa mbele ya Allaah (سبحانه وتعالى):

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ (رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ) عَنْ النَّبِيِّ (صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ) قَالَ: ((لَيْسَ شَيْءٌ أَكْرَمَ عَلَى اللَّهِ تَعَالَى مِنْ الدُّعَاءِ))
Kutoka kwa Abu Hurayrah (رضي الله عنه) kwamba Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: ((Hakuna kitu kitukufu mbele ya Allaah kama du’aa)) [Swahiyh Adab Al-Mufrad]

Na Allaah (سبحانه وتعالى) Ameiadhimisha ‘amali ya kuomba du’aa khasa katika mwezi wa Ramadhwaan kwa sababu zifuatazo:

1-Aayah ya amrisho la kumuomba du’aa Allaah (سبحانه وتعالى) imo baina ya Aayaat za Swiyaam Mwezi wa Ramadhwaan. Imeanza Aayah namba 183 mpaka Aayah namba 185 kisha ikaja kauli Yake (سبحانه وتعالى):

وَإِذَا سَأَلَكَ عِبَادِي عَنِّي فَإِنِّي قَرِيبٌ ۖ أُجِيبُ دَعْوَةَ الدَّاعِ إِذَا دَعَانِ ۖ فَلْيَسْتَجِيبُوا لِي وَلْيُؤْمِنُوا بِي لَعَلَّهُمْ يَرْشُدُونَ ﴿١٨٦﴾
Na watakapokuuliza waja Wangu kuhusu Mimi, basi Mimi ni Niko karibu (kwa ujuzi); Naitikia du’aa ya muombaji anaponiomba. Basi waniitikie Mimi na waniamini Mimi, wapate kuongoka. [Al-Baqarah: 186]

Kisha ikaendelea kuhusu Swiyaam:

أُحِلَّ لَكُمْ لَيْلَةَ الصِّيَامِ الرَّفَثُ إِلَىٰ نِسَائِكُمْ ۚ ….
Mmehalalishiwa usiku wa kufunga Swiyaam kujamiiana na wake zenu…. [Al-Baqara: 187]

2-Du’aa ya mwenye Swawm hairudishwi bali inatakabaliwa:

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ (رضي الله عنه) قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ (صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ): ((ثَلاَثَةٌ لاَ تُرَدُّ دَعْوَتُهُمْ، الإِمَامُ الْعَادِلُ، وَالصَّائِمُ حَتَّى يُفْطِرَ، وَدَعْوَةُ الْمَظْلُومِ يَرْفَعُهَا اللَّهُ دُونَ الْغَمَامِ يَوْمَ الْقِيَامَةِ وَتُفْتَحُ لَهَا أَبْوَابُ السَّمَاء،وَيَقُولُ بِعِزَّتِي لأَنْصُرَنَّكِ وَلَوْ بَعْدَ حِينٍ))
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Hurayrah (رضي الله عنه) ambaye amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: (([Watu] Watatu hazirudishwi du'aa zao; Imaam (kiongozi) muadilifu, mwenye Swawm mpaka afuturu, na du'aa ya aliyedhulumiwa, Anainyanyua Allaah bila ya mawingu Siku ya Qiyaamah na inafunguliwa milango ya mbingu na Anasema: “Kwa Utukufu Wangu, Nitakunusuru japo baada ya muda.)) [Swahiyh At-Tirmidhiy (2526) Ibn Maajah, Ahmad]

Pia katika Hadiyth:

عّنْ أَنسْ بِنْ ماَلِكْ (رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ): ((ثَلاَثُ دَعْواتِ لاَ تُرَدُّ: دَعْوَةُ الْوَالِدِ لِوَلَدِهِ، وَدَعْوَةُ الصَّائِم، وَدَعْوَةُ الْمُسَافَرَ))
Kutoka kwa Anas bin Maalik (رضي الله عنه) ((Du’aa za watatu hazirudishwi; du’aa ya mzazi kwa mwanawe, na du’aa ya mwenye Swawm, na du’aa ya msafiri)) [Al-Bayhaqiy katika Swahiyh Al-Jaami’ (3032) na katika Asw-Swahiyhah (1797)]

3-Muislamu anapaswa aombe du’aa kwa wingi katika Ramadhwaan kujikinga na Moto wa Jahannam na kuomba Jannah (Pepo), kwa sababu milango ya Moto inafungwa na milango ya Jannah inafunguliwa na mashaytwaan wanafungwa minyororo:

عن أبي هُرَيْرَةَ (رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ) قال: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ (صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ): ((إِذَا دَخَلَ رَمَضَانُ فُتِّحَتْ أَبْوَابُ الْجَنَّةِ وَغُلِّقَتْ أَبْوَابُ جَهَنَّمَ وَسُلْسِلَتْ الشَّيَاطِينُ))
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Hurayrah (رضي الله عنه) kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: ((Inapoingia Ramadhwaan, milango ya Jannah hufunguliwa, milango ya Moto wa Jahannam hufungwa na mashaytwaan hufungwa minyororo)) [Al-Bukhaariy, An-Nasaaiy]

Pia mwenye Swawm Ramadhwaan ameahidiwa kughufuriwa madhambi yake pindi akifunga kwa iymaan na akataraji malipo:

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ قَالَ قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ : مَنْ صَامَ رَمَضَانَ إِيمَانًا وَاحْتِسَابًا غُفِرَ لَهُ مَا تَقَدَّمَ مِنْ ذَنْبِهِ رواه البخاري ، ومسلم (.

Kutoka kwa Abuu Hurayrah (رضي الله عنه) ambaye amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Atakayefunga Ramadhwaan kwa Iymaan na kutaraji malipo ataghufuriwa madhambi yake yaliyotangulia.” [Al-Bukhaariy, Muslim]

4-Kuomba du’aa kila usiku wa Ramadhwaan kujaaliwa kuwa miongoni mwa watakaoepushwa na Moto kwa sababu kila inapofika usiku, kuna waja ambao Allaah (سبحانه وتعالى) Anawajaalia kuwa ni wenye kuepushwa na Moto:

عَنْ جَابِرٍ رضي الله عنه قَالَ : قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ : ( إِنَّ لِلَّهِ عِنْدَ كُلِّ فِطْرٍ عُتَقَاءَ ، وَذَلِكَ فِي كُلِّ لَيْلَةٍ ) . رواه أحمد (21698) وابن ماجه ( 1643 ) . وصححه الشيخ الألباني في " صحيح ابن ماجه " .
Imepokelewa kutoka kwa Jaabir (رضي الله عنه) kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Hakika katika baada ya kufuturu (Magharibi kuendelea), Allaah Ana watu wa kuwaepusha na Moto, na hivyo ni katika kila usiku.” [Ibn Maajah na ameisahihisha Imaam Al-Albaaniy katika Swahiyh Ibn Maajah (1340)]

Na pia,

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رضي الله عنه قَالَ : قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ : ( إِذَا كَانَ أَوَّلُ لَيْلَةٍ مِنْ شَهْرِ رَمَضَانَ صُفِّدَتْ الشَّيَاطِينُ ، وَمَرَدَةُ الْجِنِّ ، وَغُلِّقَتْ أَبْوَابُ النَّارِ ، فَلَمْ يُفْتَحْ مِنْهَا بَابٌ ، وَفُتِّحَتْ أَبْوَابُ الْجَنَّةِ ، فَلَمْ يُغْلَقْ مِنْهَا بَابٌ ، وَيُنَادِي مُنَادٍ : يَا بَاغِيَ الْخَيْرِ أَقْبِلْ ، وَيَا بَاغِيَ الشَّرِّ أَقْصِرْ ، وَلِلَّهِ عُتَقَاءُ مِنْ النَّارِ ، وَذَلكَ كُلُّ لَيْلَةٍ ) . رواه الترمذي ( 682 ) وابن ماجه ( 1642 ) . وحسَّنه الشيخ الألباني في " صحيح الجامع
Kutoka kwa Abuu Hurayrah (رضي الله عنه) kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: "Inapofika usiku wa kwanza wa mwezi wa Ramadhwaan mashaytwaan hufungwa, na majini huzuiliwa, na milango ya Moto hufungwa, haufunguliwi mlango hata mmoja humo, na Milango ya Jannah hufunguliwa, na hakuna hata mmoja unaofungwa, kisha mwenye kunadi hunadi: “Ee mtafutaji kheri, kurubia! Ee mtafuta maovu, acha! Na Allaah Anao ambao wa kuwaacha huru kutokana na Moto na hivyo ni kila usiku. [Ameisahihisha Imaam Al-Albaaniy katika Swahiyh At-Tirmidhiy (682), Swahiyh Ibn Maajah (1339), Swahiyh Al-Jaami’ (759)]

5- Kwa vile Muislamu hana budi kutawadha kwa ajili ya Swalaah zake, basi pindi akimaliza kutawadha aombe du’aa ambayo milango ya Jannah (Pepo) inakuwa wazi:

عَنْ عُمَرَ بْنِ الْخَطَّابِ (رَضِيَ اللَّه عَنْهُ) قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ (صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ): ((مَا مِنْ مُسْلِمٍ يَتَوَضَّأُ فَيُحْسِنُ الْوُضُوءَ ثُمَّ يَقُولُ: أَشْهَدُ أَنْ لاَ إِلَهَ إلاَّ اللَّهُ وَأَشْهَدُ أَنَّ مُحَمَّدًا عَبْدُهُ وَرَسُولُهُ، إلاَّ فُتِحَتْ لَهُ ثَمَانِيَةُ أَبْوَابِ الْجَنَّةِ يَدْخُلُ مِنْ أَيِّهَا شَاءَ))
Kutoka kwa ‘Umar bin Al-Khattwaab (رضي الله عنه) kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: ((Hakuna Muislamu yeyote anayetawadha akatia vizuri wudhuu wake, kisha akasema:
أَشْهَدُ أَنْ لاَ إِلَهَ إلاَّ اللَّهُ وَأَشْهَدُ أَنَّ مُحَمَّدًا عَبْدُهُ وَرَسُولُهُ،
“Ash-hadu anlaa ilaaha illa-Allaah wa ash-hadu anna Muhammadan ‘Abduhu wa Rasuwluhu [Nashuhudia kwamba hapana mwabudiwa wa haki isipokuwa Allaah, na nashuhudia kwamba Muhammad ni mja Wake na Rasuli Wake] ila atafunguliwa milango minane ya Jannah ataingia wowote apendao)) [Ibn Maajah – Swahiyh Ibn Maajah (385)]

6-Kwa vile katika Ramadhwaan Muislamu anahimizwa kuamka usiku kwa ajili ya Qiyaamul-Layl (Kisimamo cha usiku kuswali), basi anapoamka ana fadhila za kuomba du’aa:

عَنْ عُبَادَةُ بْنُ الصَّامِتِ (رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ) عَنْ رَسُولِ اللَّهِ (صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ) قَالَ: ((مَنْ تَعَارَّ مِنْ اللَّيْلِ فَقَالَ: لاَ إِلَهَ إِلاَّ اللَّهُ وَحْدَهُ لاَ شَرِيكَ لَهُ لَهُ الْمُلْكُ وَلَهُ الْحَمْدُ وَهُوَ عَلَى كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ، وَسُبْحَانَ اللَّهِ وَالْحَمْدُ لِلَّهِ وَلاَ إِلَهَ إِلاَّ اللَّهُ وَاللَّهُ أَكْبَرُ وَلاَ حَوْلَ ولاَ قُوَّةَ إِلاَّ بِاللَّهِ، ثُمَّ قَالَ رَبِّ اغْفِرْ لِي، أَوْ دَعَا اسْتُجِيبَ لَهُ، فَإِنْ عَزَمَ فَتَوَضَّأَ ثُمَّ صَلَّى قُبِلَتْ صَلَاتُهُ))
Kutoka kwa ‘Ubaadah bin Swaamit (رضي الله عنه) kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: ((Atakayeamka usiku akasema:

لاَ إِلَهَ إِلاَّ اللَّهُ وَحْدَهُ لاَ شَرِيكَ لَهُ لَهُ الْمُلْكُ وَلَهُ الْحَمْدُ وَهُوَ عَلَى كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ، وَسُبْحَانَ اللَّهِ وَالْحَمْدُ لِلَّهِ وَلاَ إِلَهَ إِلاَّ اللَّهُ وَاللَّهُ أَكْبَرُ وَلاَ حَوْلَ ولاَ قُوَّةَ إِلاَّ بِاللَّهِ، رَبِّ اغْفِرْ لِي

Laa ilaaha illa-Allaah Wahdahu laa shariyka Lahu, Lahul-Mulku wa-Lahul-Hamdu wa-Huwa ‘alaa kulli shay-in Qadiyr, wa Subhaana-Allaah wal-HamduliLLaah walaa ilaaha illa-Allaah wa-Allaahu Akbar walaa hawla walaa quwwata illa biLlaah, Rabbigh-fir-liy

(Hapana mwabudiwa wa haki isipokuwa Allaah Pekee Hana mshirika, Ufalme ni Wake na Himdi ni Zake Naye ni Mweza wa kila kitu. Ametakasika Allaah, na Himdi ni za Allaah, na hapana mwabudiwa wa haki isipokuwa Allaah, Allaah ni Mkubwa kabisa, na hapana uwezo wala nguvu ila za Allaah, ee Allaah, nighufurie) au akaomba, ataitikiwa. Na akiazimia kutawadha na kuswali atatakabaliwa Swalaah yake)) [Al-Bukhaariy na wengineo]

Na pia Allaah (سبحانه وتعالى) Huteremka kila siku thuluthi ya mwisho ya usiku kuwaitikia waja Wake du’aa zao:

عنْ أَبِي هُرَيْرَةَ (رَضِيَ اللَّهُ عَنْه)ُ أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ (صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ) قَالَ: ((يَنْزِلُ رَبُّنَا تَبَارَكَ وَتَعَالَى كُلَّ لَيْلَةٍ إِلَى السَّمَاءِ الدُّنْيَا حِينَ يَبْقَى ثُلُثُ اللَّيْلِ الآَخِرُ يَقُولُ: مَنْ يَدْعُونِي فَأَسْتَجِيبَ لَهُ ، مَنْ يَسْأَلُنِي فَأُعْطِيَهُ ، مَنْ يَسْتَغْفِرُنِي فَأَغْفِرَ لَهُ))
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Hurayrah (رضي الله عنه) kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: ((Rabb wetu Tabaaraka wa Ta’aalaa) Huteremka [kwa namna inavyolingana na utukufu Wake] kila siku katika mbingu ya dunia [ya kwanza] inapobakia thuluthi ya mwisho ya usiku na Husema: Nani ananiomba Nimtakabalie? Nani ananitaka jambo Nimpe? Nani ananiomba maghfirah Nimghufurie?)) [Al-Bukhaariy, Muslim, Abu Daawuwd, At-Tirmidhiy, Ibn Maajah, Ahmad]

Vile vile kuna Du’aa katika Saa ya usiku ambayo hairudi bali inataqabaliwa:

عَنْ جَابِرٍ (رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ) قَالَ: سَمِعْتُ النَّبِيَّ (صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّم)َ يَقُولُ: ((إِنَّ فِي اللَّيْلِ لَسَاعَةً لاَ يُوَافِقُهَا رَجُلٌ مُسْلِمٌ يَسْأَلُ اللَّهَ خَيْرًا مِنْ أَمْرِ الدُّنْيَا وَالآَخِرَةِ إِلاَّ أَعْطَاهُ إِيَّاهُ وَذَلِكَ كُلَّ لَيْلَةٍ))
Imepokelewa kutoka kwa Jaabir (رضي الله عنه) ambaye amesema: Nimemsikia Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akisema: ((Hakika katika usiku bila shaka kuna saa haimuwafikii mtu Muislamu anayemwomba Allaah khayr katika mambo ya dunia au Aakhirah ila Atampa, na hiyo ni kila usiku)) [Muslim (757), Swahiyh Al-Jaami’ (2130)]

7- Du’aa Wakati Wa Kusoma Qur-aan kwani Ramadhwaan ndio mwezi ulioteremshwa Qur-aan:

شَهْرُ رَمَضَانَ الَّذِي أُنزِلَ فِيهِ الْقُرْآنُ هُدًى لِّلنَّاسِ وَبَيِّنَاتٍ مِّنَ الْهُدَىٰ وَالْفُرْقَانِ ۚ
Mwezi wa Ramadhwaan ambao imeteremshwa humo Qur-aan ili iwe mwongozo kwa watu na hoja bayana za mwongozo na pambanuo (la haki na batili). [Al-Baqarah: 184]

Na pia Muislamu anaposoma Qur-aan, anapopitia Aayah zenye kubashiriwa Jannah, basi aiombe Jannah, na anapopitia Aayah za Moto, aombe kujikinga nao. Na anapopitia Aayah zenye maonyo ya adhabu za Allaah aombe kujikinga na adhabu za Allaah (سبحانه وتعالى) duniani na Aakhirah na aombe Rahmah za Allaah. Hivyo ni kufuata mafunzo ya Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم):

‏عن ‏حُذَيْفَةَ بِنْ اليمان (رضي الله عنه): أنَّ النَّبِيَّ‏ ‏(صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ‏) كَانَ ‏إِذَا مَرَّ بِآيَةِ رَحْمَةٍ سَألَ، وَإِذَا مَرَّ بِآيَةِ عَذَابٍاسْتَجَارَ، وَإِذَا مَـرَّ بِآيَةٍ فِيهَـا تنزيهٌ للَّهِ سبَّحَ
Imepokelewa kutoka kwa Hudhayfah bin Al-Yamaani (رضي الله عنه) kwamba Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alikuwa anapopitia Aayah ya Rahmah aliomba (Rahmah), na alipopitia Aayah ya adhabu aliomba kujikinga, na alipopitia Aayah zenye kumtakasa Allaah alimsabbih)) [Swahiyh Ibn Maajah (1119)]

Pia,
كان إذا مرَّ بآيةِ خوفٍ تعوَّذَ، و إذا مرَّ بآيةِ رَحمةٍ سألَ، و إذا مرَّ بآيةٍ فيها تَنزيهُ اللهِ سبَّحَ
Alikuwa anapopitia Aayah ya khofu, alijikinga, na alipopitia Aayah ya Rahmah aliomba (Rahmah), na alipopitia Aayah ya kumtakasa Allaah, alimsabbih)) [Swahiyh Al-Jaami’ (4782)]

Pia:

‏أَنَّهُ ‏صَلَّى إِلَى جَنْبِ النَّبِيِّ (‏صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ‏) ‏لَيْلَةً فَقَرَأ فَكَانَ إذَا مَرَّ بِآيَةِ عَذَابٍ وَقَفَ وَتَعَوَّذَ وَإذَا مَرَّ بِآيَةِ رَحْمَةٍ وَقَفَفَدَعَا
Kwamba ameswali pembeni na Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) usiku mmoja, akasoma akawa kila anapopitia Aayah ya adhabu alisita na akajikinga, na alipopitia Aayah ya Rahmah alisita akaomba. [Swahiyh An-Nasaaiy (1007)]

8-Usiku unaojulikana kwa Laylatul-Qadr, ni usiku mtukufu mno ambao humo majaaliwa ya mja yanaandikwa na pia du’aa inataqabaliwa:

عن أَبِي هُرَيْرَةَ رضي الله عنه قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم: ((مَنْ قَامَ لَيْلَةَ الْقَدْرِ إيمَانًا وَاحْتِسَابًا غُفِرَ لَهُ مَا تَقَدَّمَ مِنْ ذَنْبِهِ))
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Hurayrah (رضي الله عنه) kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: ((Atakayesimama usiku wa Laylatul-Qadr kwa iymaan na kutaraji malipo, ataghufuriwa madhambi yake yaliyotangulia)) [Al-Bukhaariy (1910) na Muslim (760)]

Na du’aa makhsusi ya Laylatul-Qadr ni kama ilivyothibiti katika Hadiyth:

عَنْ عَائِشَةَ (رضي الله عنها) أَنَّهَا قَالَتْ: يَا رَسُولَ اللَّهِ، أَرَأَيْتَ إِنْ وَافَقْتُ لَيْلَةَ الْقَدْرِ مَا أَدْعُو؟ قَالَ: ((تَقُولِينَ: اللَّهُمَّ إِنَّكَ عَفُوٌّ تُحِبُّ الْعَفْوَ فَاعْفُ عَنِّي))
Imepokelewa kutoka kwa ‘Aaishah (رضي الله عنها) amesema: Nilisema: Ee Rasuli wa Allaah! Je, nitakapojaaliwa kupata Laylatul-Qadr niombe nini? Akasema: “Sema:
اللَّهُمَّ إِنَّكَ عَفُوٌّ تُحِبُّ الْعَفْوَ فَاعْفُ عَنِّي

Allaahumma Innaka 'Afuwwun Tuhibbul-'afwa fa'-fu 'anniy. [Ee Allaah Hakika Wewe Ndiye Mwenye kusamehe Unapenda kusamehe basi nisamehe)) [Swahiyh Ibn Maajah (3119)]

Bonyeza viungo vifuatavyo uendelee kupata faida tele:

Du'aa Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)

إِيَّاكَ نَعْبُدُ وَإِيَّاكَ نَسْتَعِينُ - Wewe Pekee Tunakuabudu Na Wewe Pekee Tunakuomba Msaada

Hiswnul-Muslim: Du’aa Na Adhkaar Kusoma Na Kwa Kusikiliza (Toleo Lilohaririwa)

Sayyidul Istighfaar Du’aa Bora Kabisa Ya Kuomba Maghfirah Na Fadhila Za Kuomba Tawbah

Basi hakika Ramadhwaan ni fursa adhimu kwa Muislamu kuomba du’aa apate kutakabaliwa haja zake. Usikose kamwe kila siku kijiombea du’aa za kheri kwa ajili ya Aakhirah na dunia yako, na kuwaombea, wazazi, ndugu na jamaa na Waislamu kwa ujumla.

Ubarikiwe sana mkuu
 
Back
Top Bottom