Ramadhan Kailima: Tume ya Taifa ya Uchaguzi ni huru

Yeye nani kamteua? Je kulikuwa na uwazi kwenye uteuzi? Haramu haiwezi kuwa halali.
 
Ukiona mtu anashabikia ccm humu jua ni buku saba kwa asilimia 90 .ccm ilishakufa waliobak wachumia tumbo
 
Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Bw. Ramadhan Kailima amesema chombo anachokiongoza na kukisimamia ni Huru na wala hakiingiliwi na mtu, chama wala kikundi chochote katika kutekeleza majukumu yake kwa mujibu wa Sheria,amewataka wanasiasa wajiamini. Msikilize hapa akizungumza katika mahojiano Mubashara Dodoma FM

Mkurugenzi amenena vyema juu ya uhuru wa tume kwa mujibu wa sheria na katiba lakini hajasema mazingira yaliyopelekea uwepo wa hivyo vifungu vya katiba na sheria kwa kina.

Swali la nyongeza kwa mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi: kama kutokuhoji mahakamani katika ngazi yeyote ya mahakama matokeo ya uchaguzi ya Rais maana yake ni kuwa Tume ya Uchaguzi ya Taifa ipo huru; yaani kuhoji mahakamani ni sawa na Tume ya Uchaguzi ya Taifa sio huru. Swali: je, katiba na sheria kuruhusu kuhoji matokeo ya uchaguzi wa madiwani na wabunge mahakamani na mahakama kutoa hukumu ya aidha matokeo ni halali au sio halali maana yake Tume ya Uchaguzi ya Taifa sio huru? Kama ni huru, iweje kwenye ngazi ya Rais ionekane sio huru?

Narejea utangulizi wangu hapo juu kuwa Mhe. Mkurugenzi wa Tume ya Uchaguzi ya Taifa alitakiwa kutueleza mazingira yaliyopelekea kutungwa kwa vifungu vya katiba juu ya uchaguzi na kutungwa kwa sheria ya uchaguzi.
 
Hoja ni kwamba huyo mkurugenzi ni mteule wa rais, na rais ni mwenyekiti wa chama cha siasa ambacho kinashiriki katika chaguzi zinazo simamiwa na tume hiyo.Kinachotakiwa ni INDEPENDENT ELECTORAL COMMISSION na sio Tume ya serikali ya kusimamia uchaguzi.Kama una akili kichwani mwako, utaelewa nilicho maanisha.

Ndiyo! Na hii ni kwa Mujibu wa Katiba! unasemaje sasa maana Katiba yako ndiyo inaamua juu ya viongozi wa Tume.
 
Mkuu Upigaji wa Kura, Kuhesabu na Kutangaza matokeo ni process ambayo vyama husika wagombea na mawakala wanahusika! Hakuna rocket Science hapa mi nakumbuka 2015 vituo vya kupigia Kura baada ya kupiga kura vilitumika kuhesabia kura ambapo matokeo yaliyopatikana kwa Rais, Mbunge na Diwani yalibandikwa kituoni kuonyesha idadi ya kura alizopata kila mgombea. Na bado Mawakala walipewa copy ya matokeo na ndio maana wananchi walikua wanazunguka na mabodaboda kukusanya matokeo ya vituo hii yote ni kwamba utendaji wa mambo katika uchaguzi ulikua huru.

Kwa Tanzania Tume ndo inatangaza matokeo na process hii ilikua inahusisha ujumlishaji wa matokeo ya Kura zote halali zilizopigwa na wananchi kwa ngazi zote! kama ni Mbunge ni kura za jumla ya Kata zote zinazounda Jimbo, Kama ni Diwani hivyo hivyo kata zote na Rais Kura zote za majimbo! sasa kama unakumbuka mwaka 2015 tukio la utangazaji wa matokeo lilikua Mubashara kwa matokeo yaliyokuwa yanawasilishwa kutoka majimbo yote ya Tanzania kazi hii sio Term paper au Test.

David Kafulila na Wenje walikuwa na fomu za matokeo yote,na waliitaka mahakama iiamuru NEC ilete fomu zote za matokeo ili walinganishe matokeo waliyonayo na yale ya NEC,lakini kwa sababu serikali inafahamu kuwa wagombea wao hawakushinda kihalali mahakama zilikataa maombi hayo.

Timu ya UKAWA iliiomba NEC isitishe utangazaji wa matokeo ya urais,wakutane ili wajiridhishe kama matokeo hayo yanayotangazwa na NEC yanafanana na yale waliyoyapokea wao toka kwa mawakala wao nchi nzima,NEC walikataa,kama tume ni huru mbona huwa inakataa kila hoja inayotoa fursa ya pande zote kujiridhisha kabla ya kumtangaza mshindi?
 
Mkurugenzi amenena vyema juu ya uhuru wa tume kwa mujibu wa sheria na katiba lakini hajasema mazingira yaliyopelekea uwepo wa hivyo vifungu vya katiba na sheria kwa kina.

Swali la nyongeza kwa mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi: kama kutokuhoji mahakamani katika ngazi yeyote ya mahakama matokeo ya uchaguzi ya Rais maana yake ni kuwa Tume ya Uchaguzi ya Taifa ipo huru; yaani kuhoji mahakamani ni sawa na Tume ya Uchaguzi ya Taifa sio huru. Swali: je, katiba na sheria kuruhusu kuhoji matokeo ya uchaguzi wa madiwani na wabunge mahakamani na mahakama kutoa hukumu ya aidha matokeo ni halali au sio halali maana yake Tume ya Uchaguzi ya Taifa sio huru? Kama ni huru, iweje kwenye ngazi ya Rais ionekane sio huru?

Narejea utangulizi wangu hapo juu kuwa Mhe. Mkurugenzi wa Tume ya Uchaguzi ya Taifa alitakiwa kutueleza mazingira yaliyopelekea kutungwa kwa vifungu vya katiba juu ya uchaguzi na kutungwa kwa sheria ya uchaguzi.

Mkuu unahitaji muda kujifunza historia ya Tume ni hivi Tume ya Taifa ya Uchaguzi ilianzishwa tarehe 13 Januari, 1993, kwa mujibu wa Ibara ya 74 (1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 baada ya kurejeshwa kwa Mfumo wa Vyama vingi vya Siasa nchini Tanzania mwaka 1992.

Kwa mujibu wa Ibara ya 74 (7) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, Tume ya Taifa ya Uchaguzi ni Idara huru inayojitegemea. Aidha, Ibara ya 74(11) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inaeleza kuwa Tume katika kutekeleza majukumu yake ya Kikatiba haitalazimika kupokea maelekezo au amri kutoka kwa mtu yeyote au Idara yoyote ya Serikali au kufuata maoni ya Chama chochote cha Siasa.

Ukipitia taarifa mbalimbali utaona Majukumu ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi yameainishwa katika Ibara ya 74 (6) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, kama ifuatavyo:

(i) Kusimamia na Kuratibu Uandikishaji wa Wapiga Kura katika Uchaguzi wa Rais na Wabunge katika Jamhuri ya Muungano;

(ii) Kusimamia na kuratibu uendeshaji wa Uchaguzi wa Rais na Wabunge;

(iii) Kuchunguza mipaka na kuigawa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika maeneo mbalimbali kwa ajili ya Uchaguzi wa Wabunge;

(iv) Kusimamia na kuratibu uandikishaji wa Wapiga Kura na uendeshaji wa Uchaguzi wa Madiwani; na

(v) Kutekeleza majukumu mengine yoyote kwa mujibu wa Sheria iliyotungwa na Bunge.

Majukumu mengine ya Tume kwa mujibu wa Sheria iliyotungwa ni pamoja na yaliyotajwa katika kifungu cha 4C cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Sura ya 343, na Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa, Sura ya 292, ambayo ni:-

(i) Kutoa Elimu ya Mpiga Kura kwa nchi nzima, kuratibu na kusimamia watu wanaotoa Elimu hiyo; na

(ii) Kuteua na kuwatangaza Wabunge na Madiwani Wanawake wa Viti Maalum.
 
David Kafulila na Wenje walikuwa na fomu za matokeo yote,na waliitaka mahakama iiamuru NEC ilete fomu zote za matokeo ili walinganishe matokeo waliyonayo na yale ya NEC,lakini kwa sababu serikali inafahamu kuwa wagombea wao hawakushinda kihalali mahakama zilikataa maombi hayo.

Timu ya UKAWA iliiomba NEC isitishe utangazaji wa matokeo ya urais,wakutane ili wajiridhishe kama matokeo hayo yanayotangazwa na NEC yanafanana na yale waliyoyapokea wao toka kwa mawakala wao nchi nzima,NEC walikataa,kama tume ni huru mbona huwa inakataa kila hoja inayotoa fursa ya pande zote kujiridhisha kabla ya kumtangaza mshindi?

Ndugu yangu Haki inadaiwa Mahakamani, Kwa Mujibu wa Katiba Mahakama ndicho chombo pekee cha utoaji wa Haki hapa nchini na maamuzi yake ndiyo Alpha na Omega sasa katika hilo unataka kusema nini? kama ruling ilitolewa na Mahakama utasemaje Kafulila au Wenje Wameshinda tujifunze kukubali ukweli
 
Mkuu unahitaji muda kujifunza historia ya Tume ni hivi Tume ya Taifa ya Uchaguzi ilianzishwa tarehe 13 Januari, 1993, kwa mujibu wa Ibara ya 74 (1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 baada ya kurejeshwa kwa Mfumo wa Vyama vingi vya Siasa nchini Tanzania mwaka 1992.

Kwa mujibu wa Ibara ya 74 (7) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, Tume ya Taifa ya Uchaguzi ni Idara huru inayojitegemea. Aidha, Ibara ya 74(11) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inaeleza kuwa Tume katika kutekeleza majukumu yake ya Kikatiba haitalazimika kupokea maelekezo au amri kutoka kwa mtu yeyote au Idara yoyote ya Serikali au kufuata maoni ya Chama chochote cha Siasa.

Ukipitia taarifa mbalimbali utaona Majukumu ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi yameainishwa katika Ibara ya 74 (6) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, kama ifuatavyo:

(i) Kusimamia na Kuratibu Uandikishaji wa Wapiga Kura katika Uchaguzi wa Rais na Wabunge katika Jamhuri ya Muungano;

(ii) Kusimamia na kuratibu uendeshaji wa Uchaguzi wa Rais na Wabunge;

(iii) Kuchunguza mipaka na kuigawa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika maeneo mbalimbali kwa ajili ya Uchaguzi wa Wabunge;

(iv) Kusimamia na kuratibu uandikishaji wa Wapiga Kura na uendeshaji wa Uchaguzi wa Madiwani; na

(v) Kutekeleza majukumu mengine yoyote kwa mujibu wa Sheria iliyotungwa na Bunge.

Majukumu mengine ya Tume kwa mujibu wa Sheria iliyotungwa ni pamoja na yaliyotajwa katika kifungu cha 4C cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Sura ya 343, na Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa, Sura ya 292, ambayo ni:-

(i) Kutoa Elimu ya Mpiga Kura kwa nchi nzima, kuratibu na kusimamia watu wanaotoa Elimu hiyo; na

(ii) Kuteua na kuwatangaza Wabunge na Madiwani Wanawake wa Viti Maalum.

Kwa hiyo haya ndio mazingira yaliyopelekea matokeo ya Rais kutohojiwa mahakamani katika ngazi yoyote kwa sababu tume ni huru na wakati huo huo matokeo ya udiwani na ubunge kuhojiwa mahakamani na mahakama kutoa hukumu ya kuhalalisha au kubatilisha?

Historical context ya kurejeshwa vyama vingi ndio inahitajika hapa na wala sio historical context ya kuanzishwa kwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi.

Kwa taarifa yako ninaifahamu historical context ya kuondolewa mfumo wa vyama vingi na kurejeshwa kwake.

Sasa wewe unayejua historical context ya Tume kuanzishwa jibu swali langu hapo juu.
 
Kenya Hakuna Tume Huru maana wananchi na wanasiasa wanaipinga bado! EAC Tanzania tuko vizuri na ndio maana wanakuja kujifunza namna chaguzi za TZ zinavyoendeshwa

Wanakuja kujifunza lakini wanaishia kushangaa huu uwizi unaofanyika. Wenyewe wanasema siku Watanzania wakiacha ukondoo basi mambo yatakuwa mengine. Ki ujumla huwa wanasikitika kupoteza muda wao kuja kujifunza kwa raia makondoo wakati nchini mwao uwezo wa wananchi wao kujitambua ni mkubwa.
 
ila sisi watanzani tunapenda sana kusemasema
maneno mengi na uongo mwingi na tukibanwa tuthibitishe tunakua zero
 
Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Bw. Ramadhan Kailima amesema chombo anachokiongoza na kukisimamia ni Huru na wala hakiingiliwi na mtu, chama wala kikundi chochote katika kutekeleza majukumu yake kwa mujibu wa Sheria,amewataka wanasiasa wajiamini. Msikilize hapa akizungumza katika mahojiano Mubashara Dodoma FM

HUYU NAYE AACHE KOMEDI ZAKE NI NANI ASIYEJUA KUWA TZ. HAKUNA TUME HURU YA UCHAGUZI...UNAJUA SIJUI WATUHUVULIWA AKILI WAKATI MWINGINE WAKIONEA.
YAANI UTEULIWE NA RAIS ALAFU USEME TUME HURU WHAT IS SO FREE THERE??????????
MNATIA HASIRA NINYI,ILA NGOJA IKO SIKU MUDA UTASEMA TU...VERY SHAME..VERY MISERABLE....HUONI HATA HAYA UKIONGEA HIVI..BINAFSI NINGELIWEZA HATA KUSIMAMA MBELE NA KUONGEA LOLOTE.
 
KWANI KASEMA TUME HURU YA UCHAGUZI AU NA WEWE HUJASIKILIZA NA KUELEWA? KASEMA TUNA TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI NA AKASEMA UTENDAJI WA TUME NI HURU KWA MAANA YA KUTOINGILIWA KATIKA KAZI ZAKE.

JENGA HOJA YAKO KUTOKEA HAPO USIPOTOSHE
 
Back
Top Bottom