Ramadhan Kailima: Tume ya Taifa ya Uchaguzi ni huru

Mwakaboko King

JF-Expert Member
Apr 22, 2015
1,099
207
Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Bw. Ramadhan Kailima amesema chombo anachokiongoza na kukisimamia kinatekeleza majukumu yake kwa Uhuru na wala hakiingiliwi na mtu, chama au kikundi chochote katika kutekeleza majukumu yake ambayo yapo kwa mujibu wa Sheria, amewataka wanasiasa kote nchini wajiamini. Msikilize hapa akizungumza katika mahojiano Mubashara Dodoma FM
 
Vipi suala la Zanzibar kufutwa uchaguzi na kuitishwa kienyeji?
 
Ingefaa angesema kama haki ilifuatwa. Sio porojo za kihuni zilizofanyika ,na hata hivyo NEC hawajawahi kizungumzia chochote katika hili. Imani ni mdogo sana kwenye hekaya hizi.
 
Kairima asidhani kwamba watanzania ni mambu mbu mbu kiasi hicho ni vema akakaa kimya yeye ni nani anapingana na wasomi waliobobea wanaosema kuwa tume sio huru!
 
Kairima asidhani kwamba watanzania ni mambu mbu mbu kiasi hicho ni vema akakaa kimya yeye ni nani anapingana na wasomi waliobobea wanaosema kuwa tume sio huru!

Wakenya walipata Tume huru ila ni balaa eti hawaiamini , Tatizo wanasiasa wa Tanzania hawajiamini wanaishi kwa hisia na kuwaza kuibiwa kura. Tanzania wagombea wanaposhindwa uchaguzi, hata kama mtu kapata kura 1 na mwenzake kapata 5000 anasema wamemuibia kura wanasiasa wanatuponza sana hawaelewi siasa pia maana ya Uchaguzi.
 
Yeye kateuliwa na mwenyekiti Wa chama gani?jee Huyo aliyemteua hana mamlaka ya kumuondoa?
 
Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Bw. Ramadhan Kailima amesema chombo anachokiongoza na kukisimamia ni Huru na wala hakiingiliwi na mtu, chama wala kikundi chochote katika kutekeleza majukumu yake kwa mujibu wa Sheria,amewataka wanasiasa wajiamini. Msikilize hapa akizungumza katika mahojiano Mubashara Dodoma FM

anatii sheria kwa shuruti
 
Bongolala hakuna anayejipa Mamlaka mwenyewe! sisi wananchi ndio msingi wa Mamlaka yote ndani ya Tanzania japo najua hata hili utalipinga! huyo unayemsema sisi Watanzania tumempa mamlaka kupitia Ballot paper!
 
Tume huru Bongo! Mabilioni ya uchaguzi na ya mishahara na marupurupu ya maofisa wa tume yangetumika tuu kuiendeleza Tanzania yetu ya viwanda.
 
Back
Top Bottom